Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

Maslahi madogo Clouds yamtoa Ruby Fiesta

Kwa hiyo Ruby ndo anajua maslahi kuliko Joh Makini au Fid Q?

Au yeye pekee ndiye angelipwa kidogo kuliko wengine?

Hilo buzi linalompa jeuri likimtema ataenda kuomba msamaha tu.

Kibongo kufanya kazi na Clouds ni maslahi tosha hata kama ni bure,Kuna vijana wanavipaji unique lakini wanaishia kuwaimbia wenza wao maghettoni kisa hakuna promo.

Jide mwenyewe akipata nafasi ya pili kukutana na Clouds kwa mara ya kwanza hawezi kushupaza shingo.

Huu mgogoro umemuathiri sema ndiyo hivyo tena.
Umeongea ukweli mkuu, wote hao sio wajinga wanajua kula na kipofu na tayari washatengeneza Uzi wa mashabiki ili siku wakisimama wenyewe wasitetereke sasa huyu ruby baada ya kutoa vinyimbo viwili kashajiona untouchable hahaaaa[emoji23] [emoji23] yetu macho
 
Hii habari kama ni kweli,basi kuna mambo 2 nayaona.Iwapo Ruby anajua nini alichokifanya na kashajiandaa nacho kimkakati pamoja na kisaikolojia basi atafanikiwa dhamira yake,lakini kama anafanya kwa kujifananisha na sijui Jide hapo kafeli tena kafeli ile ya kuchorwa na masikio kabisa.Ruby bado hajawa na ubavu wa kutunishiana na Clouds si kwa maana ni poa wanavyofanya Clouds ila wewe kama msanii mchanga lichukulie jukwaa la Fiesta kwaajili ya kujitangaza.Hawa wote wanaomsifia Ruby hawapo kwenye tasnia muziki wa kibongo wakaona changamoto zake,kwa sasa wasanii ni wengi na wote wanataka kutoka na ili watoke ni lazima kwanza wakubali kuliwa,kuibiwa, kutumika visivyo ili wewe ufikie lengo lako.Ruby kama uli beep tafadhari nenda kawaombe msamaha kabla ya mambo kuwa mabaya muda wa wewe kufanya hivi bado kabisa,labda kama umeamua kuacha muziki sawa ila kama muziki ndio unataka yawe maisha yako basi fanya hima ukaombe msamaha.
 
Vipi mbona umepanic sana... Siasa za fiesta zisikie mtaani tu wewe kama unawapenda clouds ni shabiki yao nenda kawasapoti upate burudani.. Ila siasa zao ni ngumu aliyezifaulu ni AY, Jide na Diamond Platinumz wengine wamezishindwa ata Ruby atashindwa maana ata mbishi Sugu aliuza timu dakika za majeruhi.. Usipoteze nguvu zako bure hapa.
Bahati hao wote uliowataja mafanikio yao yanaonekana, kwahiyo na huyo Ruby unamlinganisha na kundi hilo
 
Katika watu walioamua kumharibia Ruby ni hawa walio mshauri kukataa hiyo show halafu haitoshi kwenda kwenye social media kujidai ana tunisha misuli.

Ruby alitakiwa kupiga hiyo show halafu ange malizana nao na bila shaka kuna sababu walizo ziona Ruby alitakiwa alipwe hiyo Laki tano.

Mbona kuna wasanii hawajapata show kabisa? Halafu Ruby alitakiwa kupiga hiyo show kama shukrani kwao tuu kwa kumsaidia kumtoa maana nasikia mwaka jana ilibdi azunguke fiesta zote bure maana ndio zawadi aliyo ahidiwa ikiwa kama kumtangaza..

Ruby hajafikia level ya kuonekana ana nyanyaswa au kunyonywa kabisa Ruby ni msanii mchanga na biashara za wasanii wachanga ndivyo zilivyo..

Kama kuna mtu anataka kufananisha misuli ya Jaydee na Ruby basi kichwani hayuko sawa.. Kama kuna mtu anataka kufananisha stuation hii ya Ruby na ya Jaydee basi anapaswa kupimwa akili.

Kwanza Ruby hajatumiwa kwa vyovyote vile na Clouds kutengeneza faida yeyote ile kwa hiyo kwa vyovyote vile Ruby hatakuwa na hoja.. Maana bila shaka Clouds wana hoja za kutaka kumlipa laki tano.

Halafu kama alikuwa hakubali hiyo offer ange kataa halafu akapiga kimya au ange angalia faida ya kukubali hiyo offer ukiacha pesa... Si kila kitu lazima kikulipe papo hapo hata Jide hizo za bure alizipiga sana? Ruby ana muda gani kwenye muziki?

Tanzania tuna media house zenye nguvu tatu tuu kwa sasa.. CLOUDS , IPP NA EFM .
Msanii akigombana na moja kati ya hizo nguvu yake hupungua.. Kinyume awe na jeuri, nguvu, kiburi, katili kama Lady Jaydee..

Unajua wengi wakiona Lady Jaydee kaweza wanadhani ni rahisi.. Hahahaha.. Huyu Jaydee huwa namuangalia mara mbili si mmalizi hakika sijawai ona mwanamke wa namna hiyo sidhani kama Ruby ataweza.

Halafu ukiaacha swala la Clouds ni wazi Ruby ana shida kidogo nadhani kuna maswala yake hayako sawa.. Sidhani kama saikolojia yake kama iko sawa.... Maana hivi karibuni amekuwa akilalamikiwa sana na watu kuwa amekuwa hatokei kwenye shooting na mambo mengine..
Mkuu umemaliza wasipokuelewa wakapimwe akili[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Kwel bhn mwisho wa siku unaagalia unachoenda kufanya na malipo...co ufanye et kisa clouds mara oooh ndo waliokutoa
Wanawake sisi ndo huwa tunaharibiana wenyewe , ngoja muone huyo ruby Kama hajaenda kupiga magoti kwa luge
 
Uongo mtupu ruby ana jeuri au kukataa kitu chochote kinaandaliwa na clouds aidha kinahusu malipo au kisichohusu malipo
 
Pamoja cloudsfm nawakubali sana na FIESTA ni platform moja nzuri ya kumtambulisha msanii kwa mashabiki wake na wapya. Ila clouds itabidi wabadilike hasa kwa wasanii wanao wasimamia, we mtu kama barnaba anauwezo kuliko kiba, mondi na ommy dimpoz na kimziki wote kawatangulia na anahit kibao lkn mziki bado haujabadilisha maisha yake upande wa uchumi. Barnaba haitaji bendi wala dj ni yy na gita lake tu na bado anakufanyia shoo kali, lkn mpogoro huyu wa kigogo luhanga bado anamafanikio ya kawaida.
 
Wanawake sisi ndo huwa tunaharibiana wenyewe , ngoja muone huyo ruby Kama hajaenda kupiga magoti kwa luge
Ruby ni mtoto wa kike anayejitambua ww ni mmoja wa wanawake walio kula kiapo ktk dini ya "Mwanamke akiwezeshwa anaweza"
 
Rubi anatakiwa afahamu duniani hakuna haki haki ipo mbinguni... Achukue hicho kidogo kilichopatikana.
 
Me nahisi hiyo ni kiki tu huenda akawa moja ya surprise fiesta ikienda Dodoma au mayb Mbeya....kama Kiba alivyokua surprise kwa watu wa Mwanza....
NB; Clouds walisema kila mkoa utakua na surprise yake!!!!
 
Back
Top Bottom