Maswali 10 kuhusu maandiko ya Lucas Mwashambwa na hoja zake

Hakuna kitu bora kama uhuru wa kutoa maoni haswa kwa jukwaa kama hili.
Maoni hayawezi kufanana wala kufaa kwa kila mtu lakini kubwa kila mmoja wetu ana pewa nafasi sawa ya kutoa maoni ili mradi tu haya utwezi utu.

Kinyume na hivyo huyu bwana luka alipaswa kuzuiliwa kutoa maoni na mada , kwa sababu mada na maoni yake hayana mashiko na yana tia mafadhaiko kwa kila anae msoma.
Ndugu Pendaelli mbona unajipinga mwenyewe tena..?

Paragraph ya kwanza umeanza vizuri sana, na huo ndio ukweli, kwamba kila mtu ana uhuru wa kujieleza ili mradi havunji sheria ikiwemo kutweza utu wa watu wengine na bila kujali kujieleza kwake huko kunawafurahisha wengine au kunawaudhi; wanaelewa au hawaelewi nk....

Lakini kwenye paragraph ya pili ukapinga ulichokiandika kwenye para ya kwanza kwa kutaka ndugu Lucas Mwashambwa azuiliwe kujieleza humu (kutumia uhuru wake wa kujieleza). Sbb unazozitoa ni kuwa maandiko yake hayana mashiko na kutia mfadhaiko kwa kila asomaye🤪🤪...!!

Mimi nilidhani kuwa ungesema "azuiliwe kwa kuwa maandiko yake yanavunja sheria fulani au yanatweza utu wa watu" lakini kumbe ni wewe tu unayaona hayana mashiko na yanafadhaisha...!

Kuhusu huyu ndugu Lucas Mwashambwa na chawa wengine wa mama Chura Kiziwi ushauri wangu kwako na kwa wengine uko hivi:​

Wewe msomaji ukiona, andiko la fulani halina maana na ni porojo tu zilizotiwa chumvi ya uongo na udanganyifu (propaganda) unaachana naye huyo mtu na kumweka kwenye orodha ya "waliopuuzwa" au "ignore list..."

However, nakubaliana na wewe kabisa kuwa maandiko yote ya Lucas Mwashambwa huwa ni propaganda za uongo na karibu yote huwa ni kumsifia na kumpamba Chura Kiziwi Samia Suluhu Hassan ambaye tunaamini ni Rais wa Tanganyika lakini siyo...

Lakini unategemea aandike nini iwapo anategemea uchawa kula chakula chake na familia yake..?

Acha atumie uhuru wake wa kujieleza. Uhuru wa kujieleza siku zote hutegemewa ulete manufaa kwa wanaokusikiliza au kusoma. Lakini huyu Lucas Mwashambwa hupoteza nguvu nyingi kuandika ujinga na upumbavu usiomsaidia mtu yeyote na wakati huohuo akijifu kuwa "na mimi natumia uhuru wangu wa kujieleza...!"

Asante..
 
Naomba uandike hayo unayoona sijaandika. Mimi naona juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Rais Samia. Kumbuka kuwa hakuna Nchi isiyo na changamoto.hata Marekani kuna changamoto kibao
We ni mjinga kabisa mbona hujajibu hizo hoja na unaonyeaha wewe una matatizo ya akili.

Ni kweli hakuna nchi isiyo na changamoto hata Marekani ina matatizo.

Lakini je,
changamoto zao zinatokana na vyombo vya dola kuua raia wao ili kulinda chama tawala? Huko Marekani polisi akimpiga raia risasi hovyo, kuna maandamano, vyombo vya habari huru vinapaza sauti, na viongozi wanajibishwa.

Sasa huku kwetu:

CAG anatoa ripoti kila mwaka ya mabilioni kupotea (2023/2024: zaidi ya Tsh 375 bilioni zilitumika bila maelezo sahihi), lakini hakuna anayekamatwa wala kuwajibishwa.

Vijana hawana ajira, lakini miradi inayozalisha ajira haijapewa kipaumbele badala yake, hela inaishia kwenye "kodi ya samaki" na safari zisizoisha.

Mikopo ya elimu inakopeshwa kwa masharti magumu, wengine hawapati kabisa — huku viongozi wakisomesha watoto wao Ulaya kwa pesa za walalahoi.

Hospitali hazina dawa, huku wakubwa wakitibiwa nje ya nchi kwa kodi zetu.

Vyombo vya dola vimetumika kudhibiti upinzani, badala ya kulinda wananchi. Viongozi wa CHADEMA wamefungwa au kunyanyaswa, wengine kuuawa au kutoweka, lakini hakuna uchunguzi huru.

Haya siyo matatizo ya "changamoto za kawaida" kama barabara au mvua zisizoeleweka hizi ni changamoto zinazotengenezwa kwa makusudi na watawala kwa maslahi yao.

