Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,877
- 2,314
Ndugu,
Hatimae nimefanikiwa kumiliki simu niliyokuwa ninaiota kwa muda, Mi 11 Lite 5G. Ndiyo ninayotumia kutype hapa. Sijaona changamoto zozote za kiutendaji kazi, ipo bomba balaa hasa spidi. Yenyewe ni ile ya RAM 6/128GB storage.
1. Ilibidi nimuagize mtu aliyekuwa anarudi nyumbani kutoka ulaya. Sikupenda kuagiza China, kwani huko kupata bidhaa ya kimataifa ni changamoto. Wao wanauza kwa matumizi yao,kwahiyo, ndani ya simu unakutana na maandishi ya kichinachina.
2. Ninachoshangaa ni kutokuona specifications za betri na camera ndani ya simu.Je, hili ni suala la kawaida? Tumezoea ukiingia setting, about the phone, unakuta hivi vitu. Hii hamna. Au kuna namna nyingine ya kucheki haya?
Kwahiyo, ukiniambia nikuhakikishie betri yangu au camera yangu ina sifa X, siwezi.
Kuna wakati napata mashaka. Lakini, kwakuwa sijaanza kupata shida, najipa moyo.
Wazoefu ninaomba maoni yenu tafadhali.