Masheikh wa Uamsho wafutiwa kesi, warejea uraiani
Chadema, Tundu Lissu,Mbowe,Maria Sarungi na wengine wengi ambao sio Waisilamu walikuwa wanapiga kelele hata kwa Mwendazake ili Mashekhe wa Uamsho na wale wengine waliosondekwa kwenye Gereza la Arusha waachiwe Huru.

Huo udini wa Raisi Samia umetoka wapi? wewe ndio unataka kufanya kuwa ni Issue ya Dini.
Achana na siasa katika jambo hili Mbowe alikuwa akimpinga JPM leo hata mwaka hamna ameanza kuongea ukwel.
Wametoka kwa msukumo wa kidini
 
Hawa jamaa watatulia kwa muda ila baada ya mama kumaliza muda wake, hysee pataanza kuchimbika Kama awamu ile
 
We ni Mbishi bana kaa na Udini wako.
Wameyatenda yote walishtakiwa nayo ndo mana hali ilikuwa salama walipokuwa ndani sasa wametoka tena tutegeme mambo kujirudia tena
mimi siyo mdini.
 
Wameyatenda yote walishtakiwa nayo ndo mana hali ilikuwa salama walipokuwa ndani sasa wametoka tena tutegeme mambo kujirudia tena
mimi siyo mdini.
Hilo Vuguvugu lilizimwa na Raisi Kikwete na Raisi Samia kawatoa sasa hao wote ni Waisilamu kinachokuwasha wewe ni nini?
 
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

SHEIKH MSELEM SHEIKH FARID WAKO NYUMBANI ZANZIBAR

Masheikh zetu wawili wako majumbani kwao na familia. Tutaendelea kukupeni taarifa awamu kwa awamu.

Lengo ni kutoa taarifa za kweli na zilizozingatia mambo yote muhimu.

Aidha viongozi wa Shura Taifa wako angani wakielekea Zanzibar.

Ibrahimu Zuberi Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania
0713118812

=======

Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu ameieleza Mwananchi Digital leo Jumatano Juni 16, 2021 kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Wawili hao ambao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Taarifa za kuachiwa huru kwa viongozi hao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana jioni zikieleza kuwa viongozi hao wawili ndio wameachiwa huru na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro amelieleza Mwananchi Digital kuwa wameshapelekwa majumbani mwao.

Katika ufafanuzi wake Mwakitalu amesema, “ni kweli wameachiwa huru. Nimewafutia wote mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Sasa suala la kutoka gerezani kama wameshatoka wote au wangapi hilo ni suala la taratibu za Magereza lakini mimi nimewafutia mashtaka wote.”

Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kujihusisha na makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002 Januari 2013 na Juni 2014.

Awali walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua za awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa usikilizwaji kamili wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 25.

Lakini Aprili 23, 2021 Mahakama Kuu iliwafutia mashtaka 14 baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wao, Daimu Halfani, Juma Nassoro, Jeremiah Mtobesya na Abubakar Salum kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo kwa kuwa makosa wanayotuhumiwa yanadaiwa kutendeka Zanzibar.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake huo uliotolewa na Jaji Mustapha Ismail baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hoja za pingamizi la utetezi na majibu ya upande wa mashtaka ulioongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga akisaidiwa na wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Paul Kadushi, ilikubaliana na hoja za utetezi.

Jaji Ismail alisema pamoja na mambo mengine kuwa kwa makosa ambayo yanadaiwa kutendeka Zanzibar, jukwaa sahihi la kuwashtaki washtakiwa ni katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Jaji Ismail aliuamuru upande wa mashaka kufafanua marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuyaondoa mashtaka hayo na kubakiza yale ambayo yamedaiwa kutendeka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara ambayo ndio mahakama hiyo ina uwezo wa kuyasikiliza.

Zaidi, soma:

-
Sheikh Farid: Tunashukuru Tumeachiwa, Ni Mwanzo Mwema wa Rais Mwinyi na Samia

- Sheikh Ponda ampongeza Mkurugenzi mpya wa mashtaka(DPP) kukutana na Masheikh wa Uamsho Gerezani

- Mufti Abubakari Zuberi ahimiza uharaka kesi ya mashehe wa Uamsho

-
Watuhumiwa wengine 16 katika kesi iliyokuwa inawakabili Masheikh wa Uamsho wameachiwa

Hivi Mkwere ndo aliwaswaga jela au Mwendazake?
Any way sasa wakatulie na waache choko choko!
 
