Maswali ambayo huwa najiuliza kuhusu maisha, destiny na “Kwa nini mimi?”

Discipline and a good attitude create the foundation for long-term success,

Discipline keeps you focused and consistent with your daily work,

A good attitude helps you overcome failures and work well with other people.
Uko sahihi kwa kiasi chake lakini inaweza tokea situation moja tu au mtu mmoja akafuck up your whole discipline and good attitude unayoisema ww
 
Hili ni swali zito sana la maisha. Kuna mambo mengi tunakuta tayari yameamuliwa kabla hata hatujapata uwezo wa kuchagua—tulizaliwa wapi, kwa nani, katika kipindi gani na katika mazingira gani. Ndiyo maana si rahisi kumhukumu mtu kwa alipo bila kuangalia safari aliyopitia. Lakini pamoja na tofauti hizo za mwanzo, bado tunayo nafasi ya kufanya maamuzi ndani ya mazingira tuliyokabidhiwa na kuacha alama yetu wenyewe katika dunia hii.
 
Majibu ya maswali haya ni kinyume chake, Kwa nini siyo wewe?
Kaa Jiulize tena "Kwa nini siyo Mimi". Majibu yote utajayoyapata yanakutafsiri wewe.
Nimekupata. Hilo la ‘Kwa nini siyo mimi?’ ni swali zito zaidi kuliko nilivyoliuliza.

Lakini nikigeuza swali na kusema ‘Kwa nini siyo mimi?’, najikuta nikitambua kwamba tofauti kati yangu na huyo mtu wakati mwingine ni mazingira tu ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyachagua.


Hata hivyo, bado najiuliza: je, jibu la ‘kwa nini siyo mimi?’ linatueleza sababu iliyofanya yeye apitie hayo na mimi nisipitie? Au linatufundisha tu kwamba sisi wote tulikuwa na uwezekano wa kuwa katika nafasi hiyo?
 
Uko sahihi kwa kiasi chake lakini inaweza tokea situation moja tu au mtu mmoja akafuck up your whole discipline and good attitude unayoisema ww
Soma paragraph ya mwisho kabisa kwenye hiyo comment uliyoiquote,

Unaweza kuanguka yes but utarudi tena kutokana na wewe ulivyojiweka.
 
Sio mara zote kuzaliwa sehemu fulani ndio kukaamua maisha yako yote,au kuzaliwa kwenye familia fulani ndio kukaamua future yako,

Kuna watu wamezaliwa kutoka kwenye familia masikini,kisha wakafight na kua matajiri wenye uwezo mkubwa,

Ukifuatilia historia za wacheza mpira wengi utaliona hilo,

Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya juu sana na kujitambua na kutambua unachokitaka,just never give up.
 
Kuna wakati nimejikuta nikifikiria sana kuhusu maisha ya mwanadamu na jinsi ambavyo kila mmoja wetu amekuja kuwa yeye.

