Katika watu walioamua kumharibia Ruby ni hawa walio mshauri kukataa hiyo show halafu haitoshi kwenda kwenye social media kujidai ana tunisha misuli.
Ruby alitakiwa kupiga hiyo show halafu ange malizana nao na bila shaka kuna sababu walizo ziona Ruby alitakiwa alipwe hiyo Laki tano.
Mbona kuna wasanii hawajapata show kabisa? Halafu Ruby alitakiwa kupiga hiyo show kama shukrani kwao tuu kwa kumsaidia kumtoa maana nasikia mwaka jana ilibdi azunguke fiesta zote bure maana ndio zawadi aliyo ahidiwa ikiwa kama kumtangaza..
Ruby hajafikia level ya kuonekana ana nyanyaswa au kunyonywa kabisa Ruby ni msanii mchanga na biashara za wasanii wachanga ndivyo zilivyo..
Kama kuna mtu anataka kufananisha misuli ya Jaydee na Ruby basi kichwani hayuko sawa.. Kama kuna mtu anataka kufananisha stuation hii ya Ruby na ya Jaydee basi anapaswa kupimwa akili.
Kwanza Ruby hajatumiwa kwa vyovyote vile na Clouds kutengeneza faida yeyote ile kwa hiyo kwa vyovyote vile Ruby hatakuwa na hoja.. Maana bila shaka Clouds wana hoja za kutaka kumlipa laki tano.
Halafu kama alikuwa hakubali hiyo offer ange kataa halafu akapiga kimya au ange angalia faida ya kukubali hiyo offer ukiacha pesa... Si kila kitu lazima kikulipe papo hapo hata Jide hizo za bure alizipiga sana? Ruby ana muda gani kwenye muziki?
Tanzania tuna media house zenye nguvu tatu tuu kwa sasa.. CLOUDS , IPP NA EFM .
Msanii akigombana na moja kati ya hizo nguvu yake hupungua.. Kinyume awe na jeuri, nguvu, kiburi, katili kama Lady Jaydee..
Unajua wengi wakiona Lady Jaydee kaweza wanadhani ni rahisi.. Hahahaha.. Huyu Jaydee huwa namuangalia mara mbili si mmalizi hakika sijawai ona mwanamke wa namna hiyo sidhani kama Ruby ataweza.
Halafu ukiaacha swala la Clouds ni wazi Ruby ana shida kidogo nadhani kuna maswala yake hayako sawa.. Sidhani kama saikolojia yake kama iko sawa.... Maana hivi karibuni amekuwa akilalamikiwa sana na watu kuwa amekuwa hatokei kwenye shooting na mambo mengine..