Mkuu
Kim Jong Jr kikubwa ni geographical position.
Stendi ya Train ipo center, posta ni kati ya jiji na kiukweli sio mbali sana ukiliiinganisha na Mbezi Louis hasa kwa kwawakazi wa maeneo ya mbagala , kigamboni, kongowe nk
Stand ya train iwe ya TRC au TAZARA, iko pale kwa muda mrefu , na usafiri wakufika pale unapatikana kw a uhakika sio ubabaishaji kama kutoka maeneo ya pembezoni mwa jiji hadi mbezi Louis,
Stend ya mabasi imekuwa haitabiriki ina hamishwa hamishwa kwa muda mrefu kwakigezo cha kuleta msongano,
Mimi sio mgeni hapa jijini Niko hapa kwa zaidi ya miaka 40 sasa, tulianza kupanda mabasi ya KAMATA, enzi hizo stend mkuu ya mabasi ikiwa pale kariakoo , gerezani kamata , traffic lights,
Wakaja wakaihamisha ile stendi ikapelekwa pale Mnazi mmoja , kwakigezo cha msongamano katikati ya jiji,
Ikaja kuhamishwa tena na kupelekwa pale kisutu, kwakigezo kuwa pale mnazi mmoja ni padogo kulingana na wingi wa watu na mabasi,
Napo pia ikahamishwa tena na kupelekwa Ubungo, kipindi hicho nilikuwa pembezoni mwa mji kama ilivyo mbezi Luis kwasasa,
Sijui na hapo mbezi Luis itakaa kwa muda gani kabla ya kuhamishwa tena?! Tatizo watu wa mipango miji wanashindwa nini kubuni eneo permanent kama stend za railways, au basi wajenge stendi hata mbili au tatu mfano iwepo mbagala, bunju na mbezi.