Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Hoja za msingi sana.[emoji117]Unakaa jela zaidi ya miaka 9, unateseka weee familia inakosa huduma yako kwa muda wote huo
[emoji117]Baada ya miaka mingi kupita DPP Anafuta kesi yako na kukuruhusu uende nyumbani
[emoji117]Unaenda nyumbani ukiwa umeathirika kisaikolojia, biashara zako/kazi zinakuwa zimekufa na muda mwingine huna pesa kabisa hivi unaishije?
[emoji117]Huwa kuna kesi hazina dhamana mtu anakaa jela wee halafu baadae anashinda kesi au DPP anafuta hiyo kesi huyu nae anaambiwa aende nyumbani tu huko anaenda kuishije?
[emoji117]Wataalamu hebu mnisaidie huwa wanapewa pesa kufidia muda walio kaa gerezani?au wanaachwa tu? Kama wana waachwa tu hili liangaliwe wawe wanapewa fidia
[emoji117]Mtu anakaa gerezani miaka sita mfano kesi ikiwa anaendelea mwaka wa saba anapewa hukumu ya kufungwa miaka 15 jela (mfano).. Je, kuna fidia ya ile miaka sita aliyo kaa kabla ya hukumu?
~Karibuni
Tujadili.