mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 32,095
- 39,619
Jambo jema ukiwa mganga wa kikristo hutumii biblia kutibu.Sio uislam tu hata ukristo
Jambo jema ukiwa mganga wa kikristo hutumii biblia kutibu.Sio uislam tu hata ukristo
Wanatumia tu , mafuta ya upako, chumvi , maji , na nkJambo jema ukiwa mganga wa kikristo hutumii biblia kutibu.
soma QRAN TUKUFU "suratul jinn"Kwanini, unaweza kutoa hata sababu moja au mbili zilizofanya uje na hilo hitimisho
Kwani waganga wote ambao ni waislamu hutumia kitabu? Navyojua kuna uganga wa majini,tunguli na vitabu. Ila pia mkuu hata maandiko ya biblia hutumika kufanyia uganga hasa Zaburi.Jambo jema ukiwa mganga wa kikristo hutumii biblia kutibu.
Mkuu hauoni kama kutaja shirki ni rahisi kuliko kuelezea ni ipi hasa hiyo shirki na ipi sio shirki?Ok nakupa mfano mwingine au narudia
Mfano ni kuomba mizimu ukupatie mvua
Mfano ni kumuomba Yesu akuponye magonjwa na changamoto za kifedha
Mfano ni kuomba kwa jina la rais wako akuletee mvua au akuponye na mabalaa
Kama na hapo hujaelewa wengine watakuja kukuelewesha
Unawaonea Bure mashehe. Mfumo mzima wa dini hiyo ndivyo ulivyo. Kitendo Cha kukubali kuwa na Imani Moja na majini ambayo ndiyo baba wa ushirikina duniani ndio kosa kubwa. Fanya tafiti Kila nje ya nyumba zao za ibada Kuna waganga wa kienyeji na machupa chupa yaadawa ya kienyeji mengi ni Yale yanayoua figo na moyo eti waongeze nguvu za kuwatosheleza wake 4 na vimada lundo. Mwisho wa siku wanaishia dialysis na moyo kusimama wakiwa guestKuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.
Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki
Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim
98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,
98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,
98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka
98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?
Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.
Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama
NB, tujadili kistaarabu
Hakuna hicho kitu,hakuna mganga yeyote utakuta anakusomea bible wala kuihusisha na hayo madude.Kwani waganga wote ambao ni waislamu hutumia kitabu? Navyojua kuna uganga wa majini,tunguli na vitabu. Ila pia mkuu hata maandiko ya biblia hutumika kufanyia uganga hasa Zaburi.
Wagalatia mlio wengi hamna elimu juu ya majini kwenye hili mnahitaji darsaUnawaonea Bure mashehe. Mfumo mzima wa dini hiyo ndivyo ulivyo. Kitendo Cha kukubali kuwa na Imani Moja na majini ambayo ndiyo baba wa ushirikina duniani ndio kosa kubwa. Fanya tafiti Kila nje ya nyumba zao za ibada Kuna waganga wa kienyeji na machupa chupa yaadawa ya kienyeji mengi ni Yale yanayoua figo na moyo eti waongeze nguvu za kuwatosheleza wake 4 na vimada lundo. Mwisho wa siku wanaishia dialysis na moyo kusimama wakiwa guest
Ndy uislam na uganga ni vitu viwili tofauti uganga/uchawi ni shirkiHivi kwani uganga unatenganishwa na uislam? Maana huku huwa naona wahuni wakiamua kuwa waganga wanaslimu kabisa. Tena baadhi wanajenga na misikiti midogo nyumbani!
Ni kumshirikisha mwenyezi mungu na kitu chochote,mfano kuomba kupitia makaburi ya mababu zetu,kuomba kupitia miti,kuomba kitu kwa mungu kupitia kitu kingine,kiumbe kingine.ni kumshirikisha munguHivi ushirikina ni nini?
Yaani tukomae na uarabu tuachane na Uafrika wetu? Hapa ndipo tulipopigwa za uso na hawa watu weupeTufuateni mafundisho ya dini tuache kuchanganya na uafrika wetu
Mkuu dini hailazimishwi ila ukiamua kuifuata ifuate kama ilivyoelekezwa haitakiwi kuchanganyaYaani tukomae na uarabu tuachane na Uafrika wetu? Hapa ndipo tulipopigwa za uso na hawa watu weupe
Nukuu nzuri kiufupi hakuna dini inayoruhusu uchawi na uganga hizo ni mila zetu waafrika ambazo hatukubali kuziacha lakini pia mafundisho ya dini nayo tunayaelewa na pepo tunaitaka na siku zote haki na batili havichangamaniWalawi 17:7
7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.
Mambo ya Walawi 19:31
“Msijigeuze kuwa na watu wenye pepo, wala kwa wachawi; msiwatafute ili mtiwe unajisi nao; Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.”
Mambo ya Walawi 20:6
“Na mtu atakayejigeuza kwenda kwa watu wenye pepo na kwa wachawi, ili azini nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake.”
Kumbukumbu la Torati 18:10-12
“Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake motoni, wala atakayejua uganga, wala mchawi, wala mshetanishi, wala mtu awaye yote aulizaye pepo, wala mchawi, wala aulizaye wafu. Kwa kuwa mtu atendaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana...”
Isaya 8:19
“Nao watakapokuambia, Tafuteni habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi, waliao na kunong’ona; je! watu hawatatafuta habari kwa Mungu wao? Je! watawaendea wafu kwa ajili ya walio hai?”
7. Ufunuo 21:8
“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu wote, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti...”