Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

Mtandaoni wa Tizneez ametoa exclusive ya kwanini Msanii Ruby hakuonekana Mwanza wala kupanda katika jukwaa la Fiesta wakati alikuwa mmoja wa wasanii waliosajiliwa... Hivi Ndivyo mtandao huo ulivyoandika

Exclusive Ruby Amezungumza mengi ila kati ya machache ni "Maslahi yamenifanya nisiende kwenye Fiesta, Kisa ni Clouds ndio nisiwe free na kuongea, end of the day it's not about clouds it's about my future.Katika shindano la super diva ilikuwa super diva mshindi atafanya Fiesta, wakati umefika lakini ntafanya Fiesta for nothing?

Mimi sitaki kuongelea price ambayo naipata sababu nahisi nikiongea sijui watu watajiskiaje ukubwa wa show ulivyo. ...Tunakuwa na menejiment ambazo zinaendesha wasanii kimabavu, unadhani kwanini @jidejaydee wanamuita komando??
alisema hayo rubby
nini maoni yako?
ata mikataba wanasainishwa kijanja kijanja mbele ya media ili wasikatae hawa wasanii waungane watete masilay yao mwisho ndo yale jina kubwa pesa hauna
 
Nashangaa watu wanaomponda ruby.
Yani kwakua ni clouds bas akubali ujinga wote anaoambiwa eti kwakua ni clouds!!?je kama clouds na wao wamekiuka masharti!?nani anaejua !?je kama mkataba alosign mbele ya kamela na ule wa utendaji kazi ni tofauti!?
Wewe kama unaona ruby anajipoteza, kaa kimya wewe ulienyooka una nini bhana, and by the way kuimba ni kipaji iwepo clouds wawepo sijui kunguru gani ruby atabaki kuwa ruby na sauti yake tu..
Yani mtu ulipwe laki tatu eti kisa ni clouds kuna njia kibao sikuhizi za kutengeneza pesa...
Kama ulipandikizwa mbengu ya kiajiliwa lazima utamdiss ruby ila kama una mawazo huru utamuona shujaaa.
Na kwa taarifa yenu Siku ya fiesta hapa dar kutakua na Bonge la surprise kutoka kwa E FM mjini utatikisika.
Go gal babe ruby..
 
Kabla ya kusigna mkataba hakuambiwa bei atayolipwa? Kwanini alisaini? Sisapoti unyonyaji ila thamani ya Ruby haiwezi kuwa sawa na Jide au weusi au msanii mwingine mkubwa na mkongwe. Ruby anahitaji kuuza jina lake fiesta ili aongeze fanbase yake. Ruby anaihitaji fiesta zaidi kuliko fiesta inavyomuhitaji Ruby

Si ndiyo huyu huyu aliyepanic baada ya Ali Kiba kumuita mbwa wake Ruby, na ni huyu aliyegoma kutokea kwenye video ya yamoto band dakika za mwisho. Pamoja na yote huyu Ruby nae inaonekana ana matatizo sana
 
Mtandaoni wa Tizneez ametoa exclusive ya kwanini Msanii Ruby hakuonekana Mwanza wala kupanda katika jukwaa la Fiesta wakati alikuwa mmoja wa wasanii waliosajiliwa...

Hivi Ndivyo mtandao huo ulivyoandika;
========

Exclusive Ruby Amezungumza mengi ila kati ya machache ni "Maslahi yamenifanya nisiende kwenye Fiesta, Kisa ni Clouds ndio nisiwe free na kuongea, end of the day it's not about clouds it's about my future.Katika shindano la super diva ilikuwa super diva mshindi atafanya Fiesta, wakati umefika lakini ntafanya Fiesta for nothing?

Mimi sitaki kuongelea price ambayo naipata sababu nahisi nikiongea sijui watu watajiskiaje ukubwa wa show ulivyo. ...Tunakuwa na menejiment ambazo zinaendesha wasanii kimabavu, unadhani kwanini @jidejaydee wanamuita komando?? alisema hayo rubby

Nini maoni yako?
Right decision at a wrong timing

Kitu cha kwanza Ruby angekifanya ni kutokukubali kusaini mkataba, sasa amesaini halafu anakataa kutokea kwenye show.

Kitu kingine Ruby hajawa msanii mkubwa kama Lady Jay Dee, ilibidi avumilie ili ajipambanue ndipo aje kufanya maamuzi kama hayo akiwa tayari msanii mkubwa.
 
