Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Mkuu hivi kujadiliana ni kuulizana maswali tu na kujibu? Nimekuuliza unataka kujua zaidi kuhusu Ruqya ili uelezwe zaidi kuhusu Ruqya maana ulikuwa unapinga kuhusu Ruqya ukataka ushahidi umepewa, ila umejibu tu sawa haujawa wazi kama umekubali kuhusu uhalali wa kisomo cha Ruqya.
Nilichojibu sawa nilikuambia hatimae umekuja na adhiko au hadithi haya tuendelee kuijadili hadithi kuhusu Rukya

Nakuuliza ni yapi masharti ya Rukya kwa mujibu wa hadithi?
 
Hapa nakubaliana nawewe hata gallow bird alisema hakuna kinga ya kuingiwa na jini nikamtalia

Hakika ukidumisha ibada hutopatwa kusumbuliwa na viumbe wabaya
Usipende kumquote mtu kwa kuondoa baadhi ya maelezo yake kisha unakuja kujibu kwa kupotosha maana. Acha ujanja ujanja.

Ibada ipi ukidumisha hutosumbuliwa na viumbe wabaya?
 
Usipende kumquote mtu kwa kuondoa baadhi ya maelezo yake kisha unakuja kujibu kwa kupotosha maana. Acha ujanja ujanja.

Ibada ipi ukidumisha hutosumbuliwa na viumbe wabaya?
Kuna ibada ngapi?
 
Nilichojibu sawa nilikuambia hatimae umekuja na adhiko au hadithi haya tuendelee kuijadili hadithi kuhusu Rukya

Nakuuliza ni yapi masharti ya Rukya kwa mujibu wa hadithi?
Hiyo maana yake bado haujakubali kuhusu Ruqya.
 
Hiyo haijaonesha masharti ya rukya, lengo ni kujua kama ni shirki au sio maana hilo ndio tunalo jadili hapa
Unakumbuka ulichokuwa unapinga? Ulisema Ruqya haijathibit, ndio maana ya kupewa hiyo hadith kuonyesha uhalali wa Ruqya.

Sasa suala la masharti ya Ruqya huko ni suala la kutaka kujua Ruqya iliyo sahihi ndio maana nikakuuliza unataka kujifunza zaidi kuhusu Ruqya?
 
Aliesema kuwa hadithi ni porojo sio Mimi mkuu tuendelee na mjadala
Yeye haamini hadithi ndio maana akakwambia wewe kuwa hadithi ni porojo, ila wewe unaamini hadithi na ulitaka ushahidi wa aya au hadithi.
 
Kusoma na kusomewa kuna matokeo tofauti katika kujenga Imani ya msomaji na msomewa, mtu akisoma kwa ufahamu hawezi fanya shirki
Ndio maana nikakwambia umeelewa lakini iyo hadithi niliyokupa ?
Sasa wewe utakuwa na uhakika gani kuwa huyu anayepiga adhana kwa kumtegemea ALLAH na sio hiyo adhana, Mpaka umuhukumu anafanya shirki?
Kwamaana hiyo unataka kusema kuwa yule swahaba alifanya shirki ? na Mtume akakubali kupokea kondoo zinazotokana na shirki.?
 
Kwanini usimfundishe afanye mwenyewe yani umfunfishe hizo surah na Aya asome mwenyewe kuliko kumsomea, kwahiyo unamuingiza mtu katika shirki ukitarajia wewe utaachwa huru na hiyo shirki?
Na mnatumia hiki kigezo kuwafunga watu midomo kuongelea mas'ala ya shirki ndio maana imeenea siku hizi na inafanywa na watu wakubwa katika dini
Kwani uislamu umekataza kumsomea mtu akhy ? kama ndio nipe dalili , Kama hapana basi hakuna ubaya kumsomea mtu. Au kumsomea mtu nayo ni shirki?
Mimi sitetei shirki(ALLAH ATUKINGE SOTE) Ila kwanini mambo ambayo siyo shirki yanatiwa shirki kwa kufuata misimamo ya watu tu, Dini ipo katika mfumo wa elmu na sio misimamo, Madhara ya kusoma misimamo badala ya elmu ndio haya ya kuja kusema kupiga adhana kwa ajili ya kufukuza mashetani ni shirki.
Yapo mambo mengi tu ambayo yapo wazi kuwa ni shirki lakini sio hili la adhana kila kitu tukipe haki yake akhy.
 
