Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Wazungu wanao msema usemao nionyeshe rafiki yako nikwambie wewe ni mtu wa aina gani. Maana yake marafiki zako ndio wanaokutambulisha mbele ya wastaarabu. Ni msemo umekuwepo kwa miaka mingi japo unajulikana kwa wale wasomaji wa vitabu vya kingereza.
Mwalimu Nyerere alikuwa na Hayati Rashid Kawawa, wakati akihutubia hupenda kumtambulisha kwa kulitaja jina lake la kwanza la Rashid. Alikuwa ni msiri wake waliyeshibana vyema, nakumbuka miaka ile pale ikulu alikuwa akitamka Rashid atageuza shingo yake na kumtazama akiwa amekaa kushoto kwake.
Awamu ya nne ilipoingia ikulu Mheshimiwa Jakaya Kikwete akaja na katibu mkuu wa CCM ambaye ni mwanajeshi mwenzake mstaafu mzee Makamba, Kuonyesha alivyoshibana haraka sana akamuondoa Mzee Mangula kutoka katika nafasi ya ukatibu mkuu ili Makamba achukue cheo chake. Hawa wameshibana sana tangu ujanani wakiwa na siri nyingi wanazozifahamu za miaka na miaka.
JK ni mpenda mno masikhara, yapo ndani ya damu yake na hawezi kuongea bila ya kuchomeka maneno mawili matatu ya utani. Makamba nae ni mule mule anamopita JK. Kauli za kebehi kwa wajane wa marais waliokuwa pale ukumbini zilipokelewa kwa tabasamu lile lile la miaka yote la bosi wake wa zamani aliyemuamini na kumpa nafasi ya juu kabisa ndani ya CCM.
Labda ni kuteleza ulimi kwa mtu mzima mwenye miaka 84 na Rais SSH akatumia busara za hapo kwa hapo za kumfichia aibu mzee Makamba pale ukumbini akitumia kiswahili kile kile laini na neno moja la kingereza kwamba mzee alikuwa na emotions wakati anatoa hotuba yake, wenye akili tulimuelewa kwanini aliamua kumsitiri mtu wa umri wa Baba yake akimuita kaka yake.
Ni yale yale ya wazungu na msemo wao nionyeshe rafiki yako nikwambie wewe ni mtu wa aina gani. Bashiru Ally Kakurwa kwa kumtazama tu akiongea ni mtu makini na mwenye kuchagua aongee lipi na kwa wakati upi, anayo kauli yenye mamlaka na ujumbe wake unafikirisha kwa msikilizaji. JPM alituonyesha yeye ni mtu wa aina gani kwa kumpa kipaumbele Bashiru Ally. Tulimjua ni mtu wa aina gani pale tulipomtazama rafiki yake.
Pengine maneno ya mzee Makamba ni matokeo ya umri kuwa umesogea, mzee wa miaka 84 hawezi kupanda jukwaani akawa sawa na mwanasiasa mwenye miaka 45 hadi 60. Na nadhani ni sababu baadhi yetu tunamshauri mzee Wasira Stephen aachane na siasa, kwani ni rika hilo hilo la Makamba.
JK analo la kubeba katika kauli iliyochukuliwa kama ni dhihaka ya Mzee Makamba wakati akihutubia. Hawezi kukwepa lawama kutoka kwa wale wenye kufikiria masuala ya kisiasa kwa kina. Tumemuona yeye mwenyewe kupitia kwa haiba ya Mzee Makamba.