Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Katika hali isiyotarajiwa mtu mmoja amezua taharuki katika eneo la Daraja la Selandar jirani na zilipo ofisi za Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti 25, 2021.
Imeelezwa kuwa tukio hilo limetokea Saba kasoro mchana huu, mtu huyo ambaye hakujulikana alikotokea, alianza kupiga risasi ovyo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Ramadhan Joseph amesema alikuwa kwenye daladala akitokea Mwenge kwenda Posta, ghafla akasikia mlio wa risasi eneo la ubalozi ndipo akamuona mtu huyo aliyevalia nguo za kiraia shati jeupe lenye mistari na suruali ya rangi ya khaki akiwa amenyanyua bunduki juu.
Na mara wakashuhudia majibizano ya risasi baina yake na polisi yalianza. “Kusema ukweli kilichotokea ni hatari, sisi tulikuwa kwenye daladala wakaanza kujibizana kwa risasi huku yule bwana akiwa akitembea kuelekea kilipo kibanda wanachokaa askari wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa, likatokea gari la GS likasogea kwenye tukio akaanza kulirushia risasi.
“Kila mmoja alikuwa anakimbia kivyake. Hali ilikuwa ngumu palikuwa hapatoshi,” amesema Joseph.
Naye Said Kiguta ambaye ni dereva wa gari aina ya Fuso anasema alikuwa anaelekea Posta, ghafla akaona gari yake inayumba ikabidi ashuke na aanze kukimbia.
“Mimi sina hili wala lile, naona gari zinageuza, nikashindwa kujiongeza nikawa naendelea na safari, ghafla gari likaanza kuyumba nikawa najiuliza imekuaje, ndiyo nikasikia mlio wa risasi, kwa hiyo ikanibidi nishuke nikimbie kwa sababu risasi ilipasua tairi ya gari yangu,” amesema.
Hata hivyo, Mwananchi limeshuhudia mwili wa mtu huyo ambaye alikuwa tayari amepigwa risasi na polisi, ukiwa umelala barabarani kwenye eneo hilo ambalo tayari lilikuwa limefungwa utepe wa kuashiria hatari, huku askari polisi wakiwa wamezingira kila kona hadi sasa.
Wakati huo huo; Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa mauaji ya askari wawili jirani na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salam lilipofanyika shambulizi hilo.
Amesema tukio hilo limetekelezwa na mtu mmoja ambaye inasemekana ni Msomali ambaye pia amefariki dunia baada ya kutekeleza mauaji hayo.
PIA SOMA:
- Breaking News: - Kinondoni, Dar: Mtu asiyejulikana na Polisi Wawili wauawa katika Majibizano ya Risasi