Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

SHEIKH MSELEM SHEIKH FARID WAKO NYUMBANI ZANZIBAR

Masheikh zetu wawili wako majumbani kwao na familia. Tutaendelea kukupeni taarifa awamu kwa awamu.

Lengo ni kutoa taarifa za kweli na zilizozingatia mambo yote muhimu.

Aidha viongozi wa Shura Taifa wako angani wakielekea Zanzibar.

Ibrahimu Zuberi Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania
0713118812

=======

Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu ameieleza Mwananchi Digital leo Jumatano Juni 16, 2021 kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Wawili hao ambao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana jioni zikieleza kuwa viongozi hao wawili ndio wameachiwa huru na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro amelieleza Mwananchi Digital kuwa wameshapelekwa majumbani mwao.

Katika ufafanuzi wake Mwakitalu amesema, “ni kweli wameachiwa huru. Nimewafutia wote mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Sasa suala la kutoka gerezani kama wameshatoka wote au wangapi hilo ni suala la taratibu za Magereza lakini mimi nimewafutia mashtaka wote.”

Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kujihusisha na makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002 Januari 2013 na Juni 2014.

Awali walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua za awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji kamili wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 25.

Lakini Aprili 23, 2021 Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka 14 baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wao, Daimu Halfani, Juma Nassoro, Jeremiah Mtobesya na Abubakar Salum kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yanadaiwa kutendeka Zanzibar.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake huo uliotolewa na Jaji Mustapha Ismail baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hoja za pingamizi la utetezi na majibu ya upande wa mashtaka ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga akisaidiwa na wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Paul Kadushi, ilikubaliana na hoja za utetezi.

Jaji Ismail alisema pamoja na mambo mengine kuwa kwa makosa ambayo yanadaiwa kutendeka Zanzibar, jukwaa sahihi la kuwashtaki washtakiwa ni katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Ismail aliuamuru upande wa mashaka kufafanua marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuyaondoa mashtaka hayo na kubakiza yale ambayo yamedaiwa kutendeka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara ambayo ndio mahakama hiyo ina uwezo wa kuyasikiliza.

Zaidi, soma: Sheikh Ponda ampongeza Mkurugenzi mpya wa mashtaka(DPP) kukutana na Masheikh wa Uamsho Gerezani
Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 
Mkawashauri sasa hao Masheikh wenzenu waishi kama dini yenu inavyotaka. Yale masuala ya kuhamasisha vurugu, utengano kwa kuwaumiza watu wasio na hatia, kumwagia watu wa imani tofauti tindikali, nk. Yalikuwa yanakiuka kabisa uvumilivu wa kiimani.
Nyamazisha bakuli hilo.

Si mlisema wanatakiwa wasitoke milele????

Tuacheni tunaandaa sherehe maalum Zanzibar huku.
 
Msiione haki kwa upande mmoja tu kutaka nyie mpewe zaidi ya wengine, huo ni ubinafsi, aina ya mahubiri mliyotoa yalihamasisha chuki zilizowaumiza wengine ambao nao wana haki zao, baada yenu kuwekwa ndani hali ikatulia.

Mkajifunze kuheshimu haki za wengine kama nyie mnavyotaka haki zenu ziheshimiwe, msijione bora zaidi ya wengine mpaka kuwasababishia maumivu ya aina yoyote.

Mmefurahi kutoka jela ila mjue sasa mna jukumu la kulinda raia wengine wasio wa imani kama yenu, muache mihemko, fanyeni yenu muwaache wengine wafanye yao kwa uhuru wao, hii Tanzania ni yetu sote, hakuna alie juu ya mwingine wala hatakuwepo.
Hili ni wengwe tu. Haki gani unaoizungumzia wewe.

Shukran Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan.

Madai ya Muungano yapo pale pale.
 
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

SHEIKH MSELEM SHEIKH FARID WAKO NYUMBANI ZANZIBAR

Masheikh zetu wawili wako majumbani kwao na familia. Tutaendelea kukupeni taarifa awamu kwa awamu.

Lengo ni kutoa taarifa za kweli na zilizozingatia mambo yote muhimu.

Aidha viongozi wa Shura Taifa wako angani wakielekea Zanzibar.

Ibrahimu Zuberi Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania
0713118812

=======

Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu ameieleza Mwananchi Digital leo Jumatano Juni 16, 2021 kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Wawili hao ambao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana jioni zikieleza kuwa viongozi hao wawili ndio wameachiwa huru na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro amelieleza Mwananchi Digital kuwa wameshapelekwa majumbani mwao.

Katika ufafanuzi wake Mwakitalu amesema, “ni kweli wameachiwa huru. Nimewafutia wote mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Sasa suala la kutoka gerezani kama wameshatoka wote au wangapi hilo ni suala la taratibu za Magereza lakini mimi nimewafutia mashtaka wote.”

Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kujihusisha na makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002 Januari 2013 na Juni 2014.

Awali walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua za awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji kamili wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 25.

Lakini Aprili 23, 2021 Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka 14 baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wao, Daimu Halfani, Juma Nassoro, Jeremiah Mtobesya na Abubakar Salum kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yanadaiwa kutendeka Zanzibar.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake huo uliotolewa na Jaji Mustapha Ismail baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hoja za pingamizi la utetezi na majibu ya upande wa mashtaka ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga akisaidiwa na wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Paul Kadushi, ilikubaliana na hoja za utetezi.

