Masikini Lowassa, nilihisi haya yatamkuta, yamemkuta

Bwashee niko mjini kitambo Sana na kinywaji nilikuwa napata hapo Puma wakati huo ikiwa Bar

Wadanganye Wagogo Wenzako huko Kongwa 😂😂
Kwa taarifa yako hapo mahala palikuwa BP, tukinywa supu ya ghoulash hapo na kina mzee Bob Makani.
Na kama unafikiri kuifahamu BP miaka hiyo ndo long time basi wewe bado pusi hapa mjini.
 
Kuyataja maovu yako ni kukuhukum? Endeleni na viwanda vya dhambi huko makanisani kwenu eti mkionywa mnahukumiwa.

Mnapoteza muda bora mkanywe pombe tu.
Wewe unaonywa na nani? Na hayo mamlaka ya kuonya amekupa nani?
 
Mpumbavu wewe, kwanza Lowassa siyo masikini
Pili, Magufuli, Maalim Seif, Anna Mghwira hawa wagombea 2015 wamefariki walizulumu viwanja wapi na wakalaaniwa na nan
 
Masahihisho kidogo:

✍️Yesu Kristo aliishi miaka 33½ pekee na siyo 36 hapa duniani.

✍️Mgawanyo wa miaka ya maisha yake ni;

• Miaka 30 ni ya kuishi maisha ya kawaida ya kujifunza na kujiandaa kwa ajili ya huduma yake ya kuukomboa ulimwengu na wanadamu kutoka ktk dhambi na matokeo yake

• Miaka 3½ ilikuwa miaka ya kutimiza kusudi la kuja kwake duniani. Ilikuwa ni miaka ya kutangaza habari njema ya wokovu na ukombozi wa ulimwengu. Ilikuwa ni miaka ya vita na mapambano dhidi ya utawala wa shetani hadi kupatikana kwa ushindi pale msalabani Golgotha. Akafa na dhambi zote za ulimwengu. Akazikwa nazo chini. Siku ya tatu akafufuka kwa ushindi mkuu akiziacha dhambi zote chini. Shetani na kazi zake akawa ameshindwa totally.

Mtu yeyote akikiri kwa mdomo wake na kuamini moyoni mwake kuwa haya yalifanyika kwa ajili yake ya kuwa Yesu Kristo aliteswa, akafa, akazikwa na siku ya tatu alifufuka toka kwa wafu, naye mtu huyu ataokolewa!.

Yesu Kristo ameketi juu ya kiti chake cha enzi. Ni mfalme wa wafalme wote duniani na mbinguni!
 
 
Huwa hatujifunzi kwa sababu huwa hatuamini yanayowatokea wenzetu nasi siku moja yatatutokea tena even worse kuliko yao !!
Wenye Nguvu waache kudhalilisha watu maana siku yao ya majuto itafika tu !!🙏🙏🙏
 
Du.... nyumba ya Sanaa, ule msonge, wewe kweli kijana mwenzangu wa siku nyingi!
Wengi kiuhalisia hawamjui Lowassa, umemuelezea kiukweli kabisa.
wengi nadhani humu hawajakuelewa. sidhani kama umeleta mada kwa nia mbaya ya kumchafua mwendazake Edo. Umeeleza uhalisia. naamini wengi tulikuwa tunam admire Edo kama kiongozi. Lakini alikuwa na makando kando mengi. Na kwa vile alikuwa kiongozi wa serikali, haya madudu yake hayakwepeki. Especially kwa sababu mengi aliyafanya akiwa na dhamana ya madaraka.

In all, binadamu wote tuna makandokando yetu. Ingawa pia, kama Masanja niliwahi kupewa dhamana ya uongozi ndani ya nchi yangu, nikitangulia mbele ya haki, watu watanizungumzia kadri ya walivyonifahamu. Kama niliwahi kumzulumu mtu, yes watasema. Kama nilikuwa fisadi....Yes they are free to say it. Kwangu mimi sioni shida ipo wapi, kama watu wanaongelea yale uliyoyafanya ukiwa hai au kwenye nafasi fulani. Ni maisha yako. Wacha watu waongee. Kama wanaweza kuongelea mazuri yangu, wacha hata mabaya yangu wayaongee.

Kujificha chini ya kivuli cha "leta ushahidi" we all know, nchi yetu inafanyaje kazi. Mwisho wa siku, kila mtu humu ana story yake kuhusu viongozi wetu wa umma. refer stories za akina Makonda, Sabaya nk. kwamba wamepata second chance....haitawahi kufuta ujinga na udhalimu waliowafanyia wasio na hatia. ni kanuni ya maisha.

Nikiishi kwa wizi na utapeli, kwa kuwadhulumu. watu, hata kesho nikiokoka, nikaanza kuchangia mamilion kanisani, au msikitini.. haitafuta story ya utapeli wangu. Ingawa waumini/wanausharika wenzangu hawatapenda "hiyo dark side" iongelewe.

Ndugu yetu Edo apumzike alipoaandaliwa na Muumba wake.

Masanja
 
Waswahili Wanasemaga Maneno kuntu !
 
Ni kweli mkuu, wengi wanafikiri nalimfahamu Lowasa kupitia Luninga. Wengi hawajui kuwa alikuwa na kampuni yake ikiitwa Barare, na nilifanya kazi nao.
Hili nililobandika si uzushi wala majungu, ni kweli tupu.
 
Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…