Masihara dhidi ya COVID-19 yamtokea puani, adakwa na Polisi

Masihara dhidi ya COVID-19 yamtokea puani, adakwa na Polisi

Serikali bwana 😂😂😂
 
mbona mshua alisema hivihivi wakamchukue na yeye
 
Huu ni upendeleo wa wazi kabisa, mbona bosi wa mizaha hakamatwi mara oh Barakola zina Corona, mara utamsikia akisema dawa iliyopulizwa inasababisha Corona hiyo ni michache tusisahau kufukiza .....

. Challenge ni afya unaita watu wa USALAMA na DINI

Hakuna nchi rahisi kuiongoza kama Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo alichokisema dogo ndio sheria watu wataifata? Hivi kuna mwenye akili timamu kweli atafanya huo ujinga aliosema dogo? Polisi wetu waache hizi mambo aisee.
 
ku
Jeshi la Polisi linamshikilia Ibrahim Peter (26) ambaye Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya Sayansi ya biolojia

Anatuhumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wa kupotosha jamii kuhusiana na Dawa ya #COVID19 katika makundi ya WhatsApp kwa kutumia simu yake ya mkononi

Miongoni mwa ujumbe alizosambaza ni kwamba ‘Dawa ya #COVID19 inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji vikombe vitano na kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu kisha jipake mwili mzima’

Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Simon Maigwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika Kijiji cha Mnyele Wilaya ya Nyasa na kitendo alichofanya ni upotoshaji, taratibu zinakamilishea ili aweze kufikishwa Mahakamani
kumbe udom
 
Kwa hiyo alichokisema dogo ndio sheria watu wataifata? Hivi kuna mwenye akili timamu kweli atafanya huo ujinga aliosema dogo? Polisi wetu waache hizi mambo aisee.
Dogo Hana kesi pale,ila lokapu atakaa
 
😂 😂 😂 😂.....Yani kuna issue unaweza kujua ni utani vile,mpaka kamanda wa mkoa anazungumzia kitu kama hiki
 
Huo ujumbe yeyote atakaesoma anajua asilimia 100 ni utani tu wa kawaida
 
Aliharibu Hapo kwenye upupu, kwenye pilipili hayuko mbali na ukweli, pilpili ni una vitamni C za kutosha kupandisha Kinga ya mwili
Upupu una vitamini D & E kwa wingi. Kinga kwnye ngozi inakuwa imara sana.

Sent using iphone pro max
 
Jeshi la polisi wametoa tamko kwa jamii kupinga huo uzuri wa jamaa au wameacha hiyo habari hivyo hivyo na kujipa kazi ya kumkamata?
Trump alisema mambo kama haya, wahusika walitoa onyo kwa umma kutofuata ushauri wa rais, na si kumkamata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom