Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu

Haiwezekani. Sheria zina loopholes nyingi sana kwenye kesi za madai

Ni sawa na nyumba ya urithi ukachukue shea ya mrithi kwa sababu unamdai. Haiwezekani.

Mali ya wanandoa huwa haiguswi na mtu ambaye si mwanandoa.

Hata mmoja awe anadaiwa trilioni bado mali ya ndoa haiguswi
Subiri mkuu utaziona tiktaka
 
B500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Unaijua Hali aliuonayo mwijaku Sasa ivi? By the way msikilize vena wakili komba amesema hiyo ni beu ya kanzia, unaweza kupunguza au kuongezeka kulingangana na mahaka itakavyoakua.
 
Kwa mujibu wa Wakili wa Masoud Kipanya, amesema Mtangazaji huto maarufu kwasasa anapata shida kujitokeza mbele ya watu kutokana na tuhuma za kujihusisha biashara haramu zilizotolewa na Mwijaku

Hayo yamebainishawa na Wakili wa Mtangazaji Masoud Kipanya, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates ambapo amedai mmteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya naye kazi.

Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au alipe Tsh 5 Bilioni.

View attachment 3018050
View attachment 3018110
View attachment 3018111
Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba

Mchora katuni maarufu, Ally Masoud Nyomwa “Masoud Kipanya”, anakusudia kumshtaki Mahakamani na kumdai fidia ya Tsh. Bilioni 5, Burton Mwemba Mwijaku kwa madai kumkashifu na kuandika maudhui ya uongo dhidi yake katika ukurasa wake wa Mtandaoni wa Facebook ambayo pia yanadaiwa kusambaa kwenye kurasa nyingine.

Ikielezwa kuwa hali hiyo imesababisha kumshushia heshima na kupelekea baadhi ya taasisi kusita kufanya naye kazi mbalimbali.

Wakili Msomi Mwandamizi wa Kampuni ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ni Wakili wa Kipanya ameyasema hayo Juni 14, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Wakili huyo akizungumzia suala hilo mbele ya Vyombo vya Habari anasema Mwijaku alitoa maneno ya uongo bila ushahidi, kwamba Kipanya anabiashara haramu na ambayo imechangia kuharibu vijana wengi.

Madai mengine ambayo Wakili anadai yalitolewa na Mwijaku ni kwamba Kipanya amezoea kuwazodoa viongozi wa Nchi na marais kwa kuwadhalilisha pamoja na madai Kipanya amekuwa akihongwa kuichafua Serikali na viongozi wake.

Wakili huyo amesema Kipanya kabla ya kuja mbele ya Vyombo vya Habari na Umma alimpa siku tatu Mwijaku kuomba radhi kwa uzito uleule aliotumia kumchafua sambamba lakini siku tatu zilipita bila kufanya alivyoelekezwa.

Anasema barua hiyo iliyoandikwa Juni 7, 2024 na kupokelewa siku tatu tokea siku hiyo, ilimwelekeza Mwijaku kujitafakari na kuomba radhi kwa maandishi kupitia mitandao yote aliyotumia.

Aidha, amedai licha ya uwepo wa taarifa inayodaiwa kuwa ni 'Press Release' iliyotolewa na Mwijaku amesema Mteja wao msimamo wake kwa sasa ni kwamba anaona kwamba njia pekee ya kutumika kumrejeshea heshima yake ni Mahakama.

Wakili huyo amesema madai ambayo yametolewa na Mwijaku dhidi ya Kipanya hayana ukweli wowote na kuwa yameendelea kumuathiri mteja wao ambaye amekuwa akifanya majukumu yake yanayogusa jamii kwa uchanya.

Amesema kwa kuwa madai hayo yanagusa mamlaka nyingine, ameeleza matarajio yao kwa Vyombo vya dola na taasisi nyingine zitakuwa zinachukua hatua, lakini amedai kwa upande wao pia wapo tayari kutoa ushirikiano kulingana na taratibu.

Amesisitiza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ambayo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa, inatoa uhuru wa kujieleza lakini pia uhuru huo una wajibu.

Pia Soma:

- Mwijaku amwandikia Waraka Mzito Masoud Kipanya, adai anafanya biashara haramu

- Mwijaku amuomba msamaha Masoud Kipanya baada ya kumtuhumu kuwa “anafanya biashara haramu” na kutukana Viongozi akiwemo Rais
Kipanya funga kabisa hilo dude jinga sana yaani funga na alipe
 
Mijitu kama hii inaharibu tasinia ya habari nakufanya taifa kuwa la wapiga upatu nakulamba miguu ya mabwana
 
Kama ataadhibiwa basi iwe fundisho kwa machawa na waropokaji wote walio jificha kwenye kichaka cha uwandishi wa habari wakati hawajakaa dasarani kusomea tasnia ya habari ila wameajiriwa kijanja janja.
 
B500 Masudi nae hayuko serious inakuwa kama kiki tu ya kuikuza Crown kwamba sasa watu wamfatilie Mwijaku akiwa Crown anasema nini kuhusu hilo huku clouds ikiendelea kufuatiliwa.
Is not about crown, mdomo wa jamaa hauna breki hauna mipaka. its time awajinishwe , si kila mtu anahitaji mdomo wake
 
Kwa jinsi sheria zilivyo Ghorofa haliwezi kuuzwa na mahakama sababu. Ni matrimonial property. Mwijaku sio lake peke yake. Na Mke wa mwijaku hausiki kwenye hiyo kesi ya madai.

Mahakama itakwama kukamata ghorofa.

Kesi za madai ni ngumu sana kwenye kukamata mali za wanandoa. Kesi za madai ni nyepesi sana kama unaidai kampuni. Maana kampuni haiingiliwi na watu. Hivyo mali za kampuni unazikamata tu na kuziuza.

Pia kesi za madai zina ujinga wa kulipa kidogo kidogo. Hata elfu 10 kwa mwezi ruksa
Sheria huwa hazisemi hivyo mkuu. Unadhani wale ambao mali zao hupigwa minada huwa ni mabachela pekee? Kuna watu walijsribu kuleta uhuni huo, yaani mali zilipokamatwa mke ndiyo akaenda kukataa mahakamani kwamba hatambui deni sababu hakuwahi kuambiwa na mali zinazokamatwa ni matrimonial properties, lakini wakaangukoa pua.
 
Vipi mwijaku akisimama mahakamani na kusema Kipanya alikuwa akifanya biashara haramu ya kutangaza pombe kipindi cha maisha plus . Unywaji wa pombe ni hatari kwa afya za vijana wengi. Kidini upande wa uislam pombe ni haram

1.serikali ya Tanzania haina dini

2. Haramu ya dini si haramu ya serikali mfano dini zote mbili uislamu na ukristo zimekataza riba ila serikali inakopesha kwa riba Kwa hiyo kutangaza pombe kiserikali ni halali kama hiyo kampuni imesajiliwa na pombe zipo kwenye ubora stahiki bali kidini ni kharamu.

3. Kwenye unywaji wa pombe kuna kauli huwa wanatumia "kunywa kistaarabu".

4. Mpaka hapo mwijaku ataombwa atoe ushahidi wenye nguvu kabisa ku support alichoiambia jamii akishindwa basi kama mwanasheria alivyosema watapika damage aliyoipata jamaa kisha utabidi alipwe na pia mwijaku itabidi atoke mbele ya hadhara kisha amsafishe masoud .
 
Back
Top Bottom