kiboboso
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 9,323
- 12,594
Mitano tenaKuna tatizo hapo imagine unashuka saa sita usiku na daladala hakuna na una mizigo mingi mikubwa!!!
Wenye mabasi kushusha ofisi zao ilikuwa ni huduma nzuri ya kumsaidia abiria
Kinachotakiwa kitamkwe ni kuwa basi zote zipitie stendi kuu kuanzia safari au kumaliza safari ziwe na abiria au la lazima zipitie ila kusema marufuku kuwa na abiria haliko sawa
Pili kuua hivyo vituo vingine vilivyokuwepo ni kuua ajira za mamia ya watu waliokuwa wakipata riziki zao kupitia hizo stendi ndogo kuanzia maduka teksi bodaboda bajaj wabeba mizigo mama lishe nk zingeachwa tu kama sehemu ya Transit kama ilivyo ndege tu kuwa stendi kuu ubungo stendi ndogo temeke Au mbagala au tegeta au kariakoo au ofisi juu ya basi nk ili kuondoa usumbufu kwa abiria .Sipati picha mtu anaishi mbagala anaenda mtwara aende mbezi kupandia gari kule wakati mfano mwenye gari ana ofisi kuu hapo hapo mbagala na basi linaanzia hapo kwenda mbezi kubeba abiria!!!!
Chukulia mfano basi zima wamekata tiketi watani zangu wamakonde wanaoishi mbagala wanaenda kwao basi linaanzia hapo hapo mbagala ofisi kuu ya basi .Kwa hiyo hao makonde wanatakiwa wapande daladala kwenda mbezi na hilo basi liende tupu hadi mbezi lipakie hao makonde kwenda nao mtwara!!! ni kituko badi watakalopanda liko mbeke yao tupu na wao wako kwenye daladala kwenda mbezi
Haya maamuzi mengine hayako sahihi