Masikitiko: Utamaduni wa wizi na kukosa uaminifu kunazuia maendeleo yetu sana!

kwa hiyo mradi wako wa bagamoyo uliokoteza watu wa barabarani ukawakabidhi...who does that? kwa nini hukumkabidhi baba yako ausimamie?....

Binafsi nina ndugu na jamaa zangu USA wamekuwa wananiomba niwasimamie maissue yao huku nyumbani ninakataa kwa sababu wakati mwingine diaspora mnakuwa wajinga sana. Unataka nitumie muda wangu mwingi kusimamia shughuli zako bila kujali nina familia inahitaji kula, kuvaa na hata ninasomesha unategemea nini kitatokea?

Na akili zenu zilivyo za ajabu wengi wenu mnadhani maisha ya miaka ya 1990 mlipoondoka ndiyo yale yale ya leo 2022.
 
Ndugu yangu acha tu umesema kweli. Hii nchi yetu ina laana gani sijui au ni nchi za kiafrika ndivyo zilivyo. Yaani ni shida kabisa. Wengine tumepigika mpaka na ndugu zetu. Niko nje kwa muda sasa na nikanunua shamba heka kama nne hivi. Nikaona nitafute hati ya kiwanja maana nilitaka kujenga shule. Nilipewa mpima ardhi (Land Surveyor) kutoka Wizara ya ardhi nikaambiwa huyo atakusaidia. Kweli walipima wakaweka mawe. Kweli akatengeneza faili na nikasaini. Mpaka hapo nimeshatoa pesa mpaka za kuwapa wajumbe wa kikao cha mtaa. Aisee miaka zaidi ya kumi na sita sasa hamna kitu. Kufuatilia yule surveyor akaniambia pesa zinahitajika tena nikalipa na kuahidiwa ukishalipa hizi pesa hati itatoka mara moja. Imekaa nikiulizia hamna majibu. Nikamtuma mtu mwingine baki anifuatilia akanipa taarifa kwamba bila pesa hati haitoki na mimi nikasema sitoi pesa ambayo siyo halali. Nina kiwanja Dar nimefuatilia hati nimeshindwa. Anyway hiyo ndiyo nchi yetu inayotafuta investors.
Huku niliko nilinunua kiwanja ili kuepuka kupanga (hapo jua mimi siyo raia nina resident permit na working permit) yaani huwezi amini three weeks baada ya kulipia pesa zinazohitajika na ku submit application NILIPIGIWA SIMU NJOO UKACHUKE HATI YAKO YA KIWANJA. Nikafuata taratibu za nchi hii nikajenga nyumba na nikapata occupation permit bila usumbufu nikawa ninaishi kwangu.
Kuna rafiki yangu tupo naye hapa, Alikuwa na kiwanja chake kikubwa tu dar akamweka mtu amwangalizie na kuweka mifugo. Alikuta jamaa keshakimega na kuuza na ameshakiandikisha kwa jina lake, Imechukua miaka kama kumi hivi akisumbuka mahakamani na haki haipatikani
Haya ni baadhi tu kuna diaspora wengi wanalia. Wanapenda ku invest home lakini mazingira siyo mazuri kabisa. Sasa kama sisi tumeshindwa je mnaposema mnatafuta wawekezaji kwa hali hii itakuwa ngumu sana sana.

Ninashauri tu watanzania wenzagu tuache hii mentality ya rushwa inatesa sana.
Kuishi kwa kutumia rushwa hakutasaidia sana maana tunaweka kizazi kijacho mahali papaya sana. Wengi watabakia maskini na litakuwa janga la taifa.

Kabla sijaenda nje kwenye miaka ya 90 hivi nilikuwa ninafanya kazi kwenye wizara fulani hivi. Kuna nchi moja ilitoa scholarships kwa ajili ya kusomesha watu katika ile wizara. Katibu akapewa ili a select vijana badala ya kuwapa watu wa chini kama DAP for implementation yeye akaificha. Yule Katibu alikuja kuondolewa pale sasa yule mwingine alipokuja akakuta zile scholarships na muda wake ulikuwa umekwisha. Alisikitika sana, hivyo ndivyo tunavyoiangusha nchi yetu wenyewe.

Anyway tumefika mahali pagumu na sijui nani atatutoa hapo lakini mwananchi wa kawaida anaumia sana maada kupata huduma ni kazi sana.
Nilipokuwa ninaangaika hapa na pale mtu mmoja akasema " inabidi Mnngu akiondoe kizazi hiki na alete kizazi kingine" . Alikuwa amekata tamaa kwa yale aliyokuwa anapitia pia na yeye. Lakini ninafikiri hatujafikia huko watatnzania bado tunaweza kubadilika tukipata uongozi mkali kama walivyo fanya wenzetu Wachina hapo siku za nyuma.
 
