Masihara dhidi ya COVID-19 yamtokea puani, adakwa na Polisi

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Polisi Ruvuma wanamshikilia Ibrahimu Bukuku kwa kusambaza ujumbe WhatsApp kupotosha kuhusu dawa ya Corona, ukisomeka, " Dawa ya corona twanga pilipili kichaa sufuria 1 halafu changanya na maji vikombe 5, kunywa kutwa mara 7 kwa siku 3, siku ya 4 chuma upupu kisha jipake".


Jeshi la Polisi linamshikilia Ibrahim Peter (26) ambaye Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya Sayansi ya biolojia.

Anatuhumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wa kupotosha jamii kuhusiana na Dawa ya #COVID19 katika makundi ya WhatsApp kwa kutumia simu yake ya mkononi

Miongoni mwa ujumbe alizosambaza ni kwamba ‘Dawa ya #COVID19 inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji vikombe vitano na kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu kisha jipake mwili mzima’.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika Kijiji cha Mnyele Wilaya ya Nyasa na kitendo alichofanya ni upotoshaji, taratibu zinakamilishwa ili aweze kufikishwa Mahakamani.
 
Sasa kwa hiyo dawa ni nani akaichukulia serious akamripoti jamaa? Ni kweli kuna mtu ametumia hiyo dawa, imemuathiri na ameamua kwenda kushtaki?

Kuna katuni ilisema imemeza kondomu ili kujikinga na ukimwi nafikiri hakuna aliyemfuata kwakuwa wote tunajua hakuna mtu timamu wa kufanya hivyo.
 
Aliharibu Hapo kwenye upupu, kwenye pilipili hayuko mbali na ukweli, pilpili ni una vitamni C za kutosha kupandisha Kinga ya mwili
 
Sijui nani ni kichaa zaidi kati aliyepost whatsapp au waliomkamata!!!
 
Ingekuwa nchi zingine uyoo kijana angeambukizwa virusi vya corona kwa makusudi ,

Alafu atumie dawa yake kujibu corona kama atapona basi iyoo dawa wapewe wagojwa wa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa nchi zingine uyoo kijana angeambukizwa virusi vya corona kwa makusudi ,

Alafu atumie dawa yake kujibu corona kama atapona basi iyoo dawa wapewe wagojwa wa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana,huyu alikuwa anafanya utani,hakuwa serious na nashangaa resource zimetumika kumkamata,wale wanaotoka na product kabisa na wanaitangaza kuponya corona.

Hawa ndo unamuweka wodi pale Amana na akiupata atumie hiyo dawa yake akipona kweli Basi dawa inaidhinishwa
 
inawezekana bwana mdogo yuko sahihi,polisi walitakiwa kuifanyia utafiti wa kitabibu hiyo dawa kabla ya kumkamata
 
Polisi wetu bhana! Huwa wanapenda kuvalia njuga vitu vya kipuuzi puuzi na ambavyo havina kichwa wala miguu! Sijajua ni kwa nini hawapendi kujikita kwenye kutoa elimu kwa raia kuhusu mambi mbalimbali.

Anyway, pongezi nyingi ziwafikie.
 
Jeshi la Polisi linamshikilia Ibrahim Peter (26) ambaye Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya Sayansi ya biolojia

Anatuhumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wa kupotosha jamii kuhusiana na Dawa ya #COVID19 katika makundi ya WhatsApp kwa kutumia simu yake ya mkononi

Miongoni mwa ujumbe alizosambaza ni kwamba ‘Dawa ya #COVID19 inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji vikombe vitano na kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu kisha jipake mwili mzima’

Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika Kijiji cha Mnyele Wilaya ya Nyasa na kitendo alichofanya ni upotoshaji, taratibu zinakamilishea ili aweze kufikishwa Mahakamani
 
Mwaka huu tutaona na kusikia mengi!

Sent using kidole gumba
 
Hongera polisi kwa kazi nzuri .Wapoteshaji wengi tu fanyeni kazi without fear or favour/ bila woga au upendeleo 😎
 
Alikuwa anafikiria nini?

Hali ni mbaya sana, changamoto ya upumuaji imekithiri tuchukue hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…