Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Kuomba kwa namna ipi? Yani kwa mfano mie nikienda kumuomba mtu anisaidie pesa au tatizo langu?
Hapana sio kuomba kwa namna hiyo

Hapa Ina maana ya kuomba kiroho au kuabudu mfano unaenda kuliomba kaburi la mzee wako ili kutatua matatizo yanayokupata

Au kuomba viumbe vingine vya Mwenyezi Mungu kwa namna hiyo
 
Wanakuaga waganga wazuri Sana Mimi waislamu nawapendea hapo tuu wanatoa waganga wazuri sana
Wanachokifanya ni kinyume na maamlisho na siku ya kiyama watapata adhabu kali, Mwenyezi Mungu anasema katika Surat-mubayyina

98:6 - Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
 
Hapana sio kuomba kwa namna hiyo

Hapa Ina maana ya kuomba kiroho au kuabudu mfano unaenda kuliomba kaburi la mzee wako ili kutatua matatizo yanayokupata

Au kuomba viumbe vingine vya Mwenyezi Mungu kwa namna hiyo
Tuache suala la kuabudu mi naulizia kuhusu kuomba, hapo kwenye kuomba kiroho ndio sijapaelewa vizuri. Kwahiyo kiujumla ni maombi ya vp huruhusiwa ambayo hayana sura ya kumshirikisha Mungu?
 
Tuache suala la kuabudu mi naulizia kuhusu kuomba, hapo kwenye kuomba kiroho ndio sijapaelewa vizuri. Kwahiyo kiujumla ni maombi ya vp huruhusiwa ambayo hayana sura ya kumshirikisha Mungu?
Maombi na sala au toba zote zinatakiwa ziwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tofauti na hapo ni ushirikina

Umepata tatizo muombe Mungu akutatulie tatizo lako usiombe mizimu, majini, mawe au binadamu mwenzio maana kuna baadhi ya watu hufanya sala na maombi kwa binadamu wenzao kutatua changamoto za kiroho

Bado hujaelewa kiongozi! Kama hujaelewa nipe mfano wako nikufafanulie
 
Shirki na Uislamu hamuwezi kutengenishwa
 
Bado najaribu kukuelewa mkuu, kuna maneno umetumia kama kuomba kiroho na changamoto za kiroho bado sijaweza kuyaelewa. Nilitoa mfano kumuomba binaadamu mwenzangu anisaidie pesa au tatizo langu ukasema hiyo sio kosa bali kinachokatazwa ni kuomba kwa kiroho ambapo sijaelewa kuomba kwa kiroho ndio kuna maana ipi tofauti na huo mfano niliyotoa?

Lakini umekuja tena kusema maombi yote ya changamoto za kiroho aombwe Mungu tu na kiumbe au kitu chochote, sijajua hizo changamoto za kiroho kama zipi hasa ndio huo uchawi au kuna zaidi?
 
Ok nakupa mfano mwingine au narudia

Mfano ni kuomba mizimu ukupatie mvua

Mfano ni kumuomba Yesu akuponye magonjwa na changamoto za kifedha

Mfano ni kuomba kwa jina la rais wako akuletee mvua au akuponye na mabalaa

Kama na hapo hujaelewa wengine watakuja kukuelewesha
 
UISLAM na UCHAWI,,mpaka wake ni mwembaba kama wembe
 
Walawi 17:7

7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.

Mambo ya Walawi 19:31
“Msijigeuze kuwa na watu wenye pepo, wala kwa wachawi; msiwatafute ili mtiwe unajisi nao; Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.”

Mambo ya Walawi 20:6
“Na mtu atakayejigeuza kwenda kwa watu wenye pepo na kwa wachawi, ili azini nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake.”

Kumbukumbu la Torati 18:10-12
“Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake motoni, wala atakayejua uganga, wala mchawi, wala mshetanishi, wala mtu awaye yote aulizaye pepo, wala mchawi, wala aulizaye wafu. Kwa kuwa mtu atendaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana...”

Isaya 8:19
“Nao watakapokuambia, Tafuteni habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi, waliao na kunong’ona; je! watu hawatatafuta habari kwa Mungu wao? Je! watawaendea wafu kwa ajili ya walio hai?”

7. Ufunuo 21:8
“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu wote, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti...”
 
Mimi ni Mkristo, lakini wewe mleta mada unawafahamu vizuri waKristo unawafahamu vizuri kabisa? Na viongozi wao unawafahamu vizuri?

Ungewafahamu basi ungewajumuisha kwenye bandiko lako...!

Na waKristo ni wabaya kuliko waIslam, usiniulize kwanini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…