Masikini UKAWA

Masikini UKAWA

Nape angalia kwenye nyayo zako kuna kitu kitakutokea ndani ya siku chache zijazo.Huo ulimi wako umekuponza.
 
Now ni bunge la dini tu hapa hamna jipya huna jipya usilete uzamani ndani ya Tz ilove
 
Niliwahi kusema nikiwa Kigoma kuwa UKAWA ni kaburi la vyama vya upinzani nchini! Sasa nimeangalia bunge asub hii na kuona hao waliokuwa wakiaminiwa kama ni UKAWA wamo bungeni. Huu ni msiba mkubwa kwa UKAWA. Sasa wamebaki Chadema,nccr na cuf tena SI WOTE!

Kimbieni msiba huu mkubwa. Cuf na nccr mnaingizwa mkenge na Chadema ambayo inaishi kwa matumaini kwasasa! Fumbueni macho!
Hongera Olouch!

Hawa wanacheza pamoja kama team kwenye maswala ya msingi.

Huu ndiyo upinzani wa kweli kwenye mambo ya msingi mnaweka itikadi za kichama pembeni.

Unashindwa kujua kitu kidogo kama hiki, umebaki kueneza propoganda.

Nafikiri unafahamu wazi kwamba simba na yanga nitimu pinzani, lakini wachezaji wake wanapokutana katika team ya taifa zile tofauti zao wanaziweka kando wanacheza kwa pamoja kwa masirahi ya taifa.

Vile vile katika hili ndivyo walivyo fanya vyama pinzani kwenye maswala ya msingi lazima tuangalie yale yaliyo ya msingi tofauti ziwekwe kando.

Unajua muungano huu unawanyima sana usingizi, lakini mwisho wa siku lazima tutaipata katiba iliyo bora kwa msingi huo huo wa ushirikiano.
 
Inasikitisha sana kuona vijana kama Nape akiwa na akili zilizokwisha muda wa matumizi.
Inasikitisha sana.
 
Thread za Nape Nnauye ni mistari mitatu au minne hembu badilika mkuu kuwa intellectual kwa ku create constructive idea
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kusema nikiwa Kigoma kuwa UKAWA ni kaburi la vyama vya upinzani nchini! Sasa nimeangalia bunge asub hii na kuona hao waliokuwa wakiaminiwa kama ni UKAWA wamo bungeni. Huu ni msiba mkubwa kwa UKAWA. Sasa wamebaki Chadema,nccr na cuf tena SI WOTE!

Kimbieni msiba huu mkubwa. Cuf na nccr mnaingizwa mkenge na Chadema ambayo inaishi kwa matumaini kwasasa! Fumbueni macho!
Hongera Olouch!
kumbuka UKAWA inaundwa na vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi. Sasa wewe usyeijua famila yako OLOUCH yupo chama gani kati ya hiyo?
 
Mtu yoyote mwenye akili timamu atakuambia serikali tatu ndio mfumo sasa..ila mtu yoyote mwenye akili timamu na anayewajua aina ya viongozi wakiopo Tanzania atakuambia serikali 2 ndio mfumo sasa kwa aina ya viongozi waliopo..
 
Hawa ukawa tushawajua sana hawana jipya tena la kutueleza wakalale nyumbani kwao huku mitaani hata wasitie mguu kabisa.

Waswahili wana msemo " ukiona adui yako anakusifia ujue wewe ni mjinga"!! Sitegemei magamba kusifia UKAWA!! Hawa magamba kama wanajiamini na hawawaogopi UKAWA, kwanini wanapiga marufuku mikutano yao??
 
- juzi nilikutana na mbunge mmoja wa chadema kwenye viwanja nikamtajia ukawa akaniomba sana na kunishi nisiseme kwa watu wasisikie maana ukawa sasa ni tatizo sana kwa wananchi, sikuamini alichokuwa anakisema kumbe na wao wameshaelewa kuwa wanayoyafanya sasa hata wananchi hawafurahii!!

Le mutuz system
u- - umoja wa
ka- - katiba ya
wa -- wachache
hii ndiyo siri iliyojificha kwenye neno ukawa.
 
Chama cha CUF ndiyo KING PIN
wa hii katiba mpya, no wonder Sitta amekwenda ZNZ kuwaangukia CUF. UKAWA
wanawahitaji CUF ili kukwamisha katiba mpya ya ki-CCM. On the other
hand CCM wanawahitaji CUF ili kupitisha katiba mpya ya ki-CCM. Hivyo
basi CUF wameshika MPINI wakati UKAWA na CCM wameshika MAKALI. Wote
(UKAWA NA CCM) wanasubiri huruma ya CUF. Kwa wale mliowahi kucheza
karata, CUF wamelamba DUME, UKAWA na CCM wamelamba MAJIKE, wanasubiri
mmoja wao aolewe na CUF.

Hay mkuu umetoka wapi? Jitazame vizuri geuka hata nyuma isijekuwa hapo upo Msalani unahara na kutapika kwa pamoja!

Unaposema "UKAWA" Unamaanisha umoja wa katiba ya wananchi ambao unaundwa na cuf,cdm na nccr jiangalie vizuri mku ulichoandika ni kituko mno.

BACK TANGANYIKA
 
u- - umoja wa
ka- - katiba ya
wa -- wachache
hii ndiyo siri iliyojificha kwenye neno ukawa.

Hongera kwa kumnukuu Amos Makala (nackia ni waziri) katika mchango wake wa leo bungeni.
 
Bila UKAWA hakuna katiba ya Wananchi. Hii ni katiba ya CCM ikishirikiana na CCM wenzao kutoka 201 kama Kingunge kutoka kundi la Waganga na Wachawi, Askofu Mtetemelwa, na Oluoch
Ongeza na Prof R. Assey na Dr Francis. Maprofesa wachumia tumbo
 
Back
Top Bottom