Kwa nini mimi nimekuwa mimi?
Kwa nini wewe umekuwa wewe?
Na kama mambo machache tu yangekuwa tofauti, je, tungekuwa watu gani leo?
Wewe unayejitambua leo ni matokeo ya moja kwa moja ya matukio yaliyotokea baada ya wewe kuzaliwa na mazingira uliyokulia. Kama ungezaliwa kipindi cha Kristo au miaka 500 iliyopita, huyo asingekuwa wewe huyu wa sasa mwenye ndoto hizi. Unajua kwa nini? Ndoto zako za sasa zinasukumwa na teknolojia na utamaduni wa sasa. Miaka 500 iliyopita, ndoto kubwa ya kijana wa miaka yako ilikuwa ni tofauti kabisa na ndoto ulizo nazo wewe sasa ndio maana nasema, you are a product of your time. Usingekuwa na personality hii kwa sababu ubongo wako ungekuwa unachakatwa na taarifa tofauti kabisa.
Kwa nini Seran asingekuwa Ephe?
Kwa nini Mbaga Jr asingekuwa Min_Me?
Kwa nini Mo Dewji asingekuwa Alex Ferguson, na Alex Ferguson asingekuwa Nikola Tesla?
Kwa nini Yoda asingekuwa Albert Einstein, na Albert Einstein asingekuwa Lucas Mwashambwa?
Mkuu maisha kwa asilimia kubwa ni biological and social lottery. Mo Dewji asingeweza kuwa Alex Ferguson kwa sababu genetics na mazingira yao ni tofauti kabisa, iko hivi mazingira yanabeba asilimia kubwa sana ya destiny ya mtu. Mtoto anayezaliwa kwenye umaskini uliopitiliza hawezi kupata lishe bora, ubongo wake haukui vizuri kiakili, na hawezi kupata fursa sawa na mtoto wa tajiri anayepata kila kitu. Hii sio kwa sababu Mungu au ulimwengu unampenda huyu kuliko yule, bali ni matokeo ya mifumo ya kibinadamu ya kiuchumi, ninacho amini mimi umaskini au utajiri wa mtu tangu kuzaliwa kwake sio agizo la kiungu, bali ni matokeo ya mifumo ya jamii ulikotokea.
Ubongo wa binadamu umeundwa kwa ajili ya kuishi na kukabiliana na hatari, ki-biolojia, ubongo wetu huwa unajifunza haraka zaidi kupitia vitu vinavyoleta maumivu au tishio ili usirudie tena kufanya kosa lilelile. Ndio maana mtoto mdogo unaweza kumwambia pasi ni ya moto mara mia asielewe, lakini akiigusa mara moja tu akapata maumivu, hatakaa aguse tena maisha yake yote! Kwahiyo bila maumivu na makosa, hekima isingekuwepo kabisa duniani, tungekuwa viumbe wajinga sana kwa sababu tusingekuwa na uwezo wa kutofautisha uamuzi mzuri na mbaya.
 
1. Lakini nadhani kuna tofauti kati ya kusema “mazingira yanakutengeneza” na kusema “mazingira ndiyo yanakuamua.”


Kwa sababu kama tungekuwa products of our time kwa asilimia 100, basi watu wote waliozaliwa kipindi kimoja, kwenye culture moja na mazingira yanayofanana wangekuwa na personality, ndoto na outcomes zinazofanana. Lakini sivyo.


Ndiyo maana mimi naona maisha kama interaction kati ya kile tunachokikuta na kile tunachofanya nacho.


Wakati unatengeneza sehemu ya wewe, lakini wewe pia una uwezo wa kuamua utakachofanya na kile wakati wako umekupa.


Na hapo ndipo swali langu la “Kwa nini siyo mimi?” linakuwa na nguvu zaidi.


Kwa sababu pengine si swali la kwa nini sikuzaliwa kwenye mazingira fulani, bali ni: kwa mazingira niliyopewa, ni nini kinachonizuia kuwa mimi ninayetaka kuwa?


2.
hapo bado nisingesema mazingira ndiyo destiny yenyewe. Ningesema mazingira yanaweka probability na starting point.


Kwa mfano, kama watu wawili wanaanzia kwenye milango miwili tofauti, ukweli kwamba mmoja ana mlango ulio rahisi kufunguka hauondoi kabisa uwezo wa mwingine kubadilisha trajectory yake. Ni vigumu zaidi kwake, probability inaweza kuwa ndogo zaidi, lakini si sawa na kusema outcome yake tayari imeandikwa.


Na hapo ndipo mimi naona kuna distinction muhimu sana:


“Hatukuchagua tulipoanzia” ni kweli.


Lakini “kwa hiyo hatuwezi kubadilisha tunakoelekea” ni conclusion nyingine kabisa.


Kwa hiyo naamini maisha yana sehemu kubwa ya lottery, lakini ndani ya hiyo lottery bado kuna sehemu ya agency. Huwezi kuchagua cards ulizopewa, lakini unaweza kuwa na influence fulani kwenye namna utakavyocheza cards hizo.


