Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Pre GE2025 Mashekhe wafanya ibada na kuomba majini yasaidie Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mmeweza kumzushia Yesu ni mungu na mkamchora katuni mkamchonga katuni na movie juu...bado hamjaridhika sahv mnadai anawatokea mpk mnauza mafuta udongo na kuchoma magari....ndo mtaweza kuuletea uzushi uislam?...ndo laana mliyoachiwa kuzusha uzushi...na hamtoacha
Bin Mwamedi punguza jazba, nawewe umeshawekewa majini au Maruani?
 
Ila mbona binaadamu tunasaidiana?
Swali lako ni muhimu sana, japo likikosa JAWABU sahihi washirikina watapata kichochoro Cha kuhalalisha ushirikina wao.
Ni kweli Allaah ametumrisha kila tunaposwali tuseme
katika Aya ya 5 ya suuratul faatiha:
{ إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ }
"Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada."

Lakini ni Allaah huyohuyo aliyesema katika Aya ya 2 ya suuratul maaidah:
وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ" وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ
" Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui."
Aya 2 hizi hazipungani na maelezo yake kama walivyoeleza wanachuoni ni kama ifuatavyo;.
1️⃣ Kumuomba msaada binadamu mwenzio anayeendelea kuishi ( sio mfu, maiti, marehemu )
katika jambo ambalo lipo katika uwezo wake wa kibinaadamu kama kukusaidia au kukukopesha pesa, kukubebea mzigo, kupeleka ujumbe fulani kwa binadamu wengine, kukutibu ugonjwa ulionao kama anayo elimu ya matibabu ( sio kuonyesha! Daktari anatibu, Allaah anaponyesha akitaka ) kusaidiana huku ni HALALI na ndio kusudio la Aya ya pili katika suuratul Maaidah.
2️⃣. Kumuomba msaada binadamu mwenzio ambayo yapo nje ya uwezo wa kibinadamu kama kuleta mvua, kuotesha mimea, kuponyesha maradhi ( sio kutibu!, daktari anatibu , Allaah anaponyesha akitaka )
kufufua wafu na mengineyo yaliyopo nje ya uwezo wa binadamu katika hali ya kawaida kusaidiana huku ni HARAMU.
3️⃣. KUWAOMBA MSAADA WATU WALIOKUFA HATA KAMA NI MITUME NA MANABII NI HARAMU.Wale waislamu wanaodai kufanya kisomo cha Albadiri kisomo hicho ni haramu kwa sababu huwa wanawaomba wafuasi wa Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم waliopigana vita pamoja na mtume katika eneo maalumu linaloitwa Badru.
Kwahiyo ukisikia kisomo cha Albadiri ni KUWAOMBA MASHUJAA WA VITA VYA BADRU. HARAMU.

4️⃣. Kuwaomba viumbe wasioonekana kwa macho ya kawaida kama malaika , majini na mashetani ( majini waovu ) pia ni HARAMU.
 
Kwa wale tu wenye Akili za kuona mbali
Je mumeshagundua nini kuhusu Uzi huu ???!
Uchaguzi umekaribia kwahiyo sisi wenye uwezo wa kudadavua mambo tunaanza kupata mashaka kwamba ukiona nyuzi zinapandishwa humu zenye muelekeo wa Udini na kisha kukaanza malumbano ya kidini nia ya waleta nyuzi siku zote inakuwa ni moja tu !
Ni ile ile principal ya tangu Enzi na Enzi
“DIVIDE THEM AND RULE “
Waleta nyuzi za namna hii huwa wana ajenda zao za Siri !

Waliosomea Cuba 🇨🇺 wanaweza wakaelewa hii maneno imekaaje !
Hiyo yaweza kua ni starting point ya kuupima upepo ili tanga likae sawa kwa ajili ya kuanza safari 😳🙄!

Muwe mukitumia common sense sometimes !

Au nasema uongo ndugu zanguni !!! 🤣🙏 🙄 !?
Post ya kipuuzi kabisa👆 kuwahi kutokea JF.
Ingekuwa umeandikwa uongo hapo ungeeleweka, lakini kumewekwa taarifa ili wananchi wafahamu kinachoendelea nchini na wapate wasaa wa kutoa maoni yao wewe unaingiza siasa. Kama uko kundi la hao mashehe ulitamani hiyo iwe siri baina yenu peke yenu basi ndiyo ujue na sie tumebahatika kuyafahamu luckily kupitia humu janvini otherwise tusingeyajua haya ambayo seriously ni muhimu kuyajua ili tuwafahamu vizuri hao mashehe, taasisi yao na misimamo yao kama viongozi wa imani(dini) au pia unaweza usiwe miongoni mwao ila ukawa ni mpambe au shabiki au chawa wa bibi Chura-Kiziwi hivyo haya ya mashehe-chawa ulitamani yasijadiliwe kwa kuwa unajua kwamba kwanza ni udini(ambao hata CCM wanadai wanaupiga vita) ambao unaleta mpasuko katika jamii na pia huyo bibi ni aibu ameshirikishwa kwenye shirki.
 
