Mashulizi Dhidi ya Iran Yalenge Watawala, Wananchi Walindwe Au Wasaidiwe Kuingia Mataifa Jirani.

Mashulizi Dhidi ya Iran Yalenge Watawala, Wananchi Walindwe Au Wasaidiwe Kuingia Mataifa Jirani.

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Mods, tafadhali naomba isomeke MASHAMBULIZI, na siyo MASHULIZI.

Siku zote nchi inapokuwa katika shida ya amani, chanzo huwa ni watawala waovu wenye kiburi. Israel na Marekani, wanajua kuwa:
1. Wahanga wakubwa wa kwanza wa utawala katili wa Ayatollah, ni wananchi wa kawaida wa Iran.
2. Wananchi wa Iran hawana uhuru hata wa kupanua vinywa vyao dhidi ya watawala wao dhalimu.
3. Siku za karibuni Dunia imeshuhudia jinsi wananchi wa Iran walioandamana walivyouawa kinyama na utawala dhalimu wa Ayatollah.
4. Wananchi wa Iran wanaishi kwenye umaskini mkubwa huku nchi yao ikiwa imejaa utajiri mkubwa wa mafuta. Pesa yote ya mafuta inaishia kutengenezea makombora, vinu vya nuclear na ufisadi wa watawala.
5. Wananchi wa Iran hawanufaiki chochote na makombora wala vinu vya nuclear.

Wananchi hawa wa Iran, walioishi kwa mateso makubwa yaliyosababishwa na watawala dhalimu, hawastahili kuongezewa mateso, bali kuonewa huruma. Nimeona video zinazoonesha wananchi wakishangilia baada ya kusikia muuaji wa watoto na ndugu zao, Ayatollah, naye ameuawa. Furaha yao hiyo isibadilishwe kuwa huzuni ya misiba yao au ndugu zao.
Ningekuwa nina uwezo ningewashauri Trump na Netanyahu wafanye kila njia ya kuwalinda hao wananchi, ikiwezekana hata baadhi kwenda kuwahifadhi kwenye mataifa jirani na kuwahudumia, huku watawala wauaji wa Iran wakiendelea kupata malipo ya matendo yao. Hata askari wa Iran ambao hawakuwa wakifurahia matendo ya watawala, wapewe nafasi ya kuondoka Iran bila ya kudhuriwa. Hilo litapeleka ujumbe kwa wananchi kuwa mashambulizi yanayoendelea ni kwaajili ya ukombozi wao.
 
Back
Top Bottom