Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo

Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo

aisee kichuya hapana,apumzike
Anapapara sana, hatulii na kufikiri afanye nini cha maana ili kuisaidia timu anapokuwa na mpira.
Ikitokea faulo wa kwanza kuikimbilia na anachofanya anajua mwenyewe.
Hata akiwa kwenye sita anapaisha sababu ya papara, akili ya mpira imemtoka kabisa, anawaza umaarufu tu.
Ndemla naye anafuta nyayo, pamoja na mashuti yake mazuri ikitokea faulo hapigi, akipata mpira anapaisha tu, akibahatika kulenga goli ni kwamba lazima afunge goli bila shaka, sijui kwanini hataki kuitumia hii faida aliyonayo, angejifunza kulenga goli tu angepandisha sana thamani yake.
David Bekham alikuwa maarufu kwa kulenga goli tu ktk faulo na shambulizi linalopangwa, chenga alikuwa hazijui kabisa.
Mi najiuliza tu, ivi huko mazoezini hawajifunzi kulenga goli ?
Mashujaa wamepiga mashuti matatu na magoli matatu.
Hakika pongezi kwao mashujaa, wamecheza mpira mzuri mno.
Wakishambulia wanaonana vizuri, wanaibia nafasi ya kufunga na wakipata mpira wa kufunga wanafunga na hakuna kupaisha mpira wala kubutua mpira.
Hakika mimi nina hamu ya kuwaona tena Mashujaa katika mechi nyingine. Mpira wao umenivutia sana, wanautendea haki mpira.
Hawa vijana wetu wanajiona wamesha jua mpira, na hakuna haja ya kujifunza chochote, wamekamilika.
Mashujaa kazeni buti, mmewafundisha mpira hao magoigoi, mpira mnaocheza ndio unaotakiwa kuchezwa.
Nina uhakika wengi wenu mtasajiriwa kwanye timu kubwa kama mtabakisha nidhamu ya mpira mliyoionesha.
Linapofika swala la mpira sisi wadau tunataka kuona mpira mzuri nasio vijana wazuri.
 
Ni matokeo ya usajili wa maonesho na kukomoa timu nyengine. Mchezaji asiyecheza mechi mara kwa mara hawezi kulinda kiwango chake, hata awe mzuri vipi. Kwa hivyo si sahihi kusajili wachezaji wawili wa kiwango sawa kwenye nafasi moja. Ni sahihi zaidi kusajili wachezaji chipukizi kuwa ndio mbadala wa wa kikosi cha kwanza. Kwa sababu hawa chipukizi watakuwa na uchu wa kuonesha uwezo wao siku wakipata nafasi. Lakini wachezaji nyota kukaa benchi kunawajengea hisia za chuki na viburi dhidi ya wenzao wanaoanza, mbali ya kufutaa kwa uwezo wao. Hata kisu kiwe kikali kiasi gani, hakitaonesha ukali huo iwapo kitabaki muda mrefu kwenye ala yake. Lakini kikosi kipana pia huundwa na wachezaji nyota wachache wa ziada wenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi. Hawa hawavunjiki moyo kwa sababu watapata mara kwa mara nafasi ya kucheza ama kwa kuendana na mfumo ataotaka mwalimu au kujaza nafasi ya aliyeumia. Wachezaji wa aina hii husaidia kuonesha tafsiri nyingine ya kikosi kijana, nayo ni uwezo wa kucheza mifumo tofauti ndani ya mechi moja kwa kuwabadilishia nafasi (rotation) na majukumu (roles) na hivyo kuonekana kama kuna timu mpya imeingia. Kwa ufupi, kuna tofauti baina ya kikosi kipana na mkusanyiko mkubwa ya wachezaji wazuri.
Kwako Mwalimu Kashasha ....agiza bili leta huku nilipe.Wakati ndio utaongea macho na masikio tunaiombea tu wawe vizuri tuone burudani nyingine kama za Nkana.Ila kusiwe na visingizo..
 
