Katika pitapita zangu za Krismasi, nilijikuta huko Mbezi kwa ndugu nikiwa nasubiri sinia la pilau na nyama ya sungura. Mazungumzo ya hapa na pale yakazua skendo inayotikisa mtaa: Jamaa mmoja alimfukuza mkewe na watoto na kuanza kuishi na "kaka poa" (shoga).
Kwa maelezo ya wenyeji, huyo kaka poa hakuonesha dalili zozote za kuwa shoga. Badala yake, alijulikana kwa shughuli nyingi zinazowaletea vijana kipato, kama ufundi wa bodaboda na kuendesha bodaboda. Mara nyingi, alionekana amekaa nje ya nyumba ya huyo kijana mwenye familia. Kumbe, usiku wa manane vijana wengine wanapotawanyika kutoka kwenye kijiwe, kaka poa huyo alikuwa wa mwisho kuondoka. Wakati huo, ndipo walikuwa wakikutana chooni kufanya yao. Mke wa jamaa alidhani mumewe anaenda kuvuta sigara!
Siku moja, mkewe aliamua kufuatilia na kufanya fumanizi. Alipogundua mke mwenza si mwanamke bali kaka poa, alijaribu kuokoa ndoa chinichini kwa kumpa ofa mumewe: kama "kupenda kwa mpalange" ndio tabia yake, basi awe anapata kwake kama mke halali. Hata hivyo, jamaa hakusikia, hali iliyosababisha fumanizi la pili. Safari hii, mke alitoa ultimatum: aidha yeye au kaka poa. Jamaa alivyokuwa bado hajajitambua, mke akaona bora afunge virago vyake na vya watoto na kuondoka.
Haikuchukua muda, nyumba ndogo (kaka poa) ikahamia rasmi pale nyumbani. Penzi lao lilijulikana mtaa mzima, na cha kushangaza ni kwamba kaka poa alikuwa akihudumiwa vyema kuliko hata mke na watoto walivyokuwa wakihudumiwa.
Maneno ya mtaani yalipomfikia mke wa zamani, akaamua kuwashirikisha ndugu wa mumewe. Baba mkwe na kaka wa mumewe waliingia mtaani na kumtembeza kichapo kizito kaka poa. Hadi sasa, mke amerudi nyumbani, lakini mume hajathubutu kurudi mtaa huo. Habari za chinichini zinasema mipango inaendelea ili familia ihame kabisa kutokana na aibu kubwa.
Dada zetu, mjihadhari katika ndoa hizi za sasa. Maana hizo "papuchi" zenu tayari zimepata mbadala mtaani. Kaka poa hawahitaji matumizi makubwa kama nyie, na kwa hali kama ya jamaa huyu, hata akikosa pesa anajua "mke no. 2" atakula ugali na dagaa bila manung’uniko!