Hilo Vuguvugu lilizimwa na Raisi Kikwete na Raisi Samia kawatoa sasa hao wote ni Waisilamu kinachokuwasha wewe ni nini?
Kinacho niwasha ni haki kwa yale waliyo yatenda na haki kwa wale waliotendewa.
Ujasikia mmoja wa hao magaidi akiwashukuru marais wa pande zote wametoka kwa msukumo bali siyo kwa kupata haki yao.
Samia amefail samia mdini.
 
Kinacho niwasha ni haki kwa yale waliyo yatenda na haki kwa wale waliotendewa.
Ujasikia mmoja wa hao magaidi akiwashukuru marais wa pande zote wametoka kwa msukumo bali siyo kwa kupata haki yao.
Samia amefail samia mdini.
Sijui kama kuna ushahidi uliowahusisha na matukio hayo wangeshahukumiwa ila kuwaweka watu jela bila ya kuwahukumu ni kosa
 
Hapo Kikwete atakuwa kavimba kama chura
Kikwete mpole sana, ingekuwa ni mimi kulingana na yale mahubiri yao ningewala vichwa ASAP sina mchezo na mtu anayehatarisha uhai wa watu wengine
 
Kikwete mpole sana, ingekuwa ni mimi kulingana na yale mahubiri yao ningewala vichwa ASAP sina mchezo na mtu anayehatarisha uhai wa watu wengine
Walihatarisha uhai aa nani? hakuna mtu ameondoa uhai wa watu kama jiwe.
 
Na tangu hawa watu wahifadhiwe, hali ilikuwa shwari.
Magaidi wa msumbiji viongozi wake wengine wanatoke a Tanzania.
Leo hii, yanatukuta tena Watanzania.
Mungu Irehemu nchi ya Tanzania, maana bila Rehema ya Mungu kinachofuata ni kilio na kusaga meno.
mnafiki mkubwa wewe. Jiwe ametesa sana watu ndio maana Mungu kampa adhabu ya kifo. Bado nyie wahuni
 
Mashekh wangu aluta Continua,
Madai ya Zanzibar yenye Mamlaka yake katika Muungano yako pale pale.
Kapumzikeni kidogo, karibuni ttaliamsha tena Dude, kwani Zanzibar bado imekaliwa kmabavi,Labda Huyu Bi kubwa afanye mndingo yake kuikwamua.
Tanzania = Tanganyika + Zanzibar

Tukipata mapato tugawane sawa sawa,
Kama Hamtaki nendeni mukaungane na Kongo ikiwa sisi munatuona wadogo, Wle ndio saizi yenu.
Nyie warabu weusi ni shida Sana,Mungu akipenda huu muungano uvunjike hauna faida kwa wabara,ajira zenyewe tu Kama za ualimu mpaka tuwaajiri
Huu ni wakati wenu muafaka wa kujitenga na Tanganyika. Mtumieni Mzanzibar mwenzenu kufanikisha jambo hilo.

Binafsi naamini hata Zanzibar ikijitenga kesho, Tanganyika haina cha kupoteza! Zaidi mapato yetu yataongezeka! Maana tutaanza kuwatoza wengi wenu mnaoishi Tanganyika vibali vya kufanya kazi na kidi nyingine mbalimbali.
Kweli kabisa hao warabu koko wamezidi kulia lia Sana na huyo goi goi wao aliyepo madarakani ebu watuachie nchi yetu Tanganyika waendeleze na siasa zao za maji taka Mara sisi waunguja Mara sisi wapemba tuna mafuta na kudumisha mila na desturi za kiarabu!huku wakila mlo mmoja kwa ck pengine na kushindia boflo! yahani wabunge tuwalipe sisi mshahara na kiinua mgongo watoto wao watumie Kodi zetu kuingia chuo kikuu ajira waajiriwe kwetu kwao sie wabara haturuhusiwi kuajiriwa Mara Zanzibar inaidai Tanganyika cjuhi sh ngpy lkn Zanzibar haidaiwi kwenye deni la taifa
 
Zamu ya sabaya bashite nao wasubirie ushahidi kukamilika kwa miaka sita hivi wachukue nafasi ya wazee wa escrow.Kulia ni kupokezana
🤣🤣🤣juzi Sabaya kukaa wiki tu wamelalamika hao utadhani mashoga. Sabaya wiki moja tu kakondeana kama anaumwa ngoma. Sijui huwa wanajionaje wanaposhabikia udhalimu
 
Back
Top Bottom