Masikini wana chuki na roho mbaya sana

Masikini wana chuki na roho mbaya sana

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Masikini wana roho mbaya
Na Paul R.K Mashauri

Watu wengi wanafikiri matajiri wengi "wealthy people" wana roho mbaya na makatili. Nazungumzia waliotafuta pesa kihalali sio "walioiba na kudhulumu"

Waliochuma kwa jasho. Hao matajiri wengi wana roho nzuri sana na ni wanyenyekevu sana "very humble PEOPLE " nitafafanua kwa kirefu namaanisha nini.

Na masikini wengi "ukiondoa" masikini wanaojitambua ambao kimsingi sio "masikini" waliobaki hao "wana roho mbaya sana" haujapata kusikia.

Hata matajiri wa kwenye Biblia hawakuwa na roho mbaya. Ayubu, Abraham, Yusufu, Boaz, Suleiman ndio usiseme. Yasome maisha yao. Walikuwa "Humble".

Kwanini? Ni kwa sababu hauwezi kuwa tajiri kama hauko "Humble". Huwezi ku "maintain" huo utajiri. Tatizo wengi wanachanganya nidhamu ya fedha wanaita "roho mbaya"

Kutokuwa na nidhamu ya fedha ukajiita "masikini jeuri" haimaanishi uko "humble". Mfano mzuri ni Afrika ya kusini. Wanaoua wageni ni masikini wasiojitambua.

Walishawahi kuniteka mimi wale usiombe ukutane nao. Wakikuonyesha bastola kama una hela wape hawatanii. Wanakuua! Unyenyekevu wao ni "ZERO". Sasa jiulize "South" kunawashinda "wangeletwa bongo"?

Masikini asiyejitambua hana cha kupoteza hata akifungwa maisha. Ndio maana kukuchoma kisu ni dakika moja tu! Na hata akiiba hela nyingi habadilishi kazi kwa sababu hajitambui!

Ukitaka kujua masikini asiyejitambua ana roho mbaya mpe gari lako aendeshe. Au mpe ajira usimfuatilie. Litarudi "scrapper" na biashara ana ifilisi. Ukimnyima hela anakutukana!

Lakini tajiri unayefikiri ana roho mbaya kwa sababu hakupi hela hawezi kukuchoma kisu. Ana cha kupoteza! Ana mali za kuchunga! Nazungumzia aliyepata hela kihalali

Na mtu mwenye hela ana namna nyingi za kukusaidia na kukupa hela ni namna ya mwisho kabisa kwa sababu sio suluhisho la umasikini! Kama hujitambui ukipewa hela zitakuua!

Wakati mwingine anajua hauhitaji hela kutoboa unahitaji kutuliza akili yako. Ndio sababu hata Yesu hakuwapa wanafunzi samaki ila aliwatuliza akili na kuwaonyesha upande wa kuvua.

Wakati mwingine anahitaji kukufundisha "nidhamu" ya fedha na jinsi ya kuvua samaki. Anahitaji kukufundisha jinsi ya kuishi na watu. Anahitaji upambane ili uthamini utakachokipafa!

"Mungu Akupe Hekima Ya Kuelewa Sio Kulaumu na kulaani. Mafanikio ni "SYSTEM" ni "PROCESS".Lazima uwe tayari kupita kwenye mchakato"
 
Hapa kufafanua kwa kirefu ndio mwanzo wa uongo wako Tajiri Mkuu. Jambo lonaloeleweka halihitaji maelezo meeeengi.
Waliochuma kwa jasho. Hao matajiri wengi wana roho nzuri sana na ni wanyenyekevu sana "very humble PEOPLE " nitafafanua kwa kirefu namaanisha nini.
 
Walishawahi kuniteka mimi wale usiombe ukutane nao. Wakikuonyesha bastola kama una hela wape hawatanii. Wanakuua! Unyenyekevu wao ni "ZERO". Sasa jiulize "South" kunawashinda "wangeletwa bongo"?
Hayo magenge yanayotembea na Bastola ndio Matajiri ya South Afrika ambayo wewe unayaita yana Roho nzuri na yako Humble.

Yako humble yakiwa barabarani....lakini yakiwa kazini" wizi na uporaji na dhulma" ni mashetani.
 