Jaji Ismail alisema pamoja na mambo mengine kuwa kwa makosa ambayo yanadaiwa kutendeka Zanzibar, jukwaa sahihi la kuwashtaki washtakiwa ni katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Ismail aliuamuru upande wa mashaka kufafanua marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuyaondoa mashtaka hayo na kubakiza yale ambayo yamedaiwa kutendeka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara ambayo ndio mahakama hiyo ina uwezo wa kuyasikiliza.

Zaidi, soma: Sheikh Ponda ampongeza Mkurugenzi mpya wa mashtaka(DPP) kukutana na Masheikh wa Uamsho Gerezani
Allahu Akbar! ALLAH Akbar! Allahu Akbar! Alshukrulillah!.
Mungu ndie mkubwa! Yeye ndio anaepaswa kushukuriwa!
 
Mkawashauri sasa hao Masheikh wenzenu waishi kama dini yenu inavyotaka. Yale masuala ya kuhamasisha vurugu, utengano kwa kuwaumiza watu wasio na hatia, kumwagia watu wa imani tofauti tindikali, nk. Yalikuwa yanakiuka kabisa uvumilivu wa kiimani.
Haki itadaiwa kwa njia zozote hata kama watafsiri hatua hiyo ni vurugu...

Na haya mambo asikudanganye mtu, chanzo chake kikuu ni MUUNGANO tu...

Na kauli au viapo batili vya viongozi vya "...nitaulinda muungano kwa gharama zozote..." zitaanza kuwatokea puani wenyewe

Hakuna kitu kama hicho tena. Utafika wakati na wakati huo umekwisha kufika wa gharama hizo kulipwa na viongozi wenyewe wanaojiapiza kijinga na kipumbavu namna ile....!
 
Hili swala Ni sensitive Sana kwa nchi yetu lakini watu wanalichukulia kisiasa lakini huko mbeleni hawa masheikh wataleta shida sana.kwa Yale mahubili yao ya kuhamadisha vulugu halafu Leo wanaachiwa huli.Tena ikizingatiwa Mambo yaliyopo Msumbiji sijui nini kitatokea.Labda watakua monitored by government nje ya hapo hawa jamaa sio watu wazuri kwa mstakabali wa nchi yetu.N mawazo yangu Wala Sina chili nao.
 
Kiusalama hii imekaaje?
Kiusalama wewe unatakiwa uende mahabusu ukakae 7 solid years then uachiwe baada ya hiyo miaka kwa kua ushahidi utakua hakuna.
Bladful, uzalendo wa kitanzania.

Nyie ndio mlikua mmefunga shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani mkidai sababu za ki integensia, sababu za ki usalama bludful kumbe mnakula keki ya kitaifa kimya kimya.
 
sasa watatokea chagadomo na kumbebesha lawama mwendazake utadhani yeye ndo aliwafungia ndani...ifikie sehemu usalama wa nchi uwe zaidi ya dini,kabila wala jinsia..big up kikwete..big up magufuri..hope mama samia kuwatoa hawa ndugu zake amewaonya waende wakatulie na kulea watoto wao..hii nchi ni zaidi ya mtu mmoja mmoja
Unajihisi hisi tu. Unajua kuwa Chadema ndio walisimama mstari wa mbele kutaka haki itendeke kwa mashekhe wote nchini waliotiwa ndani kwa kesi za kubambikia.

wakati huo nyie wachawi mnashabikia mauwaji na mateso kwa watu wengine. Bahati nzuri pioneer wa uonevu sasa akapigwa adhabu ya kifo mazima.
 
Mkawashauri sasa hao Masheikh wenzenu waishi kama dini yenu inavyotaka. Yale masuala ya kuhamasisha vurugu, utengano kwa kuwaumiza watu wasio na hatia, kumwagia watu wa imani tofauti tindikali, nk. Yalikuwa yanakiuka kabisa uvumilivu wa kiimani.
Ikiwa mahakama imewaona hawana hatia ,iweje wewe useme hivyo?
Kumwagia mtu Tindikali ni hatia ,kama wewe unao ushahidi si uende ukaweke pingamizi.!
Mzushi mkubwa weee!
Ushindwe na ulegee kwa jina la aliye Kuumba
 
Hili swala Ni sensitive Sana kwa nchi yetu lakini watu wanalichukulia kisiasa lakini huko mbeleni hawa masheikh wataleta shida sana.kwa Yale mahubili yao ya kuhamadisha vulugu halafu Leo wanaachiwa huli.Tena ikizingatiwa Mambo yaliyopo Msumbiji sijui nini kitatokea.Labda watakua monitored by government nje ya hapo hawa jamaa sio watu wazuri kwa mstakabali wa nchi yetu.N mawazo yangu Wala Sina chili nao.
Bila jiwe kufa haki isingetendeka. Mungu ni mwema
 
Hili swala Ni sensitive Sana kwa nchi yetu lakini watu wanalichukulia kisiasa lakini huko mbeleni hawa masheikh wataleta shida sana.kwa Yale mahubili yao ya kuhamadisha vulugu halafu Leo wanaachiwa huli.Tena ikizingatiwa Mambo yaliyopo Msumbiji sijui nini kitatokea.Labda watakua monitored by government nje ya hapo hawa jamaa sio watu wazuri kwa mstakabali wa nchi yetu.N mawazo yangu Wala Sina chili nao.
Kiusalama wewe unatakiwa uende mahabusu ukakae 7 solid years then uachiwe baada ya hiyo miaka kwa kua ushahidi utakua hakuna.
Bladful.

Back
Top Bottom