Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,534
- 7,866
Masikini Mh Edward Ngoyai Lowassa, mwanasiasa machachari tuliyemjua kwa miaka mingi, ametangulia mbele za haki.
Si vizuri kumuongelea vibaya marehemu, lakini hata Rais Mwinyi aliwahi kusema, maisha ninkitabu, tuishi ili wakao kisoma wafurahie hadithi ya maisha yako.
Hisia zangu ni ile miaka ya 94-2000 ambapo Lowassa alikuwa waziri wa Ardhi.
Alitenda kosa ambalo kimsingi nikajiambia, huyu mzee kajichotea laana isiyosameheka.
Lowassa kama watu wengi wa kaskazini wanapenda sana ardhi, iwe ya kudhulumu au haki. Katika hili nasikitika kusema alidhulumu ardhi ya KKKT Mbezi Beach, pale Tangi Bovu.
Mzee mmoja maarufu anaitwa Arnold Kileo, alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Breweries. Mzee Kileo alitoa ardhi yote karibia eka tatu au nne kwa kanisa.
Maombi yalipoenda wizarani kubadili jina, kiwanja kikakatwa nusu bin nusu.
Nusu moja akajimilikisha kwake Lowasa, ndugu zake na marafiki, kina Kimbisa, na nusu ndiyo akakibakishia kanisa.
Waumini wa hapo walishangaa kwani walijua Lowasa ni Mluteri, kwa nini afanye vile?
Wakamwomba Baba Askofu Sendoro akamwone waziri na kumsihi arudishe ile nusu ya eneo, Lowassa alikataa.
Alipokataa Baba Askofu alishukuru na kumtakia heri, Lawassa asijue kuwa hapo tayari ndipo laana ilipotoka.
Cha kushangaza, kila aliyeweka mradi katika kile kiwanja kilichoporwa, mradi ulikufa, TANESCO walikodi ofisi pale wakaishia kuhama. Hata jengo lililo na benki ya NMB pale nayo linakosa wapangaji.
Tukija kwa ndugu yetu Lowassa ,safari yake ya kisiasa ilienda kusuasua. Hata zlipochaguliwa waziri Mkuu, hakudumu.
Lowassa akakosana na rafikiye mkubwa, Jakaya Kikwete, na marafiki hao wakawa maadui.
Mwisho alihama CCM kabisa, na uamuzi bado haukuwa na tija, akarudi.
Lowassa akawa kama mwanasiasa anayetangatanga nyikani.
Pale kanisa la Mbezi KKKT, Lowassa hakuwahi kuslikwa shughuli yoyote ya harambee, ingawaje Sumaye alialikwa mara nyingi.
FUNZO, jamani tumwogope Mungu na tumtumikie hata tukiwa na vyeo vikubwa.
Kwa kufariki akiwa na miaka 70, Lowassa alikuwa bado mdogo mwenye miaka si chini ya 15-20 mbele. Lakini yote ni mapenzi ya Mungu RIP Edward Ngoyai Lowassa.
Shida ni pale unapokuwa na mentality kuwa KIFO ni laana au Adhabu.
Mention any Pop, Saint , Nabii, Mtume etc etc ambae hajawahi kuwfa kwa kuwa ni mtu Mzuri,
You are such a naive na hizo story za mental slavery , Lowassa muda wake is due Kama wako utakavofika, that does not mean anything
Kama ulilkuwa hujui , Lowassa was a great man and a prophet of our time,
hata hao unaowaita marafiki zake wakubwa, ni ushamba wako …… EDO hajawahi kuwa na urafiki wa karibu na huyo mtu, they just grew up pamoja and known to each other….. that doesn’t mean friendship.
Edo was genuine man , na aki interact na wewe , he interacts with pure heart and love ….. he was such a gentleman and true soul
Hao unaowaita marafiki zake, hajawahi kuwa na urafiki nae , he knew him and helped him mentally and financially to shape his career path…… and ofcourse JK alifanikiwa sana kwa msaada wa EDO.
.wakati Edo anaomba kura ya Urais, he never asked for a favor from him , he tried for his best level , only it did not work , and remained pure man.
Alienda pia kumpongeza JPM kuonesha…. Heshima na akaomba wafuasi wake waisapoti serikali mpya ya JPM
Such a gentleman with maturity , he always wanted peace
Sio hao wengine waliojaza unafiki kwenye nyuso zao na uzandiki
The better thing is that , no one will get alive out of this world .