Hoja za msingi sana.

Tujadili.
 
..Mama Samia asipojihusisha na UKATILI ataacha legacy kubwa kuliko Magufuli. Watz ni watu rahisi sana kuwaridhisha.
Hakika mkuu.

Tunamuombea kwa Mungu awe msikivu na mnyenyekevu hivi hivi. Asijikweze na kujiona Mungu mtu. Ajue ataulizwa na dunia ni mapato tu.

Leo usiku ntaamka niswali swala maalum ya kumuombea yeye tu.
 
..umfanyie DUA mikono yake isichafuke kwa damu za Watz wasio na hatia, pamoja na kashfa za ufisadi na rushwa.
 
Haswaaa.

Mtu akituhumiwa basi wachukue pasi ya kusafiria, na vitu vyake muhimu vizuiwe ila uhuru wake aachiwe.

Haya ni maoni yangu tu, upelelezi haujakamilika ni sababu ya kipuuzi na kiuonevu juu ya watuhumiwa
 
Very well said kiongozi.

Kama lilivyosikilizwa hili na serikali yetu sikivu ikiongozwa na Mama yetu Mheshimiwa rais Mama Samia Suluhu Hassan, ndivyo tunavyoamini kwamba hata la katiba mama amelisikia na analifanyia kazi.

Ndio maana tunasisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Wana roho mbaya sana hao, wabadilike sasa!!
 
aka kamama katakuja kutupeleka pabaya watu walikuwa na mashtaka ya wazi kabisa hata rohoni mwake huyu rais uchwara anajua walitenda
 
aka kamama katakuja kutupeleka pabaya watu walikuwa na mashtaka ya wazi kabisa hata rohoni mwake huyu rais uchwara anajua walitenda
Raisi Samia Suluhu anafuata Sheria, ninyi mlozowea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi, ni zamu yenu sasa mutafute Nchi inayotawaliwa na Dikteta muhamie na Magodoro yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…