Mitazamo tofauti na uelewa tofauti pia !
Naendelea kusisitiza kwamba hii itaenda kuwagawa watu wasiwe kitu kimoja katika kufanya maamuzi mwisho wa siku wanufaika siku zote wanafahamika ni wale wale tu !

Watu watasema ni bora wale wale wetu tuliowazoea miaka yote !
Na ndio hasa nia ya waleta mada za Udini Udini kama hizi 😳
 
Mbona nchi za Wakristo ndio masikini zaid ata ukienda America ya kusini umaskini umetamalaki tena ni Wakatoriki mnajiona ni Wasomi Tafaut na Nchi za Waislam Waarabu matajili Sana.,, NENDA Malawi wengi Wakristo Wadada wao wamejazana kufanya kazi za ndani apa mjini tofaut na nchi zenye Waislam wengi !!! Zaid duniani mnasifika Viongozi wenu wamakanisa wana makesi tu ya kuwala O sio kwenye Uchumi!!!!
Usidanganye watu kuwa eti nchi za kiislam ni tajiri, ni uwongo mkubwa.

Soma hapo chini, labda utaijiwa na akili:

Is Yemen a rich or poor country?

Despite possessing significant oil and gas resources and a considerable amount of agriculturally productive land, Yemen remains one of the poorest of the world's low-income countries. In 2018, more than 80 percent (2018) of the population lived in poverty.

Does Lebanon have a good economy?

Lebanon's economic and financial crisis ranks among the worst economic crises globally since the mid-nineteenth century
Ametaja na malaika si majini tu pekee yake.
Malaika hawashikamani na majini. Kiimani, hata ukimwomba Mungu, halafu ukamwunganisha katika maombi na shetani, atakuacha na shetani wako. Ni sawa utangaze kuomba msaada kutoka kwa majambazi na watu wema, watu wema watakuacha na majambazi yako.

Malaika hawasaidiani na mashetani katika utendaji wao.
 
Shehe mzima atakujaje na hii takataka?

Nadhani kuna fungu kapewa, sasa anarudisha fadhila!

Shehe ni mtu mwenye elimu ya dini ya kiislam isiyoweza kutiliwa mashaka, iweje ajifyetue kwa kiwango cha lami kiasi hicho?

Wadau fuatilie yaliyo nyuma ya pazia mtaelewa mengi yaliyo nyuma ya kauli hizi.
Rushwa hupofusha macho.
 
Post ya kipuuzi kabisa👆 kuwahi kutokea JF.
Ingekuwa umeandikwa uongo hapo ungeeleweka, lakini kumewekwa taarifa ili wananchi wafahamu kinachoendelea nchini na wapate wasaa wa kutoa maoni yao wewe unaingiza siasa. Kama uko kundi la hao mashehe ulitamani hiyo iwe siri baina yenu peke yenu basi ndiyo ujue na sie tumebahatika kuyafahamu luckily kupitia humu janvini otherwise tusingeyajua haya ambayo seriously ni muhimu kuyajua ili tuwafahamu vizuri hao mashehe, taasisi yao na misimamo yao kama viongozi wa imani(dini) au pia unaweza usiwe miongoni mwao ila ukawa ni mpambe au shabiki au chawa wa bibi Chura-Kiziwi hivyo haya ya mashehe-chawa ulitamani yasijadiliwe kwa kuwa unajua kwamba kwanza ni udini(ambao hata CCM wanadai wanaupiga vita) ambao unaleta mpasuko katika jamii na pia huyo bibi ni aibu ameshirikishwa kwenye shirki.
Hao mashehe sipendi kuamini kuwa labda mh Rais kawaambia waseme hayo waliyoyasema.
Kinachoonekana KWA KUJIPENDEKEZA ILI WAONGEZEWE MKATE WAO WANAOPEWA MARA KWA MARA!, wanemuomba au kumpa taarifa mheshimiwa rais kwamba wanataka wamfanyie dua Mungu amlinde yeye na serikali yake dhidi ya maadui.
Mh Rais ktk hali ya kawaida hata angekuwa wa chadema asingekataa ombi hili. Jambo hili msilihukumu kwamba ni udini ndani ya serikali Moja kwa moja bali lichukulieni kuwa ni jambo ambalo limefanywa n viongozi wa taasisi inayoitwa bakwata ambao wanapalilia maslahi yao ndani ya serikali iliyopo madarakani.
Siku yoyote msije kushangaa KKKT au kanisa lolote jingine na wao wakaandaa maombi ya kumuombea mama Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.
Taasisi za kidini ambazo zinapokea ruzuku za mabilioni ya pesa za walipa Kodi ni nyingi na ushahidi upo ila HAWA BAKWATA WANAJIPENDEKEZA KUPITA KIASI.
Mwaka jana nilihudhuria maadhimisho ya siku ya kansa katika hospitali ya KCMC Moshi ambapo mgeninrasmi alikuwa RC wa Kilimanjaro mh Nurudini Babu.
Katika taarifa mkurugenzi wa hospitali ya KCMC alieleza mabilioni ya pesa alizotoa mama Samia na na mabilioni mengine ambayo ameahidi kutoa kwa ajili ya kuboresha kitengo Cha saratani Cha KCMC kwa vifaa na miundombinu pesa nyingi sana ambayo Nina uhakika BAKWATA hawajawahi pewa hata robo yake kwakuwa HAWANA MIPANGO WALA MALENGO ZAIDI YA KUTANGAZA MWEZI NA SHEREHE ZA MAULIDI.
Taasisi za kidini zinazopata pesa toka serikalini ni nyingi sana hasa makanisa na miradi na taasisi za makanisa
ILA HAWA BAKWATA ULIMBUKENI WAO NDIO UNAWAFANYA WAFANYE VISA VYA AJABU KAMA VINAVYOONEKANA KWENYE HIYO VIDEO.
 
