Hii ni haki mkuu kwan si kuna usafiri wa kuwatoa watu mbagala mpaka mbezi luis.
Lengo la usafiri wa umma ni kuwasaidia watu kurahisisha safari zao, lakini unapoweka mazingira kuwa magumu zaidi hapo hauwasaidii bali unawaumiza!
Unajua umbali uliopo kutoka mbagala mpaka mbezi Luis?! Hapo sijagusia maeneo ya ndani zaidi kama charambe, matitu, chamazi, mbande, kisewe, msongola, mvuti na chanika?!
Unajua umbali uliopo kutoka kongowe, kibada , mjimwema, kigamboni, mpaka mbezi Luis?!
Unajua umbali uliopo kutoka mwandege, kivule, kisemvule mpaka mbezi Luis?!
Kote huko hakuna basi la moja kwa moja mpaka mbezi stendi kuu, lazima upande madaladala mawili au matatu kufika mbezi bus terminal,
Hapo abiria anakwenda either moshi, arusha, tabora, singida, shinyanga, mwanza ,kigoma au kagera! Aamke saa tisa usiku kuwahi daladala kutoka kisemvule, asubiri ijae, bado hujagusia foleni, ashuke kariakoo au tandika, achukue daladala nyingine hadi mbezi , mtu huyu ana watoto na mizigo tele!
Hapo utakuwa umemsaidia urahisi wa safari yake au umemtwika mateso zaidi?! Serikali iliangalie hili upya kwa jicho la tatu. Wengi tulikuwa tunategemea urahisi wa kupandia stendi ndogo na ofisi ndogo za mabasi husika ya mikoani.