Tukumbushane tu...
WARRIORS ni MASHUJAA , kwa kiswahili.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anapapara sana, hatulii na kufikiri afanye nini cha maana ili kuisaidia timu anapokuwa na mpira.
Ikitokea faulo wa kwanza kuikimbilia na anachofanya anajua mwenyewe.
Hata akiwa kwenye sita anapaisha sababu ya papara, akili ya mpira imemtoka kabisa, anawaza umaarufu tu.
Ndemla naye anafuta nyayo, pamoja na mashuti yake mazuri ikitokea faulo hapigi, akipata mpira anapaisha tu, akibahatika kulenga goli ni kwamba lazima afunge goli bila shaka, sijui kwanini hataki kuitumia hii faida aliyonayo, angejifunza kulenga goli tu angepandisha sana thamani yake.
David Bekham alikuwa maarufu kwa kulenga goli tu ktk faulo na shambulizi linalopangwa, chenga alikuwa hazijui kabisa.
Mi najiuliza tu, ivi huko mazoezini hawajifunzi kulenga goli ?
Mashujaa wamepiga mashuti matatu na magoli matatu.
Hakika pongezi kwao mashujaa, wamecheza mpira mzuri mno.
Wakishambulia wanaonana vizuri, wanaibia nafasi ya kufunga na wakipata mpira wa kufunga wanafunga na hakuna kupaisha mpira wala kubutua mpira.
Hakika mimi nina hamu ya kuwaona tena Mashujaa katika mechi nyingine. Mpira wao umenivutia sana, wanautendea haki mpira.
Hawa vijana wetu wanajiona wamesha jua mpira, na hakuna haja ya kujifunza chochote, wamekamilika.
Mashujaa kazeni buti, mmewafundisha mpira hao magoigoi, mpira mnaocheza ndio unaotakiwa kuchezwa.
Nina uhakika wengi wenu mtasajiriwa kwanye timu kubwa kama mtabakisha nidhamu ya mpira mliyoionesha.
Linapofika swala la mpira sisi wadau tunataka kuona mpira mzuri nasio vijana wazuri.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Si kwa povu hili
 
vyuraaaa katika ubora wenu!! Umeandika as if unakimbizwa! Au unatumia kasimu ka touch. Maneno kibao yana errors hats hayaeleweki " Mara Sumba (sijui ndo simba?) vipi mkuu!!
Kwahio hapa mbumbumbu alichoandika hakina errors
 
Sawa, wanacheza kwa kuzunguka. Inategemea unaangaliaje muda wa kila mchezaji kupata nafasi. Haikuzoeleka, na wenyewe hawakuzowea, kuona wachezaji waliocheza - mathalan - dhidi ya KMC kuanza. Na ndio maana washabiki wa Simba wakajilabu kuwa siku ile wamechezesha Kikosi cha pili. Na ndio maana washabiki wa Simba wanalalamikia kikosi kilichoanza jana, wakisema ni dharau. Kwa nini kiwe kikosi cha pili, kwa nini iwe dharau, iwapo hao uliowataja wanapata nafasi sawa na akina Kagere, Manula, Wawa na Okiwi? Kwa nini washabiki wawasimange waliocheza dhidi ya mashujaa kwamba wanalalamika hawapati nafasi na walipopewa hawakuitumia? Bado huamini kwamba Dida hajapata nafasi ya kuanza sawa na Manila?
Kocha anaangalia, anayepaform vizuri mazoezini ndiye anayepangwa.
Huoni Messi wa Barcalona anacheza kila mechi.
Timu inapokuwa ktk kushindania ubingwa, mchezaji bora ndiye anayepangwa na sio kupanga kwa kuangalia zamu.
Cha msingi mchezaji akitaka kuanza kikosi cha kwanza ni lazima aoneshe kiwango bora ktk mazoezi.
Kagere anaanza kwakuwa tu anaweza na sio vinginevyo. Hata mechi ya Simba na Mashujaa, akina Ali Selemani hawakutakiwa kuanza.
Kocha alizingatia ubinadamu tu na kimemgharimu.
Akiendelea kupanga kwa kuzingatia zamu ya kutoa nafasi kwa wachezaji wote atafungwa na kupoteza kibarua chake.
Kila timu kuna wachezaji wanaokalia benchi.
Jonas Mkude alikalia benchi msimu mzima wa kocha Amog lakina alipoboresha kiwango chake akapata namba ya kudumu.
Tofauti na hao vijana wakipewa nafasi badala ya kujituma nakuwa makini ili waisaidie timu wanarukaruka tu.
Utaendeleaje kuwapanga katika mechi za ushindani katika kiwango hicho.
Hao uwezo wao ndio umeishia hapo ni swala la kuamua tu, tuwapende wao au mafanikio ya timu.
Kuna baadhi yao hapo wanaweza kujirekebisha siku za usoni, lakini hao akina Ali Selemani ni bora wagombee tu uongozi wa timu.
 
Back
Top Bottom