Haaa maskini wanamchora mama samia na lait angelijua hizi ndo dalili zenyewe kwamba hatashinda
 
Mashekhe waliokutana chini ya Shekhe Mkuu Mufti Abbakari, kwenye msikiti wa kwa Mtoro, jijini Dar es Salaam wamefanya ibada maalum ya kumwombea Rais Samia ashinde kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Shekhe mkuu akiwa kwenye ibada hiyo ameagiza kuwa mashekhe wa mikoa yote, wilaya hadi kwenye kata, wafanye ibada ya kumwombea Samia ashinde kwenye uchaguzi ujao.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa anayaagiza majini yote yahakikishe Rais Samia anashinda kwenye uchaguzi wa urais mwaka huu.

SWALI:
Tukiyaamini maneno ya mashekhe hawa, ina maana uchaguzi wa safari hii utakuwa ni ushindani kati ya wanadamu na majini? Kama majini yakishinda, huyu Rais atakuwa wa wanadamu wa Tanzania au atakuwa Rais wa majini?

Wananchi wanapomchagua kiongozi wao, matarajio yao ni kuwa huyo wanayemchagua atawaongoza katika jitihada zao za kuyafikia maendeleo, sasa kama majini yatamchagua mgombea kuwa Rais, hayo majini yanatarajia kunufaika vipi na huyo yaliyempigania?

Wataalam wa majini tunaomba litoleeni ufafanuzi hili la mashekhe kuomba majini yamsaidie Rais Samia, inamaanisha nini katika tafsiri pana?
View attachment 3222655
View attachment 3222658
Uislamu ni UPUUZI.
 
Dahaaaa! Pole Mama Samia,umeruuhusu hii nchi kuwa ya kidini kwa ajili ya madaraka. Unaposema siasa isicchangaywe na dini mnamaanisha nini?
Sawa ,ebu ona atakapotokea mkristo kugombea, wakristo nao waitishe maombi huyo muumini mwenzao ashinde. Hapo mmoja asiposhinda vurugu za kutuibia kura zitaanza kusemwa misikitini na makanisani .
Toa tamko la kukemea hii tabia ya udinni.
Hizo pesa unazomwaga misikitini na makanisani zitaleta vita ambayo police hawataweza kuzuia
 
Post ya kipuuzi kabisa👆 kuwahi kutokea JF.
Ingekuwa umeandikwa uongo hapo ungeeleweka, lakini kumewekwa taarifa ili wananchi wafahamu kinachoendelea nchini na wapate wasaa wa kutoa maoni yao wewe unaingiza siasa. Kama uko kundi la hao mashehe ulitamani hiyo iwe siri baina yenu peke yenu basi ndiyo ujue na sie tumebahatika kuyafahamu luckily kupitia humu janvini otherwise tusingeyajua haya ambayo seriously ni muhimu kuyajua ili tuwafahamu vizuri hao mashehe, taasisi yao na misimamo yao kama viongozi wa imani(dini) au pia unaweza usiwe miongoni mwao ila ukawa ni mpambe au shabiki au chawa wa bibi Chura-Kiziwi hivyo haya ya mashehe-chawa ulitamani yasijadiliwe kwa kuwa unajua kwamba kwanza ni udini(ambao hata CCM wanadai wanaupiga vita) ambao unaleta mpasuko katika jamii na pia huyo bibi ni aibu ameshirikishwa kwenye shirki.
Kwhy alichofanya Samia ndo mara ya kwnz kutokea na kufanya yeye?..wagalatia mtaacha lini uzushi?..kabla ya kwnd umoja wa mataifa Nyerere hakuombewa na mashekhe bagamoyo?..kwa nini hakwnd kanisani mkalaumu?
 
