Masikhara ya JK nyuma ya uwepo wa Makamba nionyeshe rafiki nikwambia wewe mtu wa aina gani

Ungekuwa ni mtu wa CCM ningeweza kukuelewa lakini CHADEMA hata siku moja huwezi kuongea maongezi chanya lazima ukosoe tu.

Usisahau kipindi CHADEMA wanapiga kelele kuwa Magufuli amefariki mliwakebehi. Hadi walipotishia kufanya press conference ya kutangazwa kifo Cha Magufuli ndipo Mama Samiah akakurupushwa usiku wa manane.

Nina uhakika Magufuli akirudi leo Atawaomba msamaha CHADEMA, na ndio atagundua CHADEMA ndio marafiki zake wa kweli.
 
kuna Viongozi wengi tu wamefariki wakiwa madarakani ukianzia kwa Rais Karume Mkubwa, Sheikh Anri Abeid, Sokoine, Horace Kolimba, Salome Mbatia, n.k

kwanini tumekimbilia kuhisi kuwa kasemwa mtu fulani ?

Waovu Mara nyingi hujishuku. Sijasikia wafuasi wa Maalim Seif wakilalamika.
 
Kuna nini kipya ambacho kilikuwa hakijulikani? Kikwete, Kinana, Makamba na kundi lao lote walifurahia sana kutwaliwa kwaa bwana yule... Ni watanzania tu mnapenda kujadili mambo ambayo yako wazi na yale ambayo hayako wazi mnayaacha. Alichosema huyu Makamba ni sehemu ndogo tu ya undani wao.
 
Kufurahia kutwaliwa kimya kimya wengi tu walifurahia, kuna waliofanya sherehe kabisa kwa kwenda disco usiku ule ule kujipongeza.

Tatizo ni hizi hekima mbovu za uzeeni za kusema kabisa kwamba umefurahi juu ya kifo cha JPM mbele ya mjane aliyefunga safari kutoka alipotoka kwenda mkutanoni pale. Inakuwa kama vile mnamsuta yeye kwa kuwa mahali pale na kwa kuolewa na marehemu. Mzee Makamba amefanya jambo la kipuuzi sana kuongea vile hadharani.

Kauli huwa inaumba, chunga sana kitokacho kinywani mwako huweza kukuharibia maisha yako yote. Kitokacho mdomoni mwako kinakushtaki moja kwa moja kwa Mungu. Pia upo msemo Mungu hadhihakiwi.
 
kuna Viongozi wengi tu wamefariki wakiwa madarakani ukianzia kwa Rais Karume Mkubwa, Sheikh Anri Abeid, Sokoine, Horace Kolimba, Salome Mbatia, n.k

kwanini tumekimbilia kuhisi kuwa kasemwa mtu fulani ?
Watu wamechukua mbili wakajumlisha na mbili jawabu likaja nne.
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Na madaraka yanalevya kweli kweli. Sasa hivi kina Kikwete na Kinana na pia huyu mzee wameshasahau kuwa walikuwa wameshapotea mazima. Wamerudi kwa kiburi na dharau kali huku hawajui ya kesho.
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Na madaraka yanalevya kweli kweli. Sasa hivi kina Kikwete na Kinana na pia huyu mzee wameshasahau kuwa walikuwa wameshapotea mazima. Wamerudi kwa kiburi na dharau kali huku hawajui ya kesho.
JK Kwa kuwa na upande anaoshabikia anajishushia heshima yake japokuwa anajaribu kadri awezavyo aonekane ni mstaarabu.
 
Huyo babu ni kawaida yake kuropoka sijui hata watu mnashangaa nini,na hilo jopo lake litashangaa siku ataporoka chanzo halisi cha kfo cha jiwe.endeleeni kumpandisha jukwaani huvyohivyo
 
Nenda basi mahakamani, idiot
 
"JPM alituonyesha yeye mi mtu wa aina gani kwa kumpa kipaumbele Bashiru Ally."
Inawezekana hapa ukawa umewachanganya wasomaji wako wengi kwa hayo maneno kumhusu JPM na Bashiru.

Binafsi sijui mfanano wa karibu kati ya hao wawili, ila ninakumbuka maneno aliyowahi kutamka Bashiru Ali kuhusu chama kinachounda serikali kulazimika kuachia madaraka kwa matakwa ya wananchi wakati wa uchaguzi.

Yeye kwa maoni yake haoni hilo likitokea huku chama kikishikilia dola na nyenzo zake zote! sijui kama kuna mfano mwingine wowote uliowaweka hawa watu wawili karibu zaidi.
 
Mwenyekiti Mstaafu na anayeendelea walishampatia twisheni mzee asiye na breki aongee nini na hakuna litakalotokea.

Natabiri, uchaguzi wa 2025 utakuwa baina ya CCM dhidi ya JPM. Wapinzani watakuwa watazamaji
Hilo likitokea,nchi itafaidika sana.

Lakini najua ni jambo lisilowezekana kwa walafi walioko CCM. Kwao maslahi ndio kila kitu. Wakilambishwa asali akili zote zinawaruka.
 
Hizi ni porojo zingine!

Bashiru hana hizo sifa unazompa. Ni mganga njaa tu ambaye alipopewa madaraka alilewa akaanza kutumia rasilimali za umma kulangua wapinzani!

Kwa viwango vyovyote Magufuli alikuwa kiongozi muovu. Munaomuona vinginevyo ni wale muliofaidika na uovu wake kwa kupata mlichokuwa hamsitahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…