Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo



Hahahahaha hii picha yako noma kweli kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
 
Hahahahaha hii picha yako noma kweli kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
😁😁😁😁😁😁
 
Sio kwa kupaisha mipira huko,
Rashidi Juma akifika golini anapiga mpira nje.
Ndemla naye anapaisha mipira yake yote.
Salamba ndio alikuwa wa kwanza kipiga mpira juu ya goli.
Kichuya ndio kabisa hata kross anapaisha.
Jamani hivi ndivyo mnavyojifunza mazoezini, mnapaisha hata faulo?
Kila siku mpo mazoezini kwani mnajifunza nini, mbona mnapaisha sana mipira, hamjifunzi kupiga mashuti huku unakimbia na kulenga goli ?
Kama kocha hakufundishi kwanini usijifunze peke yako, kwamba unadrible mpira na unapiga kulenga goli, tena kwa faida yako.
Katika kikosi kilichoanza anayeweza kuangaliwa tena ni
Juuko Murshid, Salamba na Ndemla basi.
Wengine wote hawana kiwango cha kuichezea Simba ya Sasa hivi,
kama wataendelea kubweteka wakisubiri kocha awape mazoezi hata ya kulenga goli.
 
Ni matokeo ya usajili wa maonesho na kukomoa timu nyengine. Mchezaji asiyecheza mechi mara kwa mara hawezi kulinda kiwango chake, hata awe mzuri vipi. Kwa hivyo si sahihi kusajili wachezaji wawili wa kiwango sawa kwenye nafasi moja. Ni sahihi zaidi kusajili wachezaji chipukizi kuwa ndio mbadala wa wa kikosi cha kwanza. Kwa sababu hawa chipukizi watakuwa na uchu wa kuonesha uwezo wao siku wakipata nafasi. Lakini wachezaji nyota kukaa benchi kunawajengea hisia za chuki na viburi dhidi ya wenzao wanaoanza, mbali ya kufutaa kwa uwezo wao. Hata kisu kiwe kikali kiasi gani, hakitaonesha ukali huo iwapo kitabaki muda mrefu kwenye ala yake. Lakini kikosi kipana pia huundwa na wachezaji nyota wachache wa ziada wenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi. Hawa hawavunjiki moyo kwa sababu watapata mara kwa mara nafasi ya kucheza ama kwa kuendana na mfumo ataotaka mwalimu au kujaza nafasi ya aliyeumia. Wachezaji wa aina hii husaidia kuonesha tafsiri nyingine ya kikosi kijana, nayo ni uwezo wa kucheza mifumo tofauti ndani ya mechi moja kwa kuwabadilishia nafasi (rotation) na majukumu (roles) na hivyo kuonekana kama kuna timu mpya imeingia. Kwa ufupi, kuna tofauti baina ya kikosi kipana na mkusanyiko mkubwa ya wachezaji wazuri.
 
Sio kweli kabisa.
Hapo wanaocheza mara kwa mara ni, ( Kichuya, Ndemla, Mzamiru, Juuko, Rashidi Juma, Salamba, Kwasi
Ambao hawachezi sana ni Ali Selemani, Dida, Bukaba na huyo beki mpya Zana.
Hicho ndicho kikosi kilichoanza leo dhidi ya Mashujaa.
Hivyo timu zote kuna wale ambao hawachezi mara kwa mara.
Hivyo huwa wanacheza ni kutojitambua tu kunako waponza na kuendekeza Starehe badala ya mazoezi ya kocha na binafsi.
 
Msikilize Mzungu wenu anavyowadanganya kila siku
 

Attachments

Mkuu nyie mnakikosi kipana cha kucheza bara na zenji?
 

Attachments

Sawa, wanacheza kwa kuzunguka. Inategemea unaangaliaje muda wa kila mchezaji kupata nafasi. Haikuzoeleka, na wenyewe hawakuzowea, kuona wachezaji waliocheza - mathalan - dhidi ya KMC kuanza. Na ndio maana washabiki wa Simba wakajilabu kuwa siku ile wamechezesha Kikosi cha pili. Na ndio maana washabiki wa Simba wanalalamikia kikosi kilichoanza jana, wakisema ni dharau. Kwa nini kiwe kikosi cha pili, kwa nini iwe dharau, iwapo hao uliowataja wanapata nafasi sawa na akina Kagere, Manula, Wawa na Okiwi? Kwa nini washabiki wawasimange waliocheza dhidi ya mashujaa kwamba wanalalamika hawapati nafasi na walipopewa hawakuitumia? Bado huamini kwamba Dida hajapata nafasi ya kuanza sawa na Manila?
 
Yule mchezaji wao mwenye mvi hamna kitu pale, mashujaa walikuwa na moral ya hali ya Juu.
 
Jana hakuna hamna aliye R.I.P, wakati mwingine ni vizuri kula kichapo
 
Hii Timu yetu asipocheza Manula ni shida. Dida anadaka kama anaokota taka taka!!!
 
Pole mkuu Umeongea kwa uchungu sana!!!
 
Mbona wa Yanga wakiingia ambao huwa hawachezi wanaipa Yanga matokeo bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…