Mbona wewe unamuabudu Allah wa waarabu?
Wewe ni miongoni mwa makabila ya waarabu?
Hapo ulipo bila lugha ya kiarabu hutoboi
Ona na hii matade nyingine unafikiri mm ni mtumwa wa fikra kama wewe,
Ndugu yangu ni kwamba sisi waislamu tuko katika makundi na madhehebu tafauti tafauti.
Hao mashehe wanaotangaza ushirikina hadharani kama mlivyoona kwenye video wana wafuasi wao wanaokubaliana na uchawi na ushirikina wao na wengine wamonserikalini na wapo tayari kuwatetea na kuwaunga mkono kwa hali na mali.
Pili kidini maandamano sio njia sahihi ya kuondoa maovu katika jamii.
Tunaishi katika nchi inayoamini uhuru wa kuabudu kwahiyo nchi kama hii hata waabuduo shetani Wana haki ya kumuabudu shetani wao kulingana na katiba, sheria na kanuni za nchi, sisi tunaloweza ni kusema tu kwamba vitendo hivyo ni kinyume na uislamu sahihi aliofundisha mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Waislamu wa bongo bwana mnavyojua kutetea mila za jamii nyingine mpo vizur,hapo umeshindwa kusema tuu hao sio waislamu kwasababu wanajulikana ndio viongozi wenu,ila ingekua wale ndugu zenu wacheza vigodoro hakika ungesema wale sio waislamu
 
Bin Mwamedi punguza jazba, nawewe umeshawekewa majini au Maruani?
Hiyo ndo laana yenu kamwe haitowaacha mmeweza kwa manabii mtashndwa vipi kwa binadamu?
Juzi tuu hapa Papa Francis kaleta uzushi na kiroja cha ajabu eti kaongea na mungu awabariki LGBT...bado mtasema na mnaamini lkn hamchoki kutafuta uzushi juu ya uislamu mara ugaidi mara majini alimradi litakokupendeza...
 
H
Ona na hii matade nyingine unafikiri mm ni mtumwa wa fikra kama wewe,

Waislamu wa bongo bwana mnavyojua kutetea mila za jamii nyingine mpo vizur,hapo umeshindwa kusema tuu hao sio waislamu kwasababu wanajulikana ndio viongozi wenu,ila ingekua wale ndugu zenu wacheza vigodoro hakika ungesema wale sio waislamu
Hebu njoo mada husika hawa viongozi wa dini kuwaombea Marais ni Samia ndo wa kwnz kuombewa?
 
Huyu ni mpumbavu mmoja anajiuta Dr sule.
Anachozungumza siyo sahihi.
Mitume wa Allaah wamepewa miujiza ya kuweza kuongea na kuviamrisha viumbe ambavyo havisikii wala kuongea katika hali ya kawaida.
Baadhi ya mitume waliweza kuviamrisha hata miti na mawe na viumbe hivyo vikawasikiliza mitume na kufuata amri zao.
Nabii Suleiman aliwezeahwa kuzungumza na wanyama wote na alifundishwa lugha za ndege sisimizi na wanyama wengine ikiwa pamoja na mashetani na majini pia aliwezeahwa kuuamrisha hata upepo ufanye anavyotaka na upepo ulifanya.
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakufuga majini ila kwa uwezo wa Allaah aliweza kuongea nao na kuwadhibiti baadhi ya majini waovu wasifanye kama kupita mbele yake akiwa anaswali na kitendo hiki ni katika miujiza aliyopewa kithibitisha utume na unabii wake na haimaanishi kwamba alifuga majini.
Tukisoma biblia hata Yesu aliyaamrisha mashetani yameache mgonjwa na yahamie kwenye kundi la nguruwe na kitendo kama hicho ni katika miujiza ya kuthibitisha utume na unabii wake na kila mtume na Nabii hupewa miujiza kulingana na hali , mazingira na watu aliotumwa kwao .
Wakifanya wao ni miujiza ila tukifanya sisi waafrika ni ushirikina na uchawi,sawa mkuu umeeleweka na watumwa wenzio
 
Back
Top Bottom