Masikini Lowassa, nilihisi haya yatamkuta, yamemkuta

Masikini Lowassa, nilihisi haya yatamkuta, yamemkuta

Ishini vizuri na watu acha maneno mengi

Tuwe tayari kujifunza na sio kupinga pinga tu
Niko tayari kujifunza kwa Yesu Kristo pekee yake aliye mfano na mwanadamu mkamilifu.

Lakini nijifunze nini toka kwa mtu mwenye pomposity na anayehukumu wengine?

By the way, hebu nipe mfano mmoja tu wa kujifunza toka kwako au kwa mleta mada.

Kama una Kristo ndani yako na una - display sura na mfano wa maisha yake aliyoyaishi hapa duniani, nitakuiga na kujifunza toka kwako.
 
Mwinyi ndio SI unit ya mtu asiyelaaniwa?
Yesu alikufa na miaka 30 na kitu, naye alilaaniwa?

nimekupa Like kaka!
Inasemekana YESU alikufa Akiwa na 36yrs!
Nadhani jambo la Msingi ni Malengo!
MUNGU huwapangia watu malengo ktk kuishi…
Ukishayatimiza Malengo Then anakuchukua!
Unaweza Ishi Miaka 49 lakini ukafanya Mengi makubwa sawa au zaidi na Alieishi miaka 79Kaka!
 
Masikini Mh Edward Ngoyai Lowassa, mwanasiasa machachari tuliyemjua kwa miaka mingi, ametangulia mbele za haki.

Si vizuri kumuongelea vibaya marehemu, lakini hata Rais Mwinyi aliwahi kusema, maisha ninkitabu, tuishi ili wakao kisoma wafurahie hadithi ya maisha yako.

Hisia zangu ni ile miaka ya 94-2000 ambapo Lowassa alikuwa waziri wa Ardhi.
Alitenda kosa ambalo kimsingi nikajiambia, huyu mzee kajichotea laana isiyosameheka.
Lowassa kama watu wengi wa kaskazini wanapenda sana ardhi, iwe ya kudhulumu au haki. Katika hili nasikitika kusema alidhulumu ardhi ya KKKT Mbezi Beach, pale Tangi Bovu.

Mzee mmoja maarufu anaitwa Arnold Kileo, alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Breweries. Mzee Kileo alitoa ardhi yote karibia eka tatu au nne kwa kanisa.
Maombi yalipoenda wizarani kubadili jina, kiwanja kikakatwa nusu bin nusu.
Nusu moja akajimilikisha kwake Lowasa, ndugu zake na marafiki, kina Kimbisa, na nusu ndiyo akakibakishia kanisa.

Waumini wa hapo walishangaa kwani walijua Lowasa ni Mluteri, kwa nini afanye vile?
Wakamwomba Baba Askofu Sendoro akamwone waziri na kumsihi arudishe ile nusu ya eneo, Lowassa alikataa.

Alipokataa Baba Askofu alishukuru na kumtakia heri, Lawassa asijue kuwa hapo tayari ndipo laana ilipotoka.

Cha kushangaza, kila aliyeweka mradi katika kile kiwanja kilichoporwa, mradi ulikufa, TANESCO walikodi ofisi pale wakaishia kuhama. Ilikuwepo supermarket ya Imalaseko, Dry Cleaner na Gym , vyote vimekufa.
Hata jengo lililo na benki ya NMB pale nayo linakosa wapangaji.

Tukija kwa ndugu yetu Lowassa ,safari yake ya kisiasa ilienda kusuasua. Hata zlipochaguliwa waziri Mkuu, hakudumu.
Lowassa akakosana na rafikiye mkubwa, Jakaya Kikwete, na marafiki hao wakawa maadui.
Mwisho alihama CCM kabisa, na uamuzi bado haukuwa na tija, akarudi.
Lowassa akawa kama mwanasiasa anayetangatanga nyikani.

Pale kanisa la Mbezi KKKT, Lowassa hakuwahi kuslikwa shughuli yoyote ya harambee, ingawaje Sumaye alialikwa mara nyingi.

FUNZO, jamani tumwogope Mungu na tumtumikie hata tukiwa na vyeo vikubwa.
Kwa kufariki akiwa na miaka 70, Lowassa alikuwa bado mdogo mwenye miaka si chini ya 15-20 mbele. Lakini yote ni mapenzi ya Mungu RIP Edward Ngoyai Lowassa.
Point Ni kubwa San umeongea juu ya watu wa kazikasini kupenda ardhi Hilo si kubishii na wengi wamekufa vibaya mno kwa Kungangania mashamba ya watu

Na I wenda ikawa laana imemtafuna mzee huyu ambae ghafla aliporomoka kisiasa
 
zungumzia na mpunga aliokua nao mpka anakufa alafu kama nao ni laana basi hizo laana zake ni unyama sana......
 