Kwa hiyo, kabla hujasema “Samia ni Mwanga na nuru,” jiulize: Samia ni nuru inayowaka kwa baadhi, lakini inawazimia mamilioni ni nuru ya aina gani?
 
Manyanza umeandika kwa kutulia sana, ila shida uliyemwandikia na kuhitaji hayo majibu, nasikitika kusema hakuna ambacho atakujibu. Ni mbinafsi na mfukuzia tonge tu huyo, hakuna mtu mwenye akili timamu, kila siku akiamka, ni kuandika ujinga ambao huwa anauandika.

Kinachochosha zaidi, watu kujazana, hata kama wanambeza kwenye comments ni kama chizi akuchukulie nguo zako ukiwa unaoga mtoni, wewe umfukuze ukiwa mtupu, lazima wewe unayemkimbiza ndiyo utaonekana chizi.
Kweli kabisa Mkuu Bantu Lady 😃😃😃
Huyu jamaa ni debe tupu na ana matatizo kiakili lakini kumwandikia kama hivi maandiko yenye ujazo yanasaidia ku adjust akili yake. Sitochoka kumpiga spana kwani si amebaki yeye tu humu anayeandika ujinga kwa sasa?
 
Ndg yangu Manyanza nimekuonea huruma sana kupoteza muda wako kumuazishia uzi jamaa asiyekuwa na akili hata kidogo.
Huyu jamaa utofauti wa ubongo wake na kinyesi chake ni rangi na harufu tu.
Omukaya Nikifa MkeWangu Asiolewe huyu boya kama ni nafasi ya kumpiga spana lazima nimkaze kweli kweli kwa hoja za nguvu. Hoja ninazoandika zinawanufaisha na wengine kujua udhaifu wa utawala huu na halafu anatokea mpuuzi kana huyu anajiachia kwa kuandika mihemko na ushabiki kwa nini anyamaziwe?
 
Mithali 27:22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
 
Wana Jamiiforums huyu Member mwenye kuitwa Lucas Mwashambwa amekuwa na maandiko yenye ushabiki usio na hoja, unaokusudia kusifia kwa lugha ya mihemko badala ya kutathmini uhalisia wa utawala wa Rais Samia kwa hoja na takwimu.

Nimetumia muda mwingi kufuatilia maandiko yako ambayo yamenipelekea kupata maswali 12 ambayo ningemtaka ayajibu kwa hoja na takwimu zenye utafiti kama jinsi nilivyo yauliza hapa.

Hoja zake nyingi zimejikita kwenye kusifia sana ninamtaka anijibu haya maswali

1. “Tuna kiongozi mwenye maono…”
Maono gani hasa?

Kama maono ni kuuza Bandari kwa mkataba wa kifisadi bila ridhaa ya Bunge, basi hizo si ndoto za kiongozi bali za kikundi cha mafisadi.

Kama ni maono ni kuendelea kutumia trilioni 1.3 kwenye safari za nje bila impact kubwa kwa ajira za vijana, basi ni maono ya kujinufaisha.

2. “Nyuso za Watanzania zina bashasha na matumaini”
Uko nchi gani wewe?
Bei ya unga, mafuta, na umeme vimepanda kuliko wakati wowote, huku mishahara ya wafanyakazi ikiwa haikidhi mahitaji miaka nenda miaka rudi.

Dada zetu wanauza miili, wengine wanatorokea Arabuni kutumwa kama watumwa hiyo ndiyo bashasha unayoiona?

3. “Rais anatoka na ajira kwa vijana”

Ajira ipi?

Kwa mujibu wa ripoti ya NBS (2023), zaidi ya watanzania milioni 4 hawana ajira.

Graduates wanamaliza vyuo kwa maelfu kila mwaka, wanaishia kuuza genge au bodaboda.

Serikali yenyewe ndiyo mwajiri mkubwa, lakini imebana ajira miaka yote. Mbona mnashindwa kutangaza nafasi wazi?

4. “Rais ni Field Marshall, Komandoo, Mwanga...”

Sifa za kijeshi hazitatupeleka mbali.

Tungependa kusikia Rais ni mwenye mikakati ya kupambana na rushwa, si “Komandoo” wakati TAKUKURU ni kama kikundi cha kupamba mikutano ya chama.

Rushwa iko TRA, mahakamani, bandari, halmashauri, kwenye tume ya uchaguzi — na “Field Marshall” anaangalia tu.

5. “Aliye madarakani ana kibali cha Mungu”

Mungu si CCM.

Watanzania walinyimwa haki ya msingi ya kidemokrasia: uchaguzi wa serikali za mitaa uligubikwa na mizengwe, wapinzani wanazuiliwa kukutana, polisi na msajili wanatumika kama silaha za chama tawala.

Mungu hawezi kuwa upande wa wanaowatesa watu wake. Msilitumie jina la Mungu kuficha uovu.

6. “Samia analeta furaha kwa mamilioni”

Acha mzaha.

Je, hiyo furaha ipo Tandahimba ambako wakulima hawalipwi fedha zao?

Ipo Katavi ambako kuna upungufu wa madaktari, au Mwanza ambako wamama wanajifungulia sakafuni?

Ipo kwa vijana waliokosa mkopo wa elimu kwa sababu ya kipato cha wazazi wao kilichotafsiriwa kimakosa?

7.>Umefanyika neema kwa makundi yote”

Acha kudanganya:
Wakulima wa korosho, pamba, kahawa hawalipwi kwa wakati.

Wafanyakazi wa sekta binafsi hawana mishahara ya heshima wala pensheni ya uhakika.

Wafanyabiashara wadogo wananyanyaswa na TRA na halmashauri kila siku.

Upinzani unakandamizwa, mikutano inazuiwa, viongozi wanapigwa risasi na kukamatwa ni neema hiyo?

Kama hii ndiyo neema, basi heri ya laana yenye haki kuliko neema ya uonevu.

8.> Kazi iendelee”

Kazi ipi hasa?

Kazi ya kufunika ufisadi wa viongozi serikalini?

Au kazi ya kutumia Mahakama, Polisi, TAKUKURU na Msajili kama fimbo dhidi ya wapinzani?

Au kazi ya safari zisizoisha nje ya nchi bila impact ya moja kwa moja kwa wananchi?

Kazi ambayo haileti tija kwa mwananchi wa kawaida si kazi — ni dhuluma ya kifahari.

9.> “Mama ni nuru ya taifa letu”

Tazama “nuru” hii kwa uhalisia wake: – Afya: Wagonjwa wanalala chini hospitalini, madaktari wanalia, dawa hakuna.

Elimu: Vyumba havatoshi, wanafunzi wanakalia mawe, walimu hawatoshi.

Miundombinu: Barabara vijijini ni majanga, miradi mingi ni ya picha na kelele.

Maji: Zaidi ya nusu ya watanzania bado wanabeba maji kwa ndoo kutoka mito yenye matope.

Hii si nuru ni kivuli kizito kilichopakwa maneno matamu kuwapumbaza maskini.?

Lucas Mwashambwa usitake kutufunga macho kwa lugha ya kidini na mashairi ya kipuuzi.
Mama si mungu. Mama ni binadamu, na binadamu hukosolewa. Taifa haliwezi kuongozwa kwa nyimbo za sifa zisizo na mizani.

Tunataka maendeleo yenye usawa, haki, na uwajibikaji si furaha feki ya mitandaoni ilhali watu vijijini wanalala njaa.
Mkuu unapata shida na huyu Lucas Mwashambwa ambaye humu jukwaani Kapuuzwa kwa kiwango kikubwa.
 
Umesahaua kububujikwa na machozi.

Huyu sijui km ni mzima aisee hii sio normal Kwa mwanaume
 
Hitimisho
Tuna viongozi wanao ahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data, tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

CCM wanatumia mfumo wa unyumbu wa kisiasa kuongoza nchi

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo unao wezesha wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi kwanjia ya kujipendekeza ama kwa uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki)

Human herding in politics is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of working towards group objectives through flattering or hypocrisy similarly working towards self-absorbed group

Chimbuko la kuto kuhoji linaanzia kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukihoji kwenye ngazi hiyo utaambiwa kama umekua uondoke tabia hii ya kukataa kuhojiwa kwasasa imebebwa kwenye ngazi zote za maisha yetu iwe mashuleni, kanisani, vyuoni kwenye vyama vya siasa na kwingineko

Swali je tuliandaliwa kuto kuhoji jibu ni ndiyooo
 
Sawa ila kumfuatilia huyo jamaa ni kupoteza muda mkuu
 
Umesahaua kububujikwa na machozi.

Huyu sijui km ni mzima aisee hii sio normal Kwa mwanaume
Bado huyu ninaye nazitafakari nyuzi kama 39 hivi nazitengenezea uzi mwingine. Asante Ms Tayana-wog kwa kuongezea na hilo la kububujikwa na machozi nilitengenezea hoja na swali pia.

Hivi ni kweli jinsia ya kiume yenye maandiko kama haya inavutia wanawake?
 
Sawa ila kumfuatilia huyo jamaa ni kupoteza muda mkuu
Sio kumfuatilia ila maandiko yake ni ya kijinga sana na katika replies zote anaishia kutukanwa na maneno ya kejeli.

Kwanini asikutane na hoja kama hizi ili wengine wasome na kufaidika na kupata cha kuongeza ufahamu wao?
 
Maswali yako Yoote nilishayajibu humu jukwaani. Fungua maandiko yangu upate majibu ya maswali yako. Kwa sasa naandaa andiko zito kwa ajili ya kumjibu Polepole Humphrey
Umjibu polepole kwa hoja zipi? Wewe mjibu kinembe ndo mjinga wa hadhi yako. Vinginevyo wewe ni chawa
 
Back
Top Bottom