Mkuu ngoja nikusaidie kidogo kwenye huu utata, mfano wakristo na waislamu humtambua Yesu kitofauti sana kiasi kwamba wakristo hufikia hadi kusema yule aliyeelezwa kwenye Qur'an sio Yesu ni mtu mwengine kabisa. Sasa linapokuja suala la majini napo ni hivyo hivyo, waislamu wanawaeleza majini kama viumbe ambavyo vimeumbwa na Mungu na kwamba hivyo viumbe sio malaika wala sio binaadamu ila wakristo wanawaeleza majini kuwa ni kundi tu la malaika na si kwamba ni aina tofauti ya viumbe vilivyoumbwa na Mungu.

Kwahiyo hapo kuna utofauti mkubwa, ndio maana mkristo anashangaa inawezekana vp kundi la malaika waliyoasi kusema miongoni mwao wapo wema? wakati huo huo waislamu nao wanashangaa inawezekana vp malaika kumuasi Mungu?

Kwahiyo mwisho wa siku wakristo wanawazungumzia majini kama malaika na waislamu wanawazungumzia majini kama viumbe wengine kabisa.

Kwa upande wa Yesu Kristo wa kwenye maandiko matakatifu na Isa wa Quran, hao ni watu wawili tofauti kabisa kwa kuzitazama historia zao kutoka vitabu vinavyowaelezea

Yesu Kristo kwenye maandiko ana sifa hizi kihistoria
1. Alizaliwa Bethlehem kwenye hori la Ng'ombe
2. Mama yake ni Maria ambaye hatajwi kuwa na kaka ila dada ambaye alikuwa ni mke wa Klopa; Yohana 19:25
3. Alisukibiwa akafa, akazikwa, akafufuka, akapaa mbinguni.

Yesu wa Quran ana sifa hizi kihistoria
1. Alizaliwa chini ya mtende karibu na kijito mahali ambapo hapajatajwa kuwa ni wapi.
2. Mama yake ni Mariamu ambaye anatambulishwa kama mdogo wa Musa.
3. Hakusulubiwa ila Allah (Huyu sio YHWH wa maandiko matakatifu maana wana sifa tofauti) alimtorosha akamficha, akamweka mtu mwingine mahali pake ndio akasulubiwa na kufa.

Ngoja nisitumie muda mwingi hapo kwa Yesu, ngoja niendelee na mada. Kuhusu majini maandiko hayaonyeshi popote pale kuwa mbinguni kwa Mungu Baba kuna viumbe vyovyote vya mfanano na majini kwa haiba. Majini yote hutambuliwa kuwa nii mapepo na kazi zao ni kusababisha uharibifu kiroho. Hakunaga majini wazuri na wabaya; wote ni wabaya kwakuwa asli yao ni uovu. Majini huonekana mazuri kwa watu ambao wana mission ya kufanana na yao ambayo ni uasi na kupingana na mpango wa Mungu juu ya maisha ya wanadamu.
 
Zipo nyingi tu kama ibada ya swala,swaum,Hijja,Zakka na nyengine nyingi.
Dumu nazo hizo zote ongezea na DHIKRI, dua, sadaka, kumtendea wema ndugu au jirani yako, kuondoa mwiba ulio barabarani na kuuweka kando n.k n.k, pia jiepushe na shirki na riya mwili wako utakuwa na ulinzi madhubuti hakuna kiumbe atakae kugusa na kapu la yote hayo ni SWALAA,
Allah anasema (Ankabut)
29:45 - SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini KUMDHUKURU Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.
 
Unakumbuka ulichokuwa unapinga?
Sikupinga ila nilitaka ulete andiko na nikasema kitu kama hakina uthibitisho maana yake sio sahihi hatimae umeleta
suala la masharti ya Ruqya
Hiyo hadithi sio kuwa nilikuwa siijui ila nilihitaji uilete na umeileta haya na tuijadili ili tuone kinachofanyika katika Rukya za masheikh ni shirki au sio shirki?

Hivyo basi nipe na Hadith au andiko la masharti ya rukya ili tuendelee
 
Unaweza kulithibitisha hili ?
Uthibitisho ni kuwa wanaogangwa kwa Adhana sio wote ni waislam au wamesoma dini nawewe pia umelielezea hili kwa kutumia hadithi ileile
 
Kwani uislamu umekataza kumsomea mtu akhy ? kama ndio nipe dalili , Kama hapana basi hakuna ubaya kumsomea mtu. Au kumsomea mtu nayo ni shirki?
Hoja sio kuwa kumsomea mtu ni shirki,

Hoja imetokana na wewe kusema kwakuwa wewe msomaji unaitakidi kwa Allah na sio Adhana hivyo hata huyo unaemsomea asipoitakidi kwa Allah na akiitakidi katika Adhana au msomaji wewe msomaji haikuhusu kwa maana yeye ndio anakuwa mshirikina ila sio wewe, yani umtumbukize mwenzio katika shirki na wewe uwe salama?

Na hapo ndio utajua kuiepuka shirki kwa kuganga na Adhana ni kitu ambacho uwezekano wake ni mdogo sana kwa kuzingatia masharti na nature ya waaguliwa na muaguaji
 
Kwa upande wa Yesu Kristo wa kwenye maandiko matakatifu na Isa wa Quran, hao ni watu wawili tofauti kabisa kwa kuzitazama historia zao kutoka vitabu vinavyowaelezea

Yesu Kristo kwenye maandiko ana sifa hizi kihistoria
1. Alizaliwa Bethlehem kwenye hori la Ng'ombe
2. Mama yake ni Maria ambaye hatajwi kuwa na kaka ila dada ambaye alikuwa ni mke wa Klopa; Yohana 19:25
3. Alisukibiwa akafa, akazikwa, akafufuka, akapaa mbinguni.

Yesu wa Quran ana sifa hizi kihistoria
1. Alizaliwa chini ya mtende karibu na kijito mahali ambapo hapajatajwa kuwa ni wapi.
2. Mama yake ni Mariamu ambaye anatambulishwa kama mdogo wa Musa.
3. Hakusulubiwa ila Allah (Huyu sio YHWH wa maandiko matakatifu maana wana sifa tofauti) alimtorosha akamficha, akamweka mtu mwingine mahali pake ndio akasulubiwa na kufa.

Ngoja nisitumie muda mwingi hapo kwa Yesu, ngoja niendelee na mada. Kuhusu majini maandiko hayaonyeshi popote pale kuwa mbinguni kwa Mungu Baba kuna viumbe vyovyote vya mfanano na majini kwa haiba. Majini yote hutambuliwa kuwa nii mapepo na kazi zao ni kusababisha uharibifu kiroho. Hakunaga majini wazuri na wabaya; wote ni wabaya kwakuwa asli yao ni uovu. Majini huonekana mazuri kwa watu ambao wana mission ya kufanana na yao ambayo ni uasi na kupingana na mpango wa Mungu juu ya maisha ya wanadamu.
Sasa upi mfanano kati ya majini wa kwenye biblia na kwenye qur'an?

Maana majini wa kwenye Qur'an ni viumbe ambavyo Mungu kaviumba hivyo si katika malaika wala binaadamu, ila majini wa kwenye biblia ni sehemu ya malaika hivyo biblia haisemi kwamba Mungu aliumba viumbe vyenye kuitwa majini.

Ibilisi hutambulika alikuwa malaika akamuasi Mungu, ila waislamu humtambua Ibilisi kuwa ni jini na si malaika na kwamba malaika huwa hawamuasi Mungu.

Mpaka hapo mkuu kipi kinakufanya uone majini wenyekuzungumziwa na Qur'an ndio hao hao wenye kuzungumziwa na biblia pamoja na hizo tofauti?
 
Back
Top Bottom