Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Afu kuolewa sio basic need bhana khaaaaaa
 
Shida ilianza na kuyapa maisha standards as if ni aina fulani ya movie ambayo utalipwa kuigiza.

Nini kimebadilika kwa vijana na mabinti kuanza Maisha pamoja wakiwa hawana hata stuli?

Mbona mabinti wanakaa kigeto geto na wenzao tena wanalala sakafuni ila atagoma kuanza maisha na kijana ambaye anaishi chumba kimoja kwa kumuona ni masikini mwenye nuksi?

Atakataa kula chakula kizuri kama wali maharage na kulazimisha kutolewa out kula chakula cha 30,000 kila weekend ila akiwa magetoni na wenzake wanakula ugali na dagaa wa mchuzi waliochanganywa na ngogwe na bamia.

Atakwenda kuhangaika mjini huko plus kudanga ili anachopata alipie bills tena kwa kuchanga 50/50 na wenzake kwenye kila kitu ila ataleta dharau na ubinafsi kwa kijana ambaye amejitoa kulipia 100% ya bills zote za kwenye nyumba bila kulalamika wala kumtaka na yeye atoe kitu.

Kwa kifupi, mabinti hapa lazima mlaumiwe zaidi. Ni ninyi ambao mnachelewesha mahusiano serious kuanza sababu ya kuendekeza tamaa zenu za kitoto na kuforce maisha ya juu kwa vijana wanaojiokota na hali zao ngumu.
 
Kweli mkuu umeandika kwa busara sana. Mimi ni mhanga wa hizo kauli ila bahati nzuri na mimi huwa najibu mapigo kikatili sana kuwapunguza spidi. Imefikia point wananiambia kama hutaki kuoa tafuta mtoto... wasichokijua ni kuwa ningekuwa na mtoto wa miaka 8 ila bahati mbaya alipozaliwa hakukaa alifariki. Baada ya hapo nilijiapiza kuwa makini kutozaa nje ya ndoa kutokana na maudhi niliyokuwa napata kutoka kwa binti niliyekuwa nimempa mimba pamoja na mama yake mzazi. Nimesimulia hii stori fupi kuonyesha sio kwamba mtu hataki kuoa au kuwa na watoto bali kuna mambo hayajakaa sawa.
 
Mtu asipooa au asipoolewa hafanyi kosa lolote kimaadili. Hilo si kosa la kimaadili wala la kisheria.

Sio dhambi kutokuoa au kutoolewa.

Lililo kosa la kimaadili au kosa dhidi ya akili yaani dhambi ni: KUVUNJIKA KWA NDOA au TALAKA, UZINZI NA UASHERATI; PONOGORAFIA, MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE. Haya ndio mambo watu tunatakiwa tutafakari, tuyachunguze, tufuatilie; tujue yanasabishwa na nini, na kwa nini; halafu tuamue.

Hebu fikiria ni ndoa ngapi zinavunjika? Jiulize: ni ngapi? Jiulize; ni mateso kiasi gani watoto wanapata na kupitia kiakili na kimwili kwa wazazi kutalakiani? Ni wangapi wanateseka kwa makosa haya ya wazazi kutalakiana, magonvi, au kutengana? Madhara yake ni nini? Jiulize!!

Kwa kufanya uzinzi na uasherati, ni wanawake wangapi wamezalishwa na kutelekezwa? Wanawake wangapi wamepigwa mimba na kutelekezwa? Wangapi? Hao watoto wanatunzwa na nani? Haya sio mateso? Huu sio uuaji? Na hivi ndivyo mambo au mpango unapaswa kuwa? Hili ndilo lengo?

Huyo Mungu ambae waafrika mnapenda kumrejelea na kuficha udhaifu au ukatili au ubaya au mapungufu yenu, kwa kukosa kwenu uelewa wa mambo na elimu ya vitu, hakuna mahali amesema watu lazima waoe na kuolewa au wazaee. Hakuna!

Mwenye huu uthibitisho alete hapa.

Watanzania ni watu ambao hawatumii akili kabisa, ukiacha hekima na busara. Wanafungisha ndoa huko wanakoita makanisani na misikitini, lakini hawasimamii hizo ndoa walizozifungisha. Watu wanatalakiana, wanaachana kila siku. Kila uchao ni ugomvi, mafarakano kwenye hizo ndoa.

Wasivyo na akili, hekima, na busara, wameshindwa kushughulikia matatizo ya ndoa, sasa wanataka kuwabagua watu wasio na kosa kimaadili, yaani wale wasiooa na wasioolewa.

Huu ni wendawazimu mkubwa.

Ndugu zangu watanzania acheni kushikilia mambo na kudhani kwamba haya ni mambo yetu; na yale ni mambo yao.

Tupende kufikiri, kuchunguza, kufuatilia na kisha kuamua. Tuache kuchukua mambo kama yalivyo bila kujua yalianza vipi, wapi na kwanini.

Hivi kweli suala la mtu kutokuoa au kutoolewa nalo ni jambo zito linalohangaisha jamii au familia, kwamba mtoto wangu hajaoa au hajaolewa?

Mtu asieoa au asieolewa ana kosa nini kimaadili au kiakili; au hata kimwili?
 
Vijana wengi hatutaki kuoa bila hoja yoyote , hoja zinazojengwa zote ni sababu ya kukwepa majukumu sasa mwanaume kama unakwepa majukumu maana yake hujakamilika kujiita mwanaume
Hii ndio ukweli wa mambo watu wanaogopa majukumu wanajitetea. Kazi ya jamii ni kusimamia maadili kwa hiyo lazima uulizwe tuu ukitaka usitake utaulizwa.
 
Nyie mndio mnaoendekeza utamaduni wa kunyanyapaa watu wasiooa.

Yani uneshakariri. Kuoa = Heshima.

Wakati kuna walevi mbwa kibao wameoa na wanapiga wake zao kila siku na kufanya mambo ya kujivunjia heshima.

Halafu kuna watu poa tu hawajaoa.
Hao walevi wachache hawaondoi uhalali kuoa ni heshima na ni maadili kwenye jamii. Vijana wengi tunaogopa majukumu na kumbuka hutakuwa kijana maisha yako yote tunajidanganya kwa muda tuu
 
Acha kuiga maisha ya kimagharibi Mungu amesema tuzaliane tujaze dunia na ni muhimu watoto wazaliwe kwenye ndoa ili kutunza maadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…