Masoud Kipanya alimaanisha nini kwenye mchoro huu?

Aisee nimeona msokoto hapo kwenye hilo draft, weekend hii nangojea jioni nika-roll za kutosha nipoteze mawazo
Hivi anajua njia nzuri ya kula cannabis au mnachanganya na maua yenye high tetrahydrocannabinol concentration inayowehusha watu??
 
Masudi nae adhibitiwe huu mchoro wake unaweza kuzua taharuki binafsi nimetafsiri tofauti sana.....in a negative way
 
Ilo skeretoni ni rahisi kulihusisha na JPM cos alishafariki laiki ukitoa ilo hakuna kitu kingine ambacho unaweza kukihusisha na JPM hapo! Binafsi naona Mama yuko na Mafia fulani ndani ya chama chao.
 
Kitendo Cha mam kuguza kete moja .Ni moja kwa Moja zombi anaingia king
 
Skeleton imevaa kofia ya kijani ila kiwiliwili ni mifupa mitupu na inatisha ishara ya kwamba imejivika ngozi ya kondoo ila ni mbwa mwitu.

Kuna sigara au bangi inafuka moshi pia na mvinyo mezani vitu ambavyo ni haramu kwa mtu wa upande wa pili wa meza ila huyo mtu hana namna zaidi ya kuisikiliza skeleton.

Huyo mtu aliovaa ushungi imefikia hatua kachoka na kukata tamaa jinsi ambavyo mchezo na darsa linavyoenda kwani kuna kete mezani ishara ya kuwa kuna maamuzi anatakiwa kuyafanya .

Mbaya zaidi kalamu ambayo inatakiwa kuwa kwake ili afanye maamuzi lakini ipo kwa skeleton masikini hajui afanyeje.

Hata hivyo skeleton inalindwa na mtutu wa bunduki.
 
Maza anacheza michezo ya chama na chama ambacho kwa sasa kina michezo au siasa mfu. Yaani chama kisicho na uhai wa kisiasa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi anajua njia nzuri ya kula cannabis au mnachanganya na maua yenye high tetrahydrocannabinol concentration inayowehusha watu??
Wasiojua sayansi ya mmea wanaanza kwa pupa na jamii zenye THC kubwa wazoefu tunajua upi unafaa (THC ndogo ,CBD kubwa ama ya wastani), na wakati unaofaa...mimea ya huku Arusha inapendwa hata na watalii wastaarabu kwa sababu ukitaka experience iliyostaarabika ipo na ukitaka kuwehuka pia ipo, kwa hiyo mkuu tunakula inavyotakiwa
 
Safi mkuu..knowledge nzuri kuhusu jambo fulani ambalo unalifanya ni kitu poa sana.
 
Binafsi nmekuwa mfatiliaji wa Katuni au Vikaragosi vya Mchora katuni Nguli pengine wa Muda wote hapa Tanzania. Kikaragosi akiongeii ila utoa taarifa fulani juu ya kitu. Kama zilivyo kazi ngingine za Sanaa Vikaragosi pia uburudisha na kufkirisha sana.

Hivyo kulingana na Unyeti wa Kazi hizi za huyu bwana mkubwa kumekuwepo na hali ya baadhi ya wanajamii kufungua nyuzi nyingi za kuongeleaa katuni au vikaragosi vya Masoud maarufu kama Kipanya.

Nimeona ni busara sasa tuwe na uzi ambao utakuwa ni mkusanyiko wa vikaragosi vya Masoud ilii kutoa nafasi ya kujadili kwa pamoja ni ujumbe gani ulikusudiwa na mtunzi na mchoraji wa Vikaragosi hivii.

Vikaragosii hivii utokaa kwenye gazeti la Mwananchi au kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Masoudii....



Kwa kuanzia sasa ebu wanajamvii tuwaze hapa Kipanya alimaanisha nini.... Karibunii

Modes msiunganishe huu huziii
 
Uzi huo upo kitambo tu humu JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…