Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Msiione haki kwa upande mmoja tu kutaka nyie mpewe zaidi ya wengine, huo ni ubinafsi, aina ya mahubiri mliyotoa yalihamasisha chuki zilizowaumiza wengine ambao nao wana haki zao, baada yenu kuwekwa ndani hali ikatulia.

Mkajifunze kuheshimu haki za wengine kama nyie mnavyotaka haki zenu ziheshimiwe, msijione bora zaidi ya wengine mpaka kuwasababishia maumivu ya aina yoyote.

Mmefurahi kutoka jela ila mjue sasa mna jukumu la kulinda raia wengine wasio wa imani kama yenu, muache mihemko, fanyeni yenu muwaache nao wafanye yao kwa uhuru wao, hii Tanzania ni yetu sote, hakuna alie juu ya mwingine wala hatakuwepo.

Naunga mkono hoja, jamii ina changamoto nyingi sana zinazohitaji mafundisho ili kuzitatua kuliko, kung'ang'ana kufundisha chuki dhidi ya wengine.

Kwa uchache tu, sasa wana kazi ya kuwafundisha vijana kuacha, zinaa, wanaume kuwa waaminifu kwa wake zao na kutunza familia, jamii iepuke wizi, rushwa, madawa ya kulevya, ulevi, mauaji, uchawi n.k.

Pia wakiwahamasisha wanajamii kupendana na kusameheana lea kweli Mwenyezi Mungu atawarehemu na kuwapa barka nyingi katika maisha haya na ahera.

Bismillahir Rahmaanir Rahiim
 
Maskini machozi ya yule padre aliyemwagiwa tindikali, yule shehe mwenye asili ya tanga aliyemwagiwa tindikali, yule polisi aliyechinjwa hapo mwanakwwrekwe, wataliinwaliokuwa wanamwagiwa tindikali, makanisa yaliyokuwa yanachomwa , bar, pamoja na mabucha ya kitimoto🙆‍♂️🙆‍♂️
Strong feelings!
 
Kuna miCCM itataka kupata ujiko kwenye hili, wakati vyama vya upinzani vilipigia kelele sana kushinikiza serikali itende haki
 
Hongera sana Shehe Ponda ni wewe pekee kati ya wachache tulikusikia ukipaza sauti kwa uwazi bila ya kutetereka tikea yule aliepelekewa akae nao hajaaiaga dunia. Bila ya kuwasahau mashehe wengine waliopo vizuizini kwenye mikoa mbalimbali na pale arusha ambapo uwazi wake upo kweupe kabisa.
 
Ni bora walikuwa mahubusu kwenye utawala wa mwisilamu mwezao ingekuwa utawala wa mkristo yaani hapo yangeongelewa mengi hata mdoa ya muungano ungetikiswa kwa kiasi kikubwa
 
Umenena vyema sana. Na Mungu akujaze hekima zaidi

Back
Top Bottom