Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

Binafsi naungana na wewe, sioni maana ya kusoma democracy, government, multiparty, kinjekitile nk na kuacha kusoma vitu kama kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa kisasa kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari! Tuendako ajira rasmi zitakuwa ngumu sana ni bora kujiandaa kwa hili
 
Umewaza vizuri,lakini kuondoa masomo hayo kwenye silabasi ni tatizo.

Labda ungeshauri masomo hayo yaongezwe, vinginevyo yakiondolewa watoto shule watakuwa wameenda kusomea ujinga.
 
Mkuu
Nadhani ungetafakari umuhimu wa masomo hayo kabla hujasema.
Mtu asiyejua ametoka wapi, Yuko wapi,na Anaenda wapi (HISTORIA).,huyo hapotei. Na hawezi kuona umuhimu wa historia.
2. Kukosa uzalendo, na utanzania kwa kizazi cha sasa ni kwa vile hawakusoma Uraia(civic) walifundishwa au walisoma Siasa. Baadhi ya vitendo vya kukosa uzalendo na uhujumu wa nchi vimesababishwa na kutokuwa na elimu ya uraia. Hivyo somo hilo ni la muhimu sana maana hata hicho kilimo kinahitaji wazalendo.
Mwisho, utambulisho wa mtu, huchangiwa na utamaduni wake, lugha yake na mila na desturi. Kiswahili ni moja ya utambulisho wetu hivyo kiswahili si chakubezwa unless mtu hajitambui.
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
 
Naunga mkono hoja na yafundishwe mpaka Chuo. Kuna maprofesa wanastafu wanatia aibu mitaani.
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
hiv wewe" unahakili timamu"Kwel!?
 
tofautisha mawazo mbadala na pumba zako. narudi tena ukiona post zangu pita kushoto. sitaki kusoma upumbavu mimi
Si ulisema unaniweka kwenye ignored list?

Ukiona mtu anataka awe anaona anachopenda kukiona pekee juwa ana element za udikteta
 
Wakitoe Kiswahili halafu iweje? Kuna nchi duniani isiyofundisha watu wake lugha?

Tena mimi ningependa masomo ya lugha yaongezwe na yakaziwe msumari. Watu wajifunze lugha nyingi kadiri inavyowezekana.

Shida yenu hata maana ya elimu bora hamfahamu! Mmejaa siasa siasa tu na ushabiki maandazi.

Elimu ya Tanzania ni nzuri isipokuwa inahitaji maboresho machache. Masomo yaongezwe lakini wanafunzi wafanye uchaguzi.

Niliwahi kuandika hapa kwamba "specialization" ianze kufanyika mapema kuanzia sekondari badala ya kuwatwika wanafunzi masomo yote wasome kila kitu.

Ongeza masomo, zidisha specialization.
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
Umeongea point mkuu ila nadhani wanasiasa na wasomi lazima wafanye mjadala wa kitaifa kuhusu hili suala....mambo ya kuambiana kwenye kampeni tumeongeza mikopo ya elimu ya juu akati wanazalisha mabaamedi na marioo mjini sio sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
Historia ikiondolewa wanasheria watapatikana wapi.Au hujui somo la sheria chuo kikuu msingi wake mkuu ni somo la historia na lugha.Enzi za mwalimu primary kulikuwa na somo la kilimo kama wameondoa sina uhakika.
Wazo lako kuhusu kuwepo somo la kilimo na ufugaji naunga mkono maana ajira hakuna na duniani kote bila kilimo ni kifo.
Nasema hivyo sababu najua kuna nchi au vinchi vidogo hawana ardhi ya kilimo lakini wanategemea nchi zingine kwa chakula sisi tuna ardhi tele.
Chakufanya wajue wapenyeze wapi haya masomo.
Kiswahili kukiondoa sio sawa mbona hukusema kiingereza kiondolewe.
China,Japan,Rwanda na Burundi na kwingineko kuna watu wao wanasoma Kiswahili chuo kikuu.
 
Nauga mkono hoja,haya masomo hayana maana angalau hata kiswahili,)civics,history yanamaana gani sasa? Kama sio kubana nafasi tu ya masomo mengine kichwani. Lakin historian ndio balaa zaidi unajiuliza kwanini nilazimishwe nimujui mzungu aliyekufa miaka 200 iliyopita atanisadia nini.
 
