ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Subiri mkuu utaziona tiktakaHaiwezekani. Sheria zina loopholes nyingi sana kwenye kesi za madai
Ni sawa na nyumba ya urithi ukachukue shea ya mrithi kwa sababu unamdai. Haiwezekani.
Mali ya wanandoa huwa haiguswi na mtu ambaye si mwanandoa.
Hata mmoja awe anadaiwa trilioni bado mali ya ndoa haiguswi
Unaijua Hali aliuonayo mwijaku Sasa ivi? By the way msikilize vena wakili komba amesema hiyo ni beu ya kanzia, unaweza kupunguza au kuongezeka kulingangana na mahaka itakavyoakua.B500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Kipanya funga kabisa hilo dude jinga sana yaani funga na alipeKwa mujibu wa Wakili wa Masoud Kipanya, amesema Mtangazaji huto maarufu kwasasa anapata shida kujitokeza mbele ya watu kutokana na tuhuma za kujihusisha biashara haramu zilizotolewa na Mwijaku
Hayo yamebainishawa na Wakili wa Mtangazaji Masoud Kipanya, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates ambapo amedai mmteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya naye kazi.
Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au alipe Tsh 5 Bilioni.
View attachment 3018050
View attachment 3018110
View attachment 3018111
Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba
Mchora katuni maarufu, Ally Masoud Nyomwa “Masoud Kipanya”, anakusudia kumshtaki Mahakamani na kumdai fidia ya Tsh. Bilioni 5, Burton Mwemba Mwijaku kwa madai kumkashifu na kuandika maudhui ya uongo dhidi yake katika ukurasa wake wa Mtandaoni wa Facebook ambayo pia yanadaiwa kusambaa kwenye kurasa nyingine.
Ikielezwa kuwa hali hiyo imesababisha kumshushia heshima na kupelekea baadhi ya taasisi kusita kufanya naye kazi mbalimbali.
Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ni Wakili wa Kipanya ameyasema hayo Juni 14, 2024, Jijini Dar es Salaam.
Wakili huyo akizungumzia suala hilo mbele ya Vyombo vya Habari anasema Mwijaku alitoa maneno ya uongo bila ushahidi, kwamba Kipanya anabiashara haramu na ambayo imechangia kuharibu vijana wengi.
Madai mengine ambayo Wakili anadai yalitolewa na Mwijaku ni kwamba Kipanya amezoea kuwazodoa viongozi wa Nchi na marais kwa kuwadhalilisha pamoja na madai Kipanya amekuwa akihongwa kuichafua Serikali na viongozi wake.
Wakili huyo amesema Kipanya kabla ya kuja mbele ya Vyombo vya Habari na Umma alimpa siku tatu Mwijaku kuomba radhi kwa uzito uleule aliotumia kumchafua sambamba lakini siku tatu zilipita bila kufanya alivyoelekezwa.
Anasema barua hiyo iliyoandikwa Juni 7, 2024 na kupokelewa siku tatu tokea siku hiyo, ilimwelekeza Mwijaku kujitafakari na kuomba radhi kwa maandishi kupitia mitandao yote aliyotumia.
Aidha, amedai licha ya uwepo wa taarifa inayodaiwa kuwa ni 'Press Release' iliyotolewa na Mwijaku amesema Mteja wao msimamo wake kwa sasa ni kwamba anaona kwamba njia pekee ya kutumika kumrejeshea heshima yake ni Mahakama.
Wakili huyo amesema madai ambayo yametolewa na Mwijaku dhidi ya Kipanya hayana ukweli wowote na kuwa yameendelea kumuathiri mteja wao ambaye amekuwa akifanya majukumu yake yanayogusa jamii kwa uchanya.
Amesema kwa kuwa madai hayo yanagusa mamlaka nyingine, ameeleza matarajio yao kwa Vyombo vya dola na taasisi nyingine zitakuwa zinachukua hatua, lakini amedai kwa upande wao pia wapo tayari kutoa ushirikiano kulingana na taratibu.
Amesisitiza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ambayo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa, inatoa uhuru wa kujieleza lakini pia uhuru huo una wajibu.
Pia Soma:
- Mwijaku amwandikia Waraka Mzito Masoud Kipanya, adai anafanya biashara haramu
- Mwijaku amuomba msamaha Masoud Kipanya baada ya kumtuhumu kuwa “anafanya biashara haramu” na kutukana Viongozi akiwemo Rais
Ni b5 boss sio b 500.B500 unaifahamu lakini? Hapo kwenye B500 ndo inapokosa userious.
Na mke tutamchukua, kazidi sana kuvuka mipaka. Analeta kujuana hadi kwenye mambo hatarishi. Kashfa ya dili haramu sio nzuri kipanya akomae nae.Tutakamata ghorofa, tutakamata magari, tutakamata mshahara wake tutamuachia mke tu.
This time he mess up with a wrong dude. Big time.
Sasa sheria zikoje asipolipa atafungwa?? Na ni miaka mingapi kwa mfano?Ata 1% ya iyo hela Mwijaku hana.
Sijui msomi gani yule, unaeza toa tuhuma bila hata kutaja jina, ili iwe ngumu kutiwa hatiani sasa yeye msomi hata mitego midogo ya kisheria hajui,
MTU anaedhalilisha watu hastahili kuonewa hurumaSijui kwanini nimemuonea huruma Mwijaku..!😣
Ingawa Mwijaku halikosea, ila kitendo cha kutuhumiwa kwa Kipanya kufanya biashara haramu kuna walakini pia.Hakua specific. Either ngada, danguro au kuwadhamini upinde. Ivyo ndio vitu haramu.
Is not about crown, mdomo wa jamaa hauna breki hauna mipaka. its time awajinishwe , si kila mtu anahitaji mdomo wakeB500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Sheria huwa hazisemi hivyo mkuu. Unadhani wale ambao mali zao hupigwa minada huwa ni mabachela pekee? Kuna watu walijsribu kuleta uhuni huo, yaani mali zilipokamatwa mke ndiyo akaenda kukataa mahakamani kwamba hatambui deni sababu hakuwahi kuambiwa na mali zinazokamatwa ni matrimonial properties, lakini wakaangukoa pua.Kwa jinsi sheria zilivyo Ghorofa haliwezi kuuzwa na mahakama sababu. Ni matrimonial property. Mwijaku sio lake peke yake. Na Mke wa mwijaku hausiki kwenye hiyo kesi ya madai.
Mahakama itakwama kukamata ghorofa.
Kesi za madai ni ngumu sana kwenye kukamata mali za wanandoa. Kesi za madai ni nyepesi sana kama unaidai kampuni. Maana kampuni haiingiliwi na watu. Hivyo mali za kampuni unazikamata tu na kuziuza.
Pia kesi za madai zina ujinga wa kulipa kidogo kidogo. Hata elfu 10 kwa mwezi ruksa
Vipi mwijaku akisimama mahakamani na kusema Kipanya alikuwa akifanya biashara haramu ya kutangaza pombe kipindi cha maisha plus . Unywaji wa pombe ni hatari kwa afya za vijana wengi. Kidini upande wa uislam pombe ni haram
Hakuna huo usiriasiHii ishu ipo serious