Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Masimango na kejeli kwa wanaoonekana wamechelewa kuoa/ kuolewa na kupata watoto uzeeni au umri ukiwa umekwenda

Ndiyo hakuna asiependa heshima
Nyie mndio mnaoendekeza utamaduni wa kunyanyapaa watu wasiooa.

Yani uneshakariri. Kuoa = Heshima.

Wakati kuna walevi mbwa kibao wameoa na wanapiga wake zao kila siku na kufanya mambo ya kujivunjia heshima.

Halafu kuna watu poa tu hawajaoa.
 
Nyie mndio mnaoendekeza utamaduni wa kunyanyapaa watu wasiooa.

Yani uneshakariri. Kuoa = Heshima.

Wakati kuna walevi mbwa kibao wameoa na wanapiga wake zao kila siku na kufanya mambo ya kujivunjia heshima.

Halafu kuna watu poa tu hawajaoa.
Kuoa ni heshima full stop

Kuona kwako walevi wameoa haimaanishi kuoa siyo kitu cha maana na heshima.
 
Hapana, unalazimisha majibu rahisi kwa maswali magumu kama kawaida yenu wabongo wengi.

Yani unaishi maisha ya kukariri kariri, kuishi kwa formula rahisi rahisi. Kulazimisha lazimisha "Full Stop".

Kama kuoa ni heshima wanaooa wasingekuwa na scandal za ku cheat nyingi hivi.
Na wewe usilete mambo yako ya kulazimisha kuwa kuoa siyo kitu cha heshima
 
Ukikosa mtoto nenda vituo vya watoto yatima chukua mmoja au wawili watunze waite kwa majina yako,

kuhusu kuoa sio jambo la lazima ndomaana hata Kwenye hizo Dini zenu mnaambiwa huko mbinguni hakuna mambo za mke na mume.
Ukose mtoto kwa sababu za kiafya ila siyo kwa sababu za utoto na uzembe wako.

Utakuwa kichaa uwe na uwezo wa kuzaa halafu umeacha kuzaa wako ukaenda kutafuta watoto wa watu wa wengine ukawaita kwa jina lako.
 
Ukose mtoto kwa sababu za kiafya ila siyo kwa sababu za utoto na uzembe wako.

Utakuwa kichaa uwe na uwezo wa kuzaa halafu umeacha kuzaa wako ukaenda kutafuta watoto wa watu wa wengine ukawaita kwa jina lako.

Sio ukichaa ni maamuzi tu, Muda mwingne Unaweza kufanya kitu ukaonekan kichaa ila matokeo ndo yatatenganisha vichaa na walio timamu.
 
Na wewe usilete mambo yako ya kulazimisha kuwa kuoa siyo kitu cha heshima
Kwani wapi nimesema kuoa si kitu cha heshima?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Kwanini unaweka false dichotomy kwamba kuoa lazima ni kitu cha heshima au si kitu cha heshima? Kwa nini unaona mtu akisema kuoa si lazima kiwe kitu cha heshima, basi amemaanisha kuwa kuoa ni lazima kiwe ni kitu kisicho cha heshima?

Do you not see this as a false dichotomy logical fallacy?
 
Habari za muda huu marafiki,

Siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya kushangaza kustaajabisha kwenye jamii yetu na hasa huku mitandaoni.

Kumekuwa na wimbi la watu kuwasimanga, kuwakejeli na hata kuwacheka ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wanaoonekana kwa vigezo, mitazamo na viwango vilivyowekwa kwenye jamii kuwa wamechelewa kuoa au kuolewa hivyo kuonekana wamepata watoto wa uzeeni.

Ni jambo linaloonekana kama la kawaida lakini kwa upande mwingine linasononesha na kuvunja mioyo ya watu walioamua kujenga familia.

Ni kauli za kitoto zinazoonyesha kuwa bado hawajakomaa kiakili kwenye ulimwengu huu uliojaa harakati na purukushani za kila aina.

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwakumbusha hao wenye kuwakejeli wengine kwenye hili ya kuwa.

1) Maisha ni fumbo zito Sana ambalo mara nyingi ni wachache Sana wenye kufumbua. Mara nyingi mipango yako inaweza ikapishana na mipango ya Mungu.

2) Uhai na kifo ni vyake Mungu mwenyewe kwani hakuna ajuaye kuwa amebakisha muda gani wa kuishi hapa duniani. Wapo vijana wengi wametangulia mbele za haki wakiacha watoto wao na familia zao zikiteseka na kuwaacha wazee wakiendelea kulea watoto wao wa uzeeni mpaka wakijitegemea na kufurahia matunda yao. Hivyo kusema kuwa mwanaao akifika miaka kadhaa wewe utakuwa umeshachoka au umeshakufa ni maneno ya kufuru au ya mtu asiye na Imani kwa mola wake mlezi.

3) Kwenye maisha kila mtu Mungu amemuwekea wakati wake wa kufanya jambo lake kwa rehema zake. Wapo watu waliowahi kuoa lakini Mungu akawanyima watoto mpaka wanazeeka na wengine wanawapata uzeeni kabisa. Wapo watu wamejikuta wapo jela wakitumikia vifungo virefu na mpaka wanatoka umri umekwenda na wanaamua kujenga familia. Wapo watu walikuwa wanaugua kwa muda mrefu na hatimaye wakapona na kuanzisha familia. Hivyo basi kama wewe umewahi ni sahihi kwako lakini haiwezi kuwa makosa kwa anayeonekana amechelewa.

4) Changamoto za kifamilia na vifo.
Kuna mwingine anawahi kuoa lakini Kati Kati ya safari anawapoteza mke na watoto wote kwa pamoja Kwa ajali au maladhi ya kawaida na anaamua kuoa na kuanzisha familia upyaaa.

Kwa kifupi mambo na changamoto za kidunia ni nyingi zinazopelekea watu kuonekana wamechelewa kupata watoto au kuoa na kuolewa. Tujifunze kuwa wastaarabu kwenye maisha ya watu kwani hatujui matamshi yetu yanawaathiri vipi wenzetu.

Niko tayari kusahihishwa.

Nawasilisha.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom