Masoud Kipanya: Viongozi wetu ni wafupi

Masoud Kipanya: Viongozi wetu ni wafupi

Nguli wa vibonzo, ndugu Masoud Kipanya amedai tatizo kubwa la Viongozi ni ufupi na ni lazima sasa tuhitaji Viongozi warefu.

'...unakuta raia unalalamika kwa jambo fulani ajabu kwalo Kiongozi naye analalamikia hilohilo kitu ambacho kinaondoa utofauti wa Muongozwa na Kiongozi.'

'....ni muda sasa tupate Viongozi warefu na si wafupi wa kila kitu kama waliopo sasa.'

Kipanya.
View attachment 2427592
Hakika Kipanya ameongea ukweli halisi na ni tatizo kubwa linalotukabili hapa Tanzania.Kwanza hatuna muongozo halisi wa kuwapata viongozi .Watu wengi ambao hawana sifa za uongozi ,na hawana vision yeyote ndio wanachaguliwa kuwa viongozi ,kwa kuwa tu ni watoto wa viongozi wa Zamani au ni Wana ccm.Mm narudi nyuma kuwa tunaendelea kupoteza dira kwa kuwa marehemu Nyerere hakuandaa dira yetu.
 
Watu wanaingia kwenye siasa kwa malengo yao binafsi.

Tatizo linaanzia hapo.
 
Too general statiment
Mtu akitoa sentensi kama hizi maana yake anajificha nyuma ya tasfida na hapo ni kukwepa uwajibikaji na uwezo mdogo wa kuwa wazi na kunyooka kwenye hoja
Sasa viongozi wafupi ni akina nani? Watajwe

Ni matumizi ya lugha tu, unachopaswa kukielewa hapo ni tafsiri ya tamathali iliyotumika...
 
Too general statiment
Mtu akitoa sentensi kama hizi maana yake anajificha nyuma ya tasfida na hapo ni kukwepa uwajibikaji na uwezo mdogo wa kuwa wazi na kunyooka kwenye hoja
Sasa viongozi wafupi ni akina nani? Watajwe
Yeye ameanza malizia wewe
 
Nguli wa vibonzo, ndugu Masoud Kipanya amedai tatizo kubwa la Viongozi ni ufupi na ni lazima sasa tuhitaji Viongozi warefu.

'...unakuta raia unalalamika kwa jambo fulani ajabu kwalo Kiongozi naye analalamikia hilohilo kitu ambacho kinaondoa utofauti wa Muongozwa na Kiongozi.'

'....ni muda sasa tupate Viongozi warefu na si wafupi wa kila kitu kama waliopo sasa.'

Kipanya.
View attachment 2427592
Hivi kipanya motor's imeishia wapi au ndio serikali isha zima ndoto zake.
 
Too general statiment
Mtu akitoa sentensi kama hizi maana yake anajificha nyuma ya tasfida na hapo ni kukwepa uwajibikaji na uwezo mdogo wa kuwa wazi na kunyooka kwenye hoja
Sasa viongozi wafupi ni akina nani? Watajwe
Akitaja si ndio anaharibu inakuwa kama vita?.
Anachomaanisha ni viongozi wawe sehemu ya utatuzi wa matatizo kuliko kuwa chanzo cha tatizo
 
Kwamba alitakiwa afanyike utatuzi wa kutochoma vifaranga hakuwa badala yake sasa naye analalamika sio?
Mbele ya lile jitu nani angeweza kusema ngw'e!!!! Walioweza ni wawili tu nchi mzima Lissu na Sheikh Ponda wengine woooote nyongo zilikua zinatumbukia tu tumboni tukiwa kimya
 
Too general statiment
Mtu akitoa sentensi kama hizi maana yake anajificha nyuma ya tasfida na hapo ni kukwepa uwajibikaji na uwezo mdogo wa kuwa wazi na kunyooka kwenye hoja
Sasa viongozi wafupi ni akina nani? Watajwe
Viongozi wafupi ni wale wasio na maono ya mbali wanaovitazama vitu kwa upeo mdogo
 
Too general statiment
Mtu akitoa sentensi kama hizi maana yake anajificha nyuma ya tasfida na hapo ni kukwepa uwajibikaji na uwezo mdogo wa kuwa wazi na kunyooka kwenye hoja
Sasa viongozi wafupi ni akina nani? Watajwe
Tuseme tu ukweli, yule bibi kizee wa Kizanzibari ni "mfupi sana".
 
Mbele ya lile jitu nani angeweza kusema ngw'e!!!! Walioweza ni wawili tu nchi mzima Lissu na Sheikh Ponda wengine woooote nyongo zilikua zinatumbukia tu tumboni tukiwa kimya
Lakini angenyamaza milele, naona ni unafiki kwasasa kuongea aliyoshindwa kuyafanya wakati ule
 
Back
Top Bottom