Naunga mkono hoja na kwa kuongezea hicho kilimo kiwe cha vitendo wanafunzi waende na majembe yenye mipini mifupi,shoka ,panga,chepe na toroli .Hakuna cha madaftari .Wamenyeke haswa mashambani .Shule zote zivunjwe.Mitihani ifanyikie pori la Burigi -Chato unapewa robo heka uilime kwa kutumia jembe lenye mpini mfupi na butu ulime eneo lenye vichuguu.Ukihitimu upewe majembe matano chapa jogoo ndio kiwe cheti chako.
 
Unashauri somo la Lugha inayotambulisha Taifa na Utamaduni wa Mtanzania iondolewe. Pia somo linalohusu maisha ya kila siku ya jamii yetu civics liondolewe???

Fikiri kwa mara ya pili.
Kiswahili tayari tunacho.kichwani ni.lugha yetu ya kila siku shule za msingi mtu kasoma kiswahili miaka Saba Tena masomo yote Bado tununampa zigo O level.Somo la kiswahili na uraia yafundishwe mwisho primary .Mtu akitaka kuwa specialist wa hayo masomo akayasome A Level.akitaka.
Mfano somo la economics hakifundishwi primary Wala O level liko A level Ya combination za ECA,HGE na EGM

Form four mtoto anakuwa kaiva kiumri kujitengemea Huwezi rudisha mtoto mtaani awezaye ongea tu Kama bwege kiswahili, history na Civics wakati hajui kulima,kufuga,Wala kupika hata maandazi au chapati kutumia ngano yetu auze apate pesa aache kelele za kusema ajira hamna

Elimu itoe wanafunzi wa kuajirika au kujiajiri Civics,kiswahili na history hayana huo ubavu yanazalisha wajinga tu Mitaani wasioweza jiajiri au kuajirika
 
We ni mpumbavu kweli.

Wakitoe Kiswahili halafu iweje? Kuna nchi duniani isiyofundisha watu wake lugha?

Tena mimi ningependa masomo ya lugha yaongezwe na yakaziwe msumari. Watu wajifunze lugha nyingi kadiri inavyowezekana.

Shida yenu hata maana ya elimu bora hamfahamu! Mmejaa siasa siasa tu na ushabiki maandazi.

Elimu ya Tanzania ni nzuri isipokuwa inahitaji maboresho machache. Masomo yaongezwe lakini wanafunzi wafanye uchaguzi.

Niliwahi kuandika hapa kwamba "specialization" ianze kufanyika mapema kuanzia sekondari badala ya kuwatwika wanafunzi masomo yote wasome kila kitu.

Ongeza masomo, zidisha specialization.
Malugha mengi ya kazi gani? Lugha anayotakiwa kujua mtu ni English, hii ukienda China, Ufaransa, Ujerumani, Canada, Japan, Iran, Suriname au popote pale lazima utawasiliana tu, ndio lugha ya Dunia hiyo na hakuna lugha ya taifa lolote isiyokuwa na direct translation to English

Tofauti na lugha Kama Kichina, ukijua Kichina ukaenda hata Iran kumpata Muiran anahejua Kichina ni ishu, hata kupata kamusi ya Farsi to Mandarin ni ishu

Kuanza kujifunza sijui Kifaransa, Kichina, Kihispaniola, ni mzigo tu, labda Kama unafanya kazi ya kupokea watalii
 
Unashauri somo la Lugha inayotambulisha Taifa na Utamaduni wa Mtanzania iondolewe. Pia somo linalohusu maisha ya kila siku ya jamii yetu civics liondolewe???

Fikiri kwa mara ya pili.
Hiyo lugha ya Kiswahili akimaliza shule atatumia hiyo kama asset wapi ili apate pesa?
Hiyo civics ataitumia wapi ili ajiajiri aitumie imwingizie pesa?
 
Ni kweli tuondoe fiction books watoto wasome reality books.Kama how to be a millionaire nk
Unajua kwamba non fiction inachosha Kusoma au kutizama?anagalia watoto walivo wepesi kufuatilia series hata mwaka mzima bila kuchoka lakini hawezi kusikiliza hotuba ya dakika 30 AI taarifa ya habari ya dkk 30.

Kinachotakiwa kuwekwa kwenye fiction hizo wanazosoma ni Ujumbe unaokusudiwa,kama ni mbinu za kilimo au how to be rich n.k.
 
Back
Top Bottom