Nashangaa watu wanaomponda ruby.
Yani kwakua ni clouds bas akubali ujinga wote anaoambiwa eti kwakua ni clouds!!?je kama clouds na wao wamekiuka masharti!?nani anaejua !?je kama mkataba alosign mbele ya kamela na ule wa utendaji kazi ni tofauti!?
Wewe kama unaona ruby anajipoteza, kaa kimya wewe ulienyooka una nini bhana, and by the way kuimba ni kipaji iwepo clouds wawepo sijui kunguru gani ruby atabaki kuwa ruby na sauti yake tu..
Yani mtu ulipwe laki tatu eti kisa ni clouds kuna njia kibao sikuhizi za kutengeneza pesa...
Kama ulipandikizwa mbengu ya kiajiliwa lazima utamdiss ruby ila kama una mawazo huru utamuona shujaaa.
Na kwa taarifa yenu Siku ya fiesta hapa dar kutakua na Bonge la surprise kutoka kwa E FM mjini utatikisika.
Go gal babe ruby..
Kwahiyo hadi anaanza ku-post mapicha Instagram akichelekea Fiesta bado tu alikuwa hajagundua kwamba mkataba ni wa Kimangungo?

Ruby1.png

Ruby2.png

Au unataka kusema na wakati anaandika yote hayo tena with excitement bado alikuwa amesimamiwa na media? Au unataka kusema wakati ana-saini mkataba alikuwa hajausoma hata kwa kuuperuzi?! Na hata wakati anaandika yote hayo alikuwa hajasoma? Kama ndiyo; sasa hilo ni tatizo la Clouds au la kwake yeye mwenyewe?!

Wakati wewe unawakejeli wanaomponda Ruby ni wale waliopandikizwa mbegu za maisha ni hadi kuajiriwa; nawe pia na wenzako ni wale wasiofahamu nini maana ya mikataba! Kutosoma mkataba ni ujinga kama sio upu'mbavu wa aliyepewa mkataba na sio aliyetoa mkataba! Na kutosoma mkataba haiwezi kuwa excuse hata siku moja zaidi ya ku-reveal ujinga wa muhusika!

By the way, sasa suala la EFM linaingia vipi kwenye mjadala wa Clouds na EFM?! Waambieni EFM wafanye kazi badala ya kutaka kushindana na Clouds; ni ujinga uliopitiliza! EFM ni EFM na Clouds itaendelea kubaki kuwa Clouds! Acheni kuleta mambo ya Bongo Flavor... mada ya Diamond unakuta mtu bila sababu za msingi analeta habari za Ali Kiba and vice versa!
 
Hizo zote ni speculations tu wewe ulimuona akisign huo mkataba!!?au huo mkataba uliuona!?au ndo kusikia tu redion clouds wakifanya promo!?
Utake usitake ukiitaja clouds lazima tuitaje Efm likija swala la entertainment, kibongobongo kunawasanii kibao hiyo clouds hawajui hata ikowapi lakini wametoboa, hao kina shoro mwamba na kina manfongo unaowaona clouds wanawashobokea leo walitoboa bila hata support ya hiyo clouds yenu.
Ruby sio Nyumba kama hao Nyumba wengine...
 
Hiyo mikataba haina tofauti na form za kujaza unapofungua account bank..
Hakuna majadiliano....
Wewe ni kujaza tu na Kusign basi
Hiyo inaitwa Mikataba ya upande mmoja...
 
Hebu hii kazi ya kutabiri kitachofuata kwa Ruby tumuachie jamaa mmoja anaitwa MUDA,huyo msela huwa haongopi.Sasa kama kilichopo ndicho na Clouds wakampotezea basi huyo jamaa atatupa mrejesho.
 
Huyu Rubi ukomandoo anaujua lkn asije baadaye tena akatuita ukumbi wa maelezo kutuomba msamaha mara kamsingizia shetani.Mara ushauri alipewa mbaya.
 
Kabla ya kusigna mkataba hakuambiwa bei atayolipwa? Kwanini alisaini? Sisapoti unyonyaji ila thamani ya Ruby haiwezi kuwa sawa na Jide au weusi au msanii mwingine mkubwa na mkongwe. Ruby anahitaji kuuza jina lake fiesta ili aongeze fanbase yake. Ruby anaihitaji fiesta zaidi kuliko fiesta inavyomuhitaji Ruby

Si ndiyo huyu huyu aliyepanic baada ya Ali Kiba kumuita mbwa wake Ruby, na ni huyu aliyegoma kutokea kwenye video ya yamoto band dakika za mwisho. Pamoja na yote huyu Ruby nae inaonekana ana matatizo sana
Su nitamwambia babae nitamwambia babaee[emoji23] [emoji23] [emoji23] naskia hakutokea coz dogo aslay alimchomolea
 
Back
Top Bottom