Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Ulivyosema hakuna ithibati ya Ruqya ulikuwa umekusudia nini?
 
Kwahiyo unachosema inatakiwa muislamu afanye ibada zote kwa ujumla wake hadi kuondoa jiwe njiani hapo ndio atapata ulinzi?
 
Nionavyo mimi, Uislam uko karibu sana na ushirikina, uchawi na uganga.
 
Nilikusudia ulete andiko kuthibitisha maana ulikuwa waongea maneno tu bila ushahidi
Kwahiyo nisingeleta ingebaki kauli yako kwamba Ruqya haina ithibati kwamba ushahidi wa Ruqya.
 
Kwahiyo nisingeleta ingebaki kauli yako kwamba Ruqya haina ithibati kwamba ushahidi wa Ruqya.
Unaongea bila uthibitisho yani unatoa kichwani na yenyewe umeleta hadithi moja ya kuokoteza hadi sasa

Kuleta nyingine au andiko kuhusu masharti ya Rukya hutaki maana unajua itakavyokuwa kwa uganga unaofanywa na masheikh unaangukia kwenye shirki haukidhi vigezo vya Rukya unayopigia gitaa hapo
 
Lakini mwanzoni ulisema ni shirki.
sasa hivi unasema tena kutokana na mimi nilivyosema, Mimi nimeeleza kidogo tu kuhusu shirki ilivyokuwa pana, Unafikiri hata wewe unavyodai mtu afundishwe ajisomee mwenyewe hawezi kufanya shirki ?.
Wewe unaweza kumfundisha vizuri kabisa kuwa ajisomee qur an na awe na itakidi kuwa anayeponya ni ALLAH apo wewe umemaliza kwa upande wako suala linabaki kwake je yeye atafanya hivyo au ataitakidi tofauti.
 
Lakini mwanzoni ulisema ni shirki.
Na hata andiko langu limejikita hapo ila wewe ndio ukaelezea na kusema shirki ni pana ila ukweli kumsomea mtu ni shirki hasa kwa waganga hawa wa kiafrika ila tukizungumza hayo mnakuja na utetezi wa kuwa shirki ni jambo kubwa kwahiyo tusiwaseme kuwa wanafanya shirki
Wewe unaweza kumfundisha vizuri kabisa kuwa ajisomee qur an na awe na itakidi kuwa anayeponya ni ALLAH apo wewe umemaliza kwa upande wako suala linabaki kwake je yeye atafanya hivyo au ataitakidi tofauti.
Ni bora umfundishe asome mwenyewe na ajue jinsi ya kujikinga na madhara yatokayo na majini kuliko kufanya kitengo cha uganga na kuwasomea wenye majini tena kwa Adhana eti wanaagua majini. Na siku hizi hadi matangazo wanatoa kabisa halafu tukisema ni shirki tunaambiwa tunahukumu yani tusizungumze kabisa kuhusu shirki maana tukizungumza tunahukumu
 
Haya lete wewe basi hadithi sahihi yenye kueleza masharti na vigezo vya Ruqya unayoisema wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…