Umaskini upo kwenye namna ya kufikiri. Kuna jambo mtu anavyoliwaza tu na kulitamka, unaona kabisa huyu ni maskini. Bila kubadili mtazamo wake, kutoboa inakua ngumu sana.
Kabisa
Umasikini huanzia ROHONI
 
Upo sahihi utajiri unashikiliwa na hekima and (humbleness)

Pia ukiwa positive na kuthamini utu Wa MTU kuna namna utaanza kuona Nuru Katika maisha yako.

Masikini ni akili ,akili ikiwa ikigoma kufunguka unaanza kuamini waliofanikiwa wote wanaiba na wezi.

Watu tunatamani kucheza mpira kwa kiwango cha juu na kupata hela nyingi Sana Ila hatupo tyari kufanya mazoezi makali ili tuwe na kiwango bora.
 
Masikini wana roho mbaya
Na Paul R.K Mashauri

Watu wengi wanafikiri matajiri wengi "wealthy people" wana roho mbaya na makatili. Nazungumzia waliotafuta pesa kihalali sio "walioiba na kudhulumu"

Waliochuma kwa jasho. Hao matajiri wengi wana roho nzuri sana na ni wanyenyekevu sana "very humble PEOPLE " nitafafanua kwa kirefu namaanisha nini.

Na masikini wengi "ukiondoa" masikini wanaojitambua ambao kimsingi sio "masikini" waliobaki hao "wana roho mbaya sana" haujapata kusikia.

Hata matajiri wa kwenye Biblia hawakuwa na roho mbaya. Ayubu, Abraham, Yusufu, Boaz, Suleiman ndio usiseme. Yasome maisha yao. Walikuwa "Humble".

Kwanini? Ni kwa sababu hauwezi kuwa tajiri kama hauko "Humble". Huwezi ku "maintain" huo utajiri. Tatizo wengi wanachanganya nidhamu ya fedha wanaita "roho mbaya"

Kutokuwa na nidhamu ya fedha ukajiita "masikini jeuri" haimaanishi uko "humble". Mfano mzuri ni Afrika ya kusini. Wanaoua wageni ni masikini wasiojitambua.

Walishawahi kuniteka mimi wale usiombe ukutane nao. Wakikuonyesha bastola kama una hela wape hawatanii. Wanakuua! Unyenyekevu wao ni "ZERO". Sasa jiulize "South" kunawashinda "wangeletwa bongo"?

Masikini asiyejitambua hana cha kupoteza hata akifungwa maisha. Ndio maana kukuchoma kisu ni dakika moja tu! Na hata akiiba hela nyingi habadilishi kazi kwa sababu hajitambui!

Ukitaka kujua masikini asiyejitambua ana roho mbaya mpe gari lako aendeshe. Au mpe ajira usimfuatilie. Litarudi "scrapper" na biashara ana ifilisi. Ukimnyima hela anakutukana!

Lakini tajiri unayefikiri ana roho mbaya kwa sababu hakupi hela hawezi kukuchoma kisu. Ana cha kupoteza! Ana mali za kuchunga! Nazungumzia aliyepata hela kihalali

Na mtu mwenye hela ana namna nyingi za kukusaidia na kukupa hela ni namna ya mwisho kabisa kwa sababu sio suluhisho la umasikini! Kama hujitambui ukipewa hela zitakuua!

Wakati mwingine anajua hauhitaji hela kutoboa unahitaji kutuliza akili yako. Ndio sababu hata Yesu hakuwapa wanafunzi samaki ila aliwatuliza akili na kuwaonyesha upande wa kuvua.

Wakati mwingine anahitaji kukufundisha "nidhamu" ya fedha na jinsi ya kuvua samaki. Anahitaji kukufundisha jinsi ya kuishi na watu. Anahitaji upambane ili uthamini utakachokipafa!

"Mungu Akupe Hekima Ya Kuelewa Sio Kulaumu na kulaani. Mafanikio ni "SYSTEM" ni "PROCESS".Lazima uwe tayari kupita kwenye mchakato"
Ndio maana anaetumbua viongozi na kukamata wenye hela anapendwa sana.
 
Back
Top Bottom