Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Wana Jamiiforums huyu Member mwenye kuitwa Lucas Mwashambwa amekuwa na maandiko yenye ushabiki usio na hoja, unaokusudia kusifia kwa lugha ya mihemko badala ya kutathmini uhalisia wa utawala wa Rais Samia kwa hoja na takwimu.
Nimetumia muda mwingi kufuatilia maandiko yako ambayo yamenipelekea kupata maswali 12 ambayo ningemtaka ayajibu kwa hoja na takwimu zenye utafiti kama jinsi nilivyo yauliza hapa.
Hoja zake nyingi zimejikita kwenye kusifia sana ninamtaka anijibu haya maswali
1. “Tuna kiongozi mwenye maono…”
Maono gani hasa?
Kama maono ni kuuza Bandari kwa mkataba wa kifisadi bila ridhaa ya Bunge, basi hizo si ndoto za kiongozi bali za kikundi cha mafisadi.
Kama ni maono ni kuendelea kutumia trilioni 1.3 kwenye safari za nje bila impact kubwa kwa ajira za vijana, basi ni maono ya kujinufaisha.
2. “Nyuso za Watanzania zina bashasha na matumaini”
Uko nchi gani wewe?
Bei ya unga, mafuta, na umeme vimepanda kuliko wakati wowote, huku mishahara ya wafanyakazi ikiwa haikidhi mahitaji miaka nenda miaka rudi.
Dada zetu wanauza miili, wengine wanatorokea Arabuni kutumwa kama watumwa hiyo ndiyo bashasha unayoiona?
3. “Rais anatoka na ajira kwa vijana”
Ajira ipi?
Kwa mujibu wa ripoti ya NBS (2023), zaidi ya watanzania milioni 4 hawana ajira.
Graduates wanamaliza vyuo kwa maelfu kila mwaka, wanaishia kuuza genge au bodaboda.
Serikali yenyewe ndiyo mwajiri mkubwa, lakini imebana ajira miaka yote. Mbona mnashindwa kutangaza nafasi wazi?
4. “Rais ni Field Marshall, Komandoo, Mwanga...”
Sifa za kijeshi hazitatupeleka mbali.
Tungependa kusikia Rais ni mwenye mikakati ya kupambana na rushwa, si “Komandoo” wakati TAKUKURU ni kama kikundi cha kupamba mikutano ya chama.
Rushwa iko TRA, mahakamani, bandari, halmashauri, kwenye tume ya uchaguzi — na “Field Marshall” anaangalia tu.
5. “Aliye madarakani ana kibali cha Mungu”
Mungu si CCM.
Watanzania walinyimwa haki ya msingi ya kidemokrasia: uchaguzi wa serikali za mitaa uligubikwa na mizengwe, wapinzani wanazuiliwa kukutana, polisi na msajili wanatumika kama silaha za chama tawala.
Mungu hawezi kuwa upande wa wanaowatesa watu wake. Msilitumie jina la Mungu kuficha uovu.
6. “Samia analeta furaha kwa mamilioni”
Acha mzaha.
Je, hiyo furaha ipo Tandahimba ambako wakulima hawalipwi fedha zao?
Ipo Katavi ambako kuna upungufu wa madaktari, au Mwanza ambako wamama wanajifungulia sakafuni?
Ipo kwa vijana waliokosa mkopo wa elimu kwa sababu ya kipato cha wazazi wao kilichotafsiriwa kimakosa?
7.>Umefanyika neema kwa makundi yote”
Acha kudanganya:
Wakulima wa korosho, pamba, kahawa hawalipwi kwa wakati.
Wafanyakazi wa sekta binafsi hawana mishahara ya heshima wala pensheni ya uhakika.
Wafanyabiashara wadogo wananyanyaswa na TRA na halmashauri kila siku.
Upinzani unakandamizwa, mikutano inazuiwa, viongozi wanapigwa risasi na kukamatwa ni neema hiyo?
Kama hii ndiyo neema, basi heri ya laana yenye haki kuliko neema ya uonevu.
8.> Kazi iendelee”
Kazi ipi hasa?
Kazi ya kufunika ufisadi wa viongozi serikalini?
Au kazi ya kutumia Mahakama, Polisi, TAKUKURU na Msajili kama fimbo dhidi ya wapinzani?
Au kazi ya safari zisizoisha nje ya nchi bila impact ya moja kwa moja kwa wananchi?
Kazi ambayo haileti tija kwa mwananchi wa kawaida si kazi — ni dhuluma ya kifahari.
9.> “Mama ni nuru ya taifa letu”
Tazama “nuru” hii kwa uhalisia wake: – Afya: Wagonjwa wanalala chini hospitalini, madaktari wanalia, dawa hakuna.
Elimu: Vyumba havatoshi, wanafunzi wanakalia mawe, walimu hawatoshi.
Miundombinu: Barabara vijijini ni majanga, miradi mingi ni ya picha na kelele.
Maji: Zaidi ya nusu ya watanzania bado wanabeba maji kwa ndoo kutoka mito yenye matope.
Hii si nuru ni kivuli kizito kilichopakwa maneno matamu kuwapumbaza maskini.?
Lucas Mwashambwa usitake kutufunga macho kwa lugha ya kidini na mashairi ya kipuuzi.
Mama si mungu. Mama ni binadamu, na binadamu hukosolewa. Taifa haliwezi kuongozwa kwa nyimbo za sifa zisizo na mizani.
Tunataka maendeleo yenye usawa, haki, na uwajibikaji si furaha feki ya mitandaoni ilhali watu vijijini wanalala njaa.