Maswali kuhusu Xiaomi

Maswali kuhusu Xiaomi

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Ndugu,

Hatimae nimefanikiwa kumiliki simu niliyokuwa ninaiota kwa muda, Mi 11 Lite 5G. Ndiyo ninayotumia kutype hapa. Sijaona changamoto zozote za kiutendaji kazi, ipo bomba balaa hasa spidi. Yenyewe ni ile ya RAM 6/128GB storage.

1. Ilibidi nimuagize mtu aliyekuwa anarudi nyumbani kutoka ulaya. Sikupenda kuagiza China, kwani huko kupata bidhaa ya kimataifa ni changamoto. Wao wanauza kwa matumizi yao,kwahiyo, ndani ya simu unakutana na maandishi ya kichinachina.

2. Ninachoshangaa ni kutokuona specifications za betri na camera ndani ya simu.Je, hili ni suala la kawaida? Tumezoea ukiingia setting, about the phone, unakuta hivi vitu. Hii hamna. Au kuna namna nyingine ya kucheki haya?

Kwahiyo, ukiniambia nikuhakikishie betri yangu au camera yangu ina sifa X, siwezi.

Kuna wakati napata mashaka. Lakini, kwakuwa sijaanza kupata shida, najipa moyo.

Wazoefu ninaomba maoni yenu tafadhali.
 
User Interface ya simu ndio inaweza kuwa na option ya kuona specs za simu hiyo. Sio kila interface inakubali kuonyesha. Hata kwa Xiaomi kuna baadhi zenye user interface inayoonyesha specs. Redmi 9C nadhani inaonyesha.

Ila sio tatizo, downlaod CPUz au Aida64 itakuonyesha specs zote.
 
Asante mkuu kwa kunitoa hofu. Hizi CPUz na Aida64 ni apps zinapatikana Play store? Matumizi yake yapoje? Ninaingia tu huko itanielekeza?
 
As

Asante mkuu kwa kunitoa hofu. Hizi CPUz na Aida64 ni apps zinapatikana Play store? Matumizi yake yapoje? Ninaingia tu huko itanielekeza?

Ziko free play store. Angalia Icon zake hapo na hiyo screenshot ya cpuZ Na hizo ni baadhi specs unazoweza kuziona.

Screenshot_20211006-154438~2.png


Screenshot_20211006-154259~2.png
 
nataka kuona picha zake yaani zilizopigwa kwa simu iyo napenda kumiliki iyo kitu
 
Ivi morogoro kuna Duka la vifaa vya Xiaomi? anaejua tafadhali anielekeze
 
User Interface ya simu ndio inaweza kuwa na option ya kuona specs za simu hiyo. Sio kila interface inakubali kuonyesha. Hata kwa Xiaomi kuna baadhi zenye user interface inayoonyesha specs. Redmi 9C nadhani inaonyesha.

Ila sio tatizo, downlaod CPUz au Aida64 itakuonyesha specs zote.
Ndugu, umenisaidia sana. Ninashukuru mno.Nilikosa raha kwa muda wa wiki hivi tangu nimepokea mzigo huu. CPU5 na AIDA64 zimenisaidia. Aida ndiyo imetoa taarifa nyingi zaidi kuliko CPU. Zote hazijaweza kutoa taarifa za Camera,lakini, walau sasa nimejua kuhusu battery na taarifa nyingine nyingi. Na zote zimeendana na specs nilizozitaka na kuziona kabla sijaagiza. After all, camera ipo njema ,nimeridhika.

N.B: Nimejidai kujiongeza, nimefanya zoezi hili kwa laptop pia. Safi sana!

Shukrani
 
Hapo chief umeeleza kitu sahihi maana hao jamaa wanachofanya nikucheza tu na akili ya kwetu
 
Kuna MI 11 lite na MI 11 lite 5G.

Hio yenye 5G mbele ni simu kali sana. Hio lite ni redmi note 10 pro iliochangamka.
Kwakweli.Mimi ni hii kutokuona hizo specs za camera na battery tu. Na ni mazoea ndo yameniponza. Vinginevyo mpaka sasa sijutii milioni yangu. Kitu kipo👌👌

Ila nimegundua. Simu inaweza kuwa ileile lakini ikatofautiana kulingana na region inakouzwa. Ndiyo maana kwenye maelekezo lazima wakwambie huduma hii inapatikana kwa watu wa eneo fulani tu.
 
Back
Top Bottom