Na pengine ndiyo maana swali la “Kwa nini siyo mimi?” lina maana kwangu — si kwa kudhani kila mtu ana starting point sawa, bali kwa kujiuliza: pamoja na cards nilizopewa, ni kiwango gani cha trajectory yangu bado kiko ndani ya uwezo wangu?
 
Watu wa aina hiyo ni "outliers", hata hivyo mfano wa wachezaji mpira sio sahihi sana kwa sababu mpira kwa kiasi kikubwa ni jambo la kipaji na mazingira, ndio maana India hakuna wachezaji mpira wa miguu.
 
Marcostilone
 
Watu wa aina hiyo ni "outliers", hata hivyo mfano wa wachezaji mpira sio sahihi sana kwa sababu mpira kwa kiasi kikubwa ni jambo la kipaji na mazingira, ndio maana India hakuna wachezaji mpira wa miguu.
Kila jambo linahitaji kipaji pia,hata kufanya biashara sio kila mtu anaweza kua mfanya biashara,

India haiwezi kutoa wacheza mpira coz sio mchezo wao pendwa ila huko India kuna watu walitoka familia masikini wakatajirika kwa kucheza Cricket au Movie Bollywood,

Hizo familia za kitajiri,hawakuzaliwa wakaukuta utajiri sebuleni bali kuna mtu alifight na akaendeleza wealth generation.
 
Kila jambo linahitaji kipaji pia,hata kufanya biashara sio kila mtu anaweza kua mfanya biashara,
Sio kila jambo linahitaji kipaji, huitaji kipaji kuwa dereva, mama ntilie, mwalimu, daktari. Huhitaji kipaji kuwa mfanyabiashara. Kila mtu hawezi kuwa mfanyabiashara ila watu wengi wanaweza kuwa wafanyabiashara na watu wengi ni wafanyabiashara. Ni watu wachache sana duniani wanaweza kuwa wachezaji mpira, wanamuziki, waandishi vitabu, mabondia au actors.

Mamilioni ya watu nchi hii wakiwekewa mazingira mazuri ya biashara wanaweza kufanya biashara kama Wachina ila watu wengi duniani hata uwawekee mazingira yenye kila kitu cha muziki, acting au michezo bado hawataweza kabisa kutoboa kuwa wachezaji, actors au waimbaji achilia mbali kuwa bora kata hayo maeneo.
 
Naona kama kawaida yako umejipanga kubishana,

Wewe mtaalamu weka comment yako na uachane na comment yangu coz hata hueleweki unachokiongea.
 
Mkuu ni kweli huwezi kuchagua kadi ulizogawiwa mkononi, lakini una uwezo wa kuamua uicheze vipi kila kete uliyo nayo ili ushinde mchezo.

Ukiligeuze swali lako kwamba kwa nini nimezaliwa hapa na sio kule linageuka moja kwa moja kuwa ni swali la kiuwajibikaji na siyo la kulalamika tena au kujionea huruma.

Jiulize hivi "Kwa mazingira niliyopewa na kadi nilizonazo mkononi sasa hivi, ni nini hasa kinachonizuia kuwa mimi ninayetaka kuwa?" unaona hili swali jinsi linavyokuondoa kwenye ule mtego wa kujiona mhanga wa mazingira na linakurudishia nguvu zote wewe?

Kimsingi hapa unakuwa umetengeneza uwiano mzuri sana kati ya kukubali uhalisia wa kikatili wa maisha kwamba kuna mambo hatuyadhibiti na wakati huo huo hutokata tamaa kwamba bado una namna nzuri unayoweza kufanya kwenye huo huo uhalisia wa kikatili wa maisha.

Ninachokieleza hapa kifupi ni kwamba trajectory ya maisha yetu, kwa asilimia kubwa, bado ipo mikononi mwetu licha ya wapi tulipoanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…