Point Ni kubwa San umeongea juu ya watu wa kazikasini kupenda ardhi Hilo si kubishii na wengi wamekufa vibaya mno kwa Kungangania mashamba ya watu

Na I wenda ikawa laana imemtafuna mzee huyu ambae ghafla aliporomoka kisiasa
Mkuu watu wanajisahau, ukila sahani moja na mali za Mungu, sadaka etc, imekula kwako.
 
Kisa chako kinaweza kuwa na funzo ila kukihusisha na kifo cha Lowasa ni kupotoka! Kwamba laana ya 1994 ndio imekuja kujibu 2024? Kwamba maisha aliyoishi Lowasa sio ya mafamikio? Wewe ambaye hukuiba kiwanja cha kanisa, umfikia alikofika? Je, sio imani ya wakristo kwamba atubuye dhambi husamehewa? Kwa nn unambebesha jambo ambalo yumkini alishasamehewa na Mungu wake?
Fanya toba leo, haya unayosema leo ni amri ya Mungu kwamba samehe 7*70 lakini wewe kwa miaka 30 bado uko na kinyogo kwa marehemu.
Mpumbavu kweli mleta màda... Lowasa alitungiw kashfa kibai za magumashi ... Kungekuwana Hilo mbona kina Nape na CCM taka wangelishupalia
 
Mtoa mada kulingana na ID yako utakuwa unamfahamu Amani Nzugile Jidulamabambasi aliyetaka kumpindua mzee John Cheyo kwenye uenyekiti wa UDP mwaka 2003,na baadae akarudi CCM,huyu ndugu alifariki mwaka 2010 akiwa hsjafikisha hata umri wa Lowassa,ukiambiwa alifariki kwa laana ya kutaka kumpindua Bwana Mapesa utakubali?
 
Shida ni pale unapokuwa na mentality kuwa KIFO ni laana au Adhabu.

Mention any Pop, Saint , Nabii, Mtume etc etc ambae hajawahi kuwfa kwa kuwa ni mtu Mzuri,

You are such a naive na hizo story za mental slavery , Lowassa muda wake is due Kama wako utakavofika, that does not mean anything

Kama ulilkuwa hujui , Lowassa was a great man and a prophet of our time,

hata hao unaowaita marafiki zake wakubwa, ni ushamba wako …… EDO hajawahi kuwa na urafiki wa karibu na huyo mtu, they just grew up pamoja and known to each other….. that doesn’t mean friendship.

Edo was genuine man , na aki interact na wewe , he interacts with pure heart and love ….. he was such a gentleman and true soul

Hao unaowaita marafiki zake, hajawahi kuwa na urafiki nae , he knew him and helped him mentally and financially to shape his career path…… and ofcourse JK alifanikiwa sana kwa msaada wa EDO.

.wakati Edo anaomba kura ya Urais, he never asked for a favor from him , he tried for his best level , only it did not work , and remained pure man.

Alienda pia kumpongeza JPM kuonesha…. Heshima na akaomba wafuasi wake waisapoti serikali mpya ya JPM

Such a gentleman with maturity , he always wanted peace

Sio hao wengine waliojaza unafiki kwenye nyuso zao na uzandiki

The better thing is that , no one will get alive out of this world .
Kwa maelezo yako haya, inaonekana ulikuwa unamfahamu vyema, na pengine kuwa naye karibu lowasa.

Alichoeleza kikubwa Jidu La Mabambsi, ni lowasa kupora ardhi ya kanisa iliyotolewa na mzee Kileo.

Kwenye maelezo yako marefu kumhusu lowasa, hujasema lolote kuhusiana na uporaji huo kama kweli alipora au majungu tu.
 
Kuna yule mzee wa Musoma alikuwa katibu wa Nyerere aliwahi kuandika juu ya ''usafi'' wa Edo na kisa cha kwanini Nyerere alimkataa.
Mzee Kasomi. Kilichofuata ni Kasomi kuwindwa auwawe ikabidi aukimbie mji wake kuokoa maisha.

Zee fisadi liuaji lilikuwa la hovyo sana hili.
 
Hata mimi naitaka hiyo laana kama aliyopata Hayati Lowassa ili nipande ngazi hadi kufikiwa kuwa PM na chupuchupu kuwa Rais kupitia Chama Cha Mbowe (CCM B). Hiyo KKKT ambayo usipotoa michango siku ukifa unaweza zikwa na housegirl wa mlinzi wa kanisa si la kumtisha mtu.
Huu uzi ufungwe sasa
😂
 
Back
Top Bottom