Masoud Kipanya aongeza mke wa nne

Watu wa mjini ndiyo wanadiss hizi mambo za mitala. Lakini mikoa ndani ndani huko watu kuoa mitala kawaida hata kama dini zao haziruhusu.
 
Punguza wivu
 
Umewaita, sasahivi wanakuja na mabomu yao
 
Ni dini yako?
 
Duh!
Kumbe wanne,
Nlijua wa pili,
Heko kwake
 
Uchu tu!hakuna mwanaume wa miaka 50 anaeweza kuridhisha wanawake wanne labda atumie booster
 
Kwahiyo Mfalme Suleiman na hekima zake zote alikuwa anazini?

Alikuwa na wake 700 na masulia 300.
Uki soma vitabu vya Mfalume Suleiman uta ana sema kabisa yote aliyo fanya ni "utupu na kujilisha upepo" yani ana juta, ana hakuona faida yoyote ya kua na wake wengi.

Kwenye ulimwengu wa kistaarabu tu kuwa na wanawake wanne ni ubatili. Yani hisia zime zidi ufahamu wako ama zime kutawala.
 
Hizo ni tamaa tu hata kama dini inalihusu lakin mazingira yamebadilika
Kivipi? Mazingira yanafanyaje suala la kuoa mke zaidi ya mmoja kwa Waislam lisiwezekane?
Hata Huko Uarabuni vijana wengi wa huko Sasa hivi wanaoa mwanamke mmoja tu
Hao vijana sio viigizo vyetu katika Dini yetu. Viigizo vyetu sisi ni Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) na Maswahaba zake (Salaf).

Hivyo sisi na hao vijana wa Kiarabu wote tunatakiwa kuiga kutoka kwa viigizo vyetu katika Uislam.


.Kuoa wanawake wengi ni migogoro katika familia
Elezea kivipi?
Sawa ana uwezo wa kuwahudumia na ni maisha yake lakini sio mfano wa kuigwa katika jamaii .Ingekua vizuri Sana nisikie Kipanya kafungua kampuni na sio kuongeza mke wa nne.
Kwahiyo Mtu asiifuate dini yake inavyomfundisha kwa kuhofia jamii (ambayo ndani yake pia kuna watu wasio katika dini yake). Masoud Kipanya kufanya hivi ni mfano mzuri kwa Waislam wanaofuata Dini. Wewe kama sio Muislam subiri afungue Kampuni umsifu. Suala la Dini yake halikuhusu.
 
Waarabu wa sasa sio kiigizo katika Dini. Tayari Waislam Duniani kote wana wa kuwaiga katika kuifuata Dini. Hao Waarabu wako pia wanatakiwa waige mfano wa Salaf. Kama hawafanyi hivyo basi ni wao wanazembea kama vile tunavyozembea baadhi yetu sisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…