Ila mbona binaadamu tunasaidiana?
Swali lako ni muhimu sana, japo likikosa JAWABU sahihi washirikina watapata kichochoro Cha kuhalalisha ushirikina wao.
Ni kweli Allaah ametumrisha kila tunaposwali tuseme
katika Aya ya 5 ya suuratul faatiha:
{ إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ }
"Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada."
Lakini ni Allaah huyohuyo aliyesema katika Aya ya 2 ya suuratul maaidah:
وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ" وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ
" Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui."
Aya 2 hizi hazipungani na maelezo yake kama walivyoeleza wanachuoni ni kama ifuatavyo;.
1️⃣ Kumuomba msaada binadamu mwenzio anayeendelea kuishi ( sio mfu, maiti, marehemu )
katika jambo ambalo lipo katika uwezo wake wa kibinaadamu kama kukusaidia au kukukopesha pesa, kukubebea mzigo, kupeleka ujumbe fulani kwa binadamu wengine, kukutibu ugonjwa ulionao kama anayo elimu ya matibabu ( sio kuonyesha! Daktari anatibu, Allaah anaponyesha akitaka ) kusaidiana huku ni HALALI na ndio kusudio la Aya ya pili katika suuratul Maaidah.
2️⃣. Kumuomba msaada binadamu mwenzio ambayo yapo nje ya uwezo wa kibinadamu kama kuleta mvua, kuotesha mimea, kuponyesha maradhi ( sio kutibu!, daktari anatibu , Allaah anaponyesha akitaka )
kufufua wafu na mengineyo yaliyopo nje ya uwezo wa binadamu katika hali ya kawaida kusaidiana huku ni HARAMU.
3️⃣. KUWAOMBA MSAADA WATU WALIOKUFA HATA KAMA NI MITUME NA MANABII NI HARAMU.Wale waislamu wanaodai kufanya kisomo cha Albadiri kisomo hicho ni haramu kwa sababu huwa wanawaomba wafuasi wa Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم waliopigana vita pamoja na mtume katika eneo maalumu linaloitwa Badru.
Kwahiyo ukisikia kisomo cha Albadiri ni KUWAOMBA MASHUJAA WA VITA VYA BADRU. HARAMU.
4️⃣. Kuwaomba viumbe wasioonekana kwa macho ya kawaida kama malaika , majini na mashetani ( majini waovu ) pia ni HARAMU.