Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Sipati picha basi limetoka mtwara mtu anashuka Mbagala mwenye basi akifika mbagaka anaongeza mwendo anasema hakuna kushuka hapa lazima nikawashushe Mbez.

Au basi limetoka Moshi au Arusha watu wanashuka Tegeta dereva anaongeza moto kuwa hakuna kushuka lazima nikawsdhushe Mbezi maruhuni nyie hashishwi mtu hapa! Haturuhusiwi tumeambiwa lazima tuwashushe Mbezi.

Sipati picha kitakachomkuta dereva!!!!
 
Mitano tena
 
Katika ile mitano tena ndio kwanza tupo mwaka wa kwanza tena mwezi wa pili tu, mtanyooka.
 
Kuna njia pale kibamba ccm nasikia ina pigwa mkeka inatokea tgt sijui bunju, ila kama ujuavyo makampuni mengi ya mabasi yamefungua ofisi zao so usiwe na wasi wasi, kama zaman stand ilikuwa kisutu na watu walikuwa wanatoka mbagala hadi kisutu
 
Hii stendi ni yetu watu wa Kinondoni, haiwahusu watu wa Ilala wala Temeke. Wajenge zao
 
Twende tu Mbezi with time tutazoe. Ni sawa na kupanda ndege whether unakaa ukonga, kigamboni au Dodoma ukitaka usafiri utaufata Kipawa. Kuhusu daladala usiku ni fursa ya biashara kwa wenye daladala
 
Kuna njia pale kibamba ccm nasikia ina pigwa mkeka inatokea tgt sijui bunju, ila kama ujuavyo makampuni mengi ya mabasi yamefungua ofisi zao so usiwe na wasi wasi, kama zaman stand ilikuwa kisutu na watu walikuwa wanatoka mbagala hadi kisutu
Mbagala hadi kisutu mbona sio mbali mkuu,

Imagine mbagala hadi mbezi Louis?! Wengine wanatokea mbande, chamazi mpaka mbezi mwisho?!

Wengine wanatokea kongowe, mwandege, kigamboni, kibada, kisemvule mpaka mbezi Luis ?!

Ukifahamu fika hakuna route ya basi la moja kwa moja kutoka mbagala, mbande, chamazi, kongowe, kigamboni au kisemvule mpaka mbezi ?! Si mateso hayo?!

Hii sio haki ni unyanyasaji mkubwa!

Mabasi yaruhusiwe kupakia abiria kutoka ofisi zao ndogo lakini lazima yapitie stend kuu ya mbezi, na sio kuyazuia kabisa kupakia kwenye stand zao ndogo!
 
Gharama za usafiri zitapanda sana
Usumbufu kwa abiria utakuwa mkubwa
Usalama kwa abiria wa mbali utarudi
Foleni zitarudi upya maana njia zote hizo zitatumia kituo kimoja tuu
Zinahitajika stand kama hiyo Temeke/ Mbagal, Tegeta
 
Hii ni haki mkuu kwan si kuna usafiri wa kuwatoa watu mbagala mpaka mbezi luis.
 
Wadau ondoeni shaka!.

Hii kitu isiwaumize kichwa, jambo lolote likiwa jipya lazima liwe na usimamizi na kufuatiliwa kwa sababu macho yote yanaangalia hapo.

Muda, taratibu na mambo mengine yataendelea kama kawaida, mfano basi za Esta zina vituo Mbagala, Gongo la mboto, Kivule sijui Kigamboni abilia wote watapandia huko huko saa 11asubuhi na watakuja hapo mbezi na kuchukua wengine na kuondoka.

Pale Musoma ukiwa unakuja Dar unapanda JM Luxury saa 11asububi kule mkendo na kwenda stendi mpya kupakia abilia wengine, muda ukifika 12:00 mnaondoka.

Hayo mengine ni kuchangia mada tu ili tutoe ya moyoni but mfano halisi ni stendi ya Dodoma.

NOTE: Vaa barakoa na unawe mikono kwa sabuni na maji tiririka pia ukae mbali na mikusanyiko.
 
Vitaendelea kutoa huduma zote ila sio kupakia na kushusha abiria
Target ya serikali ni wakusanye mapato so bus zote lazima ziingie stand ziache hesabu na kukaguliwa kisha nadhani watapewa karisit kisha wataondoka na abiria wao kwenda wanakojua wao.
 
Hii ni haki mkuu kwan si kuna usafiri wa kuwatoa watu mbagala mpaka mbezi luis.


Lengo la usafiri wa umma ni kuwasaidia watu kurahisisha safari zao, lakini unapoweka mazingira kuwa magumu zaidi hapo hauwasaidii bali unawaumiza!

Unajua umbali uliopo kutoka mbagala mpaka mbezi Luis?! Hapo sijagusia maeneo ya ndani zaidi kama charambe, matitu, chamazi, mbande, kisewe, msongola, mvuti na chanika?!

Unajua umbali uliopo kutoka kongowe, kibada , mjimwema, kigamboni, mpaka mbezi Luis?!

Unajua umbali uliopo kutoka mwandege, kivule, kisemvule mpaka mbezi Luis?!

Kote huko hakuna basi la moja kwa moja mpaka mbezi stendi kuu, lazima upande madaladala mawili au matatu kufika mbezi bus terminal,

Hapo abiria anakwenda either moshi, arusha, tabora, singida, shinyanga, mwanza ,kigoma au kagera! Aamke saa tisa usiku kuwahi daladala kutoka kisemvule, asubiri ijae, bado hujagusia foleni, ashuke kariakoo au tandika, achukue daladala nyingine hadi mbezi , mtu huyu ana watoto na mizigo tele!

Hapo utakuwa umemsaidia urahisi wa safari yake au umemtwika mateso zaidi?! Serikali iliangalie hili upya kwa jicho la tatu. Wengi tulikuwa tunategemea urahisi wa kupandia stendi ndogo na ofisi ndogo za mabasi husika ya mikoani.
 
Yani basi linalala yard kwangu na abiria wa karibu wanakuja kupandia hapo nalo ni kosa.....
Mkuu kumbuka kuna ushuru (mara ya mwisho kuingia Ubungo pale nililipa Tsh 200 nahisi hii ya Mbezi watafanya 500) nitaulipa mimi abiria wa basi lako nikitaka kuja kuifata gari stand,na wewe kitendo cha driver wako kusaini mule ndani kwamba bus inatoka kuna salio ataacha pale.

Na akirudi mwendo ni huo huo aingie tena ndani kuacha salio,ni usumbufu mkubwa sana.
 
Mkuu tukitaka kila mtu kituo kiwe karibu na kwake tutafika kweli?

Katika inchi zilizoendelea stand kubwa itabaki kuwa moja tu ktkt mji husika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…