Si kwamba wamesema istikhara hufanywa usiku bali baadhi ya hao waja wema huifanya kabla ya kulala. Hata hivyo lengo langu si kuijadili sana istikhara bali kuonyesha tu kwamba yapo mambo mengi tu ambayo tunaweza kuyafanya pasina kutumia njia za shirki na uchawi na ukapata matokeo yale yale.
Kwahiyo hata kwenye kuwasiliana na jini si lazima zitumike njia za kichawi.
SWALI LA KWANZA kwako, ni kwanini baadhi ya hao waja wema wafanye istikhara kabla ya kulala na si wakati mwingine?!
SWALI LA PILI, ni njia gani ambazo unaweza kutumia kuwasiliana na majini bila kutumia njia zilizotajwa katika vitabu vya uchawi?!
SWALI LA TATU. Tukiachana na manabii nitajie mtu mwema mmoja tu ambaye alikuwa akiwasiliana na majini na alikuwa anataka nini kwa hao majini ambacho hawezi kukipata kwa wanaadamu wenzake?!
SWALI LA NNE. Majini hatuna uwezo wa kuwaona kwa macho japo wao wanatuona kama Quran ilivyoeleza kwenye suuratul Aaraafu Aya ya 27:
{ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ }
Hakika yeye (shetani )na kabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wa wasio amini."
Na suuratul jinni imebainisha kuwa Kuna majini wema kwa waovu , waislamu na makafiri.
Na waislamu tunakatazwa kutafuta ushauri na msaada kwa watu waovu hata kama ni binadamu wenzetu wachilia mbali kutafuta ushauri kwa jini muovu.!
Sasa SWALI NI KWAMBA , IKIWA JINI MPAGANI AU MKRISTO AU MYAHUDI AKIKUDANGANYA KUWA YEYE NI MUISLAMU NA ANASWALI SWALA TANO NA ANAENDA HIJA KILA MWAKA.
Ni njia gani utatumia kujua kuwa huyu jini ni MUONGO?!
Kumbuka ikiwa kuna binadamu waongo majini waongo pia wapo kutokana na yanayopatikana katika baadhi ya Aya katika suuratul Jinni hasa Aya ya 11 na 14.
Na MWISHO ni jinsi gani utajua kuwa ushauri au maelekezo uliyopewa na jini ni sahihi wakati hujui jini huyo kama ni mwema au muovu?! Au unadhani jini muovu anaweza yeye mwenye kujitaja kuwa ni muovu.
Je unakumbuka maneno ambayo ibilisi aliyatumia kuwapoteza wazazi wetu Adamu na Hawaa hadi kufukuzwa peponi yalikuwa mazuri hadi Ibilisi aliapa kwamba anawapa nasaha na ushauri mzuri ?!
Allaah kalitaja tukio hili ndani ya suuratul Aaraafu Aya ya 21 hadi 22 kwa kusema:
{ وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ }
NAYE (Ibilisi )AKAWAAPIA (Adamu na Hawaa akawaambia ) KWA YAKINI MIMI NI MIONGONI MWA WANAOKUNASIHINI . (wanaokupeni nasaha na ushauri mzuri)
{ فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ }
Basi akawateka (Adamu na Hawaa) kwa KHADAA. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri?"
HUYO NDIYE SHETANI .
Anapotaka kukupoteza atakwambia yeye ni mwema na anakupendanna anataka upate kheri na mafanikio duniani na akhera kumbe ndiyo anakipoteza kidogo kidogo!.