Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Jumla ya mashirika ya misaada 18 yakiwemo ya UN leo yametoa tamko la pamoja kuibembeleza Israel isimamishe vita kutokana na kihoro cha maangamizi walichokiona.
Mashirika hayo yameweka pembeni kila aina ya hisia na imani walizonazo na kubakiwa na ubinadamu tu na kuona inatosha adhabu iliyokwishakutolewa kwa raia na wengine wasiohusika.
Katika taarifa yake Umoja wa mataifa umesema umepoteza jumla ya wafanyakazi 78 tangu vita vya Gaza vianze idadi ambayo ni kubwa kuliko zote kwenye mzozo wawote uliowahi kutokea duniani na wao kuhusika kusaidia.
Wakati huo huo kwa mara nyengine jeshi hilo limesema limeuzingira mji wa Gaza na kwamba wakati wowote wataingiza askari wa miguu kupambana na Hamas ili kuwamaliza pamoja na kuokoa mateka.
Wale wote waliobaki eneo hilo la kaskazini ya Gaza wanaokadiriwa nusu milioni pamoja na kuishiwa na mahitaji muhimu wameamua kutokuondoka kufuata njia ya Salah Din waliyoelekezwa kuitumia.
Wamesema hawawezi kufanya hivyo kwanza kwa kutoakuamini ahadi za Israel baada ya wenzao wengi kuuliwa wakiwa wanatekeleza amri hiyo.Sababu nyengine ni kuwa njia hiyo imebomolewa na haiwezekani tena kupitika