Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi

Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Katika hali isiyotarajiwa mtu mmoja amezua taharuki katika eneo la Daraja la Selandar jirani na zilipo ofisi za Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti 25, 2021.

Imeelezwa kuwa tukio hilo limetokea Saba kasoro mchana huu, mtu huyo ambaye hakujulikana alikotokea, alianza kupiga risasi ovyo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Ramadhan Joseph amesema alikuwa kwenye daladala akitokea Mwenge kwenda Posta, ghafla akasikia mlio wa risasi eneo la ubalozi ndipo akamuona mtu huyo aliyevalia nguo za kiraia shati jeupe lenye mistari na suruali ya rangi ya khaki akiwa amenyanyua bunduki juu.

Na mara wakashuhudia majibizano ya risasi baina yake na polisi yalianza. “Kusema ukweli kilichotokea ni hatari, sisi tulikuwa kwenye daladala wakaanza kujibizana kwa risasi huku yule bwana akiwa akitembea kuelekea kilipo kibanda wanachokaa askari wanaolinda ofisi za Ubalozi wa Ufaransa, likatokea gari la GS likasogea kwenye tukio akaanza kulirushia risasi.

“Kila mmoja alikuwa anakimbia kivyake. Hali ilikuwa ngumu palikuwa hapatoshi,” amesema Joseph.

Naye Said Kiguta ambaye ni dereva wa gari aina ya Fuso anasema alikuwa anaelekea Posta, ghafla akaona gari yake inayumba ikabidi ashuke na aanze kukimbia.

“Mimi sina hili wala lile, naona gari zinageuza, nikashindwa kujiongeza nikawa naendelea na safari, ghafla gari likaanza kuyumba nikawa najiuliza imekuaje, ndiyo nikasikia mlio wa risasi, kwa hiyo ikanibidi nishuke nikimbie kwa sababu risasi ilipasua tairi ya gari yangu,” amesema.

Hata hivyo, Mwananchi limeshuhudia mwili wa mtu huyo ambaye alikuwa tayari amepigwa risasi na polisi, ukiwa umelala barabarani kwenye eneo hilo ambalo tayari lilikuwa limefungwa utepe wa kuashiria hatari, huku askari polisi wakiwa wamezingira kila kona hadi sasa.

Wakati huo huo; Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa mauaji ya askari wawili jirani na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salam lilipofanyika shambulizi hilo.

Amesema tukio hilo limetekelezwa na mtu mmoja ambaye inasemekana ni Msomali ambaye pia amefariki dunia baada ya kutekeleza mauaji hayo.

PIA SOMA:
- Breaking News: - Kinondoni, Dar: Mtu asiyejulikana na Polisi Wawili wauawa katika Majibizano ya Risasi
 
Huyu
IMG-20210825-WA0008.jpg
jamaa sijui zilimruka,
Unafanyaje shambulio la namna ile huku unatembea katikati ya barabara?
 
Na kama huyu jamaa angetulia trust me wasingekuwa askari wawili tuu... huwaaa nacheka sana polis wanapojimwambafy kuwaa wapo tayar kwa lolote askari hajawahi kwenda range kwa miaka kazaa anapga risasi had 5 ndo anapata target inatia uchungu sana
 
Kwa tukio la leo nimeelewa why Lissu hakudedi... Askari hawana shabaha.. yaani mtu anapiga risasi kibao anakosa nadhani hata iliyompata ni bahati tu... Leo ule msemo wa Mama umepigwa chini kuwa Askari wake huwa hawakosi shabaha
 
Mambo ya dola unayaweka hadharani kwa faida ya nani?

Ukikamatwa utoe ushahidi wa kutosha kwa maelezo yako utalalamika unaonewa.

Kuwa na uhuru wa mitandao si sababu uwe unajua kuelezea kila kitu, ukimya nao ni busara.
 
Huyu kama alikua gaidi au jambazi bado napata mashaka,kwanini alikua kindezi ndezi vile ilhali anajua kabisa anapambana tena kwa risasi,alafu sijawai ona gaidi anaacha raia wakiwa hai mbele yake.
 
Polisi wetu ni wataalamu wa kupambana na raia wa upinzani wasio na siraha, kwa mwenye siraha hawana weledi kabisa. Muda wa kukaa chuoni ni mfupi, wanaochukuliwa chuoni sifa kuu ni nafasi ya baba au ndugu yake polisi au ofisi ya serikali. Kuna mbumbumbu kibao polisi, mchujo wa vyeti fake ulisiti kuingia polisi kwani ingekuwa fedheha.
 
Na kama huyu jamaa angetulia trust me wasingekuwa askari wawili tuu... huwaaa nacheka sana polis wanapojimwambafy kuwaa wapo tayar kwa lolote askari hajawahi kwenda range kwa miaka kazaa anapga risasi had 5 ndo anapata target inatia uchungu sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mambo ya dola unayaweka hadharani kwa faida ya nani?

Ukikamatwa utoe ushahidi wa kutosha kwa maelezo yako utalalamika unaonewa.

Kuwa na uhuru wa mitandao si sababu uwe unajua kuelezea kila kitu, ukimya nao ni busara.
Hii comment nitakuwa nasoma Kila siku [emoji23][emoji23][emoji23] una busara za viwango
 
Na kama huyu jamaa angetulia trust me wasingekuwa askari wawili tuu... huwaaa nacheka sana polis wanapojimwambafy kuwaa wapo tayar kwa lolote askari hajawahi kwenda range kwa miaka kazaa anapga risasi had 5 ndo anapata target inatia uchungu sana

endelea kucheka.
 
Huyu kama alikua gaidi au jambazi bado napata mashaka,kwanini alikua kindezi ndezi vile ilhali anajua kabisa anapambana tena kwa risasi,alafu sijawai ona gaidi anaacha raia wakiwa hai mbele yake.
Nawaza labda akili zilimruka mbona alikuwa anarusha risasi hewani badala alenge watu? Police nao shabaha hawana wakashindwa kulenga hata za miguu ili asaidie kwenye upelelezi naona walikuwa wanabahatisha ili tu risasi impate popote
 
Kwa tukio la leo nimeelewa why Lissu hakudedi... Askari hawana shabaha.. yaani mtu anapiga risasi kibao anakosa nadhani hata iliyompata ni bahati tu... Leo ule msemo wa Mama umepigwa chini kuwa Askari wake huwa hawakosi shabaha
Yawezekana lengo ilikuwa kumpata akiwa hai
 
Na kama huyu jamaa angetulia trust me wasingekuwa askari wawili tuu... huwaaa nacheka sana polis wanapojimwambafy kuwaa wapo tayar kwa lolote askari hajawahi kwenda range kwa miaka kazaa anapga risasi had 5 ndo anapata target inatia uchungu sana
Ungekuwa mmoja wa waliokuwepo kwenye ile daladala naimani saiv ungekuwa kanisani Au msikitini unashukuru, ila kwakua hayajakukuta basi endelea kucheka ka raha zako.

Ni matukia mangapi tumeyasikia kwenye nchi kama Marekani, mtu anavamia mahali na kusababisha vifo kwa raia wasio na hatia?

Tupunguze ujuaji wa kishamba
 
Back
Top Bottom