Hili swala la Uamsho mimi nalirudisha nyuma kidogo kipindi cha Big Ben mwaka 2000 kipindi cha uchaguzi mkuu kama utakumbuka vizuri kuna watu wengi sana waliuwawa na wengine waliofanikiwa kutoroka walitorokea Shimoni(Mombasa). Hawa watu hawakukaa kimya kama tunavyodhani, ama usione walikotokea hao Masheikh ni coincidence. Haya mambo yalishapangwa kitambo na yalikuwa yanasubiri muda ujiri, yakamilike.
Nakumbuka mwaka 2015 Maalim Seif katika moja ya hotuba zake akiwa ni mgombea wa urais Z'bar alisema kwa uwazi kabisa, atapokuwa rais, jambo la kwanza ndani ya siku 100 za uongozi wake ni kuuvunja Muungano ili Z'bar iwe na mamlaka kamili. Isingekaa kuja kutokea Maalim Seif kuja kuwa rais wa Z'bar, huu ulikuwa ni mkakati wa muda tu wala mtu wa kinasaba chake kuja kuwa Rais hapo.
Hawa watu walichokuwa wanakifanya ni kuwalainisha Wazanzibari kwa lugha laini yenye utamu wa Asali na kuificha shubiri mwisho kabisa kwa kivuli cha Uislam na kuukataa ukafir wanaotendewa kama walivyokuwa wanahubiri. Hawakuwa wanaishia hapo tu kwan walitaka Pwani yote ya Bahari ya Hindi iwe chini ya Dola moja ya kiislam iongozwe na Sharia
Kitu kama hukijui, omba usaidiwe kukifahamu, sio ugonjwa. Kundi lililofanya ushenzi Kibiti, lililomtoa IGP Mangu, lile la mapango ya Amboni, kuna lipo lilikuwa Arusha na Mwanza yote yalinyamazishwa ila kuna kitu mpaka leo bado kinatupa mashaka. Kuna watoto zaidi ya 500 hapo Mkuranga na maeneo jirani walipotea, nikisema watoto sio wa shule ya msingi, wengi walikuwa wanaanzia umri wa miaka 14 mpaka 17.