Wa-TZ sio wote ni wabaya, tupo tulio waaminifu.

Ukiwatumia hao, mambo yako yataenda vizuri.

Diaspora; msikate tamaa, leteni pesa na mitaji yenu muwekeze huku nyumbani. Waaminifu tupo.
 
Yote uliyoongea ni kweli kabisa na hakika mi nimepeleka fundi site afanye tathmini ya umeme Kila kifaa kkaweka ten percent ya hatari kisa nilimwambia nachukua dukani kwake dah hadi nikachoka maana kama kazidisha hivyo gharama uhakika kuwa hataiba nautoa wapi!?
 
Wa-TZ sio wote ni wabaya, tupo tulio waaminifu.

Ukiwatumia hao, mambo yako yataenda vizuri.

Diaspora; msikate tamaa, leteni pesa na mitaji yenu muwekeze huku nyumbani. Waaminifu tupo.
Nakazia hapa, samaki wengine hatujaoza wakuu msisite kuja kutuona bado tu waminifu
 
Bora wewe umewajua watz mapema. Kuna jamaa alikaa botswana miaka akijima akituma pesa ajengewe nyumba na ndugu yake aliishia kuonyeshwa picha za nyumba nyingine hela anafanyia starehe karudi bongo hata kiwanja Hakuna.
Ushauri wangu kama upo mkoani au nje ya nchi ni salama zaidi kama unatunza pesa zako ikifika likizo njoo mwenyewe mwezi mmoja unatosha kumaliza nyumba au kama huna mda ni bora uje ununue mwenyewe nyumba Ili zije zikufae uzeeni. Usimwamini ndugu au jamaa yasije kukuta.
1.Utajengewa KWA gharama kubwa zaidi hata mara tatu.
2.utajengewa chini ya kiwango
3.Utaonyeshwa picha za jengo hewa
 
Usinunuwe shamba kama hujawa tayari kulima na uko mbali nalo. Ni tabia yetu maarufu Watanzania kurudia kuuza tulivyokwisha vipokelea pesa. Hata serikali za vijiji wanashiriki uovu huu.
Tumejenga utamaduni wa kuto heshimu mali za wengine. Bahati mbaya vyombo vya kusimamia sheria havisimamii haki. Muhimu kwao mabishano ya vifungu vya sheria. Kupata haki mahakamani ni matokeo ya bahati tu.
 
Kwa hiyo ulianzisha dhehebu lako ili upige pesa za wajinga. Una tofauti gani na hao waajiriwa mafisadi?
Kuna mahali umeona nimeandika kuwa nilianzisha dhehebu au ndiyo unaonyesha uhalisia wa tatizo kubwa la afya ya akili kwa Watanzania wengi!!???
 
Mishahara haitoshi ndio sababu kubwa.
Thus watanzania wengi wanajiongeza kwa kuweka cha juu
Kwa wengine inaweza kuwa hivyo lakini na kwa wale wenye mishahara minono na bado wanataka 10% Unasemaje hapo. ?? Mtu mwenye tamaa huyo ni lazima atake cha juu hata kama ana ukwasi wa kutisha !! Na ndilo tatizo kuu la Inji hii !!
 
Pole sana kiongozi!
Nimesikitika sana kuona uliomba quotation ya kupitisha vifaa tiba bandarini ukaambiwa havilipiwi ila ulipo leta ukaambiwa 15M??? hii haijakaa sawa....
Natamani Ushuru uwe wazi watu waweze kuona online kwani itaepusha rushwa au kukomoana kwa wasiokuwa na nia njema
 
Wapiga dili hizo za haramu huku mitaani wanaitwa wajanja !
 
Mkuu naungana na wewe kwa 100%
Hili la watu kutokua waaminifu ni tatizo kubwa sana,tena akiona wewe upo nje ndio anakupiga hasa,utafikiri ukiwa abroad hela hua ni za kuokota tu Barabarani,inasikitisha sana.
 


Nakubaliana na wewe. Tatizo kubwa hasa kwa sisi tunaojaribu kuleta vitu hata kama unataka kuomba msaada huwezi kubadilika kila mara mfano ningejua hata jamaa walioniuzia wangeweza kunipa pesa kama msaada na baadae kutoa kwenye kodi zao kama charity lakini nataka documents kabla ya kutuma mzigo. Yaani tuna systems ambazo zinanufaisha wezi